Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 8/1 kur. 11-16
  • Washindi wa Ulimwengu kwa Imani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Washindi wa Ulimwengu kwa Imani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • ULE USHINDI KWA IMANI
  • MSHINDI ALIYE KIELELEZO
  • IMANI INAYOSONGEZA MILIMA
  • USHINDI UNAOENDELEA KWA IMANI
  • MAJARIBU ZAIDI YA IMANI
  • Kumwamini Mwana wa Mungu Kukuhusuje Wewe?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • “Imani Iliyotenganishwa na Matendo Imekufa Kama Mzoga”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Onyesha Imani Yako Katika Ahadi za Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
  • Ubora Uliojaribiwa wa Imani Waleta Uvumilivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 8/1 kur. 11-16

Washindi wa Ulimwengu kwa Imani

“Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.”​—⁠1 Yohana 5:4.

1, 2. (a) Wale ambao wangekuwa washindi wa ulimwengu wamepatwa na kitu gani? (b) Mshindi mmoja wa ulimwengu ametofautianaje na hawa wengine? (c) Ni kwa sababu gani ushindi wa Huyu na wafuasi wake hauna kifani?

HISTORIA yatueleza habari za watu wengi ambao wangaliushinda ulimwengu. Lakini mwishowe, wote hao wakapaswa kukubali ushinde. Farao hodari wa Misri, Nebukadreza wa Babeli mwenye majisifu, Aleksanda aliye Mkuu, wale Makaisari wa Rumi, Napoleon, Hitler​​—⁠utukufu wao ulikuwa wa muda mfupi sana! Walakini kuna mshindi mmoja wa ulimwengu ambaye utukufu wake hautafifia hata kidogo. Yeye hakujisifu kuwa na makundi ya mashujaa wenye silaha, wala vikosi vikubwa vya merikebu za vita. Lakini ushindi wake umekuwa kamili, kwa faida ya milele ya wale wanaoukubali ufalme wake.

2 Watu wengi walijikwaa juu ya mshindi huyo aliye hodari sana, kwa maana walimdhani kuwa mwana wa seremala maskini tu. Wananchi wenzake walimdharau. Wakati mamlaka ya Kirumi yenye kutawala nchi yao ilipomwua, wafuasi wake wachache walitawanyika. Lakini mtu huyo​—⁠Yesu Kristo​—⁠hana kifani kama mshindi wa ulimwengu. Katika jioni ya kuuawa kwake angeweza kuwaambia wanafunzi wake hivi: “Jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” (Yohana 16:33; Marko 6:3; Isa. 53:3) Zaidi ya hilo, alisema wao pia wangeushinda ulimwengu. Lakini namna gani? Ni kama vile alivyosema mmoja wa wafuasi wake wapendwa baadaye: “Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.”​—⁠1 Yohana 5:4.

ULE USHINDI KWA IMANI

3. Hii imani ishindayo ni kitu gani?

3 Ushindi huu wa kutumia imani ni ushindi wa namna gani? Kuwa na imani maana yake ni kusadiki sana sana mambo yasiyoonekana au mambo ya wakati ujao mpaka mambo hayo yanakuwa ni kama yametimia kabisa kwa mwenye kuyaamini. Imani ya kweli ya Kikristo, ambayo inatofautiana sana na kukubali mambo upesi upesi bila kufikiri kwa kutegemea mishtuko ya moyo au ushirikina, imejengwa juu ya msingi hakika wa Yesu Kristo. Hiyo haiharibiki, ni kama ‘dhahabu, fedha na mawe ya thamani.’ (1 Kor. 3:11-14) Inasadiki kwamba kuna Mungu yule mmoja aliye hai Yehova na kwamba yeye atakitetea cheo chake kama Bwana Mwenye Enzi Kuu wa ulimwengu wote. Imani hiyo nanga yake ni zile ahadi za Mungu “asiyeweza kusema uongo.” Inamkazia macho Yesu kama Mkamilishaji wake na kama Wakili Mkuu wa Mungu wa kutimiza makusudi Yake yote matukufu kuhusiana na ufalme wake.​—⁠Ebr.11:1, 6; 12:2; Tito 1:2.

4. Ni wakati gani na jinsi gani tunashinda kwa imani?

4 Maadamu tunashikamana na imani hiyo bila kuiacha kwa woga, tunaweza kusema kwamba tumeushinda ulimwengu. Hapana, si lazima tungoje mpaka Har–​Magedoni ifike ndipo tushinde hivyo. Tunajiondokea tukaushinde ulimwengu tunapogeuka na kuacha kuzifuata njia za ulimwengu, halafu kwa kuitegemea imani tuliyo nayo katika Bwana Yesu Kristo tunaweka maisha zetu wakf kwa Yehova na kupokea ubatizo wa maji. Hivyo tunashinda kwa imani. Walakini, huo ni ushindi ambao lazima tuuendeleze katika hali ziwazo zote, za uzuri au za magumu, kwa sababu ya kuuthamini upendo tulioonyeshwa na Yehova na Mwanawe.

5. (a) Tunawezaje kushinda “na zaidi ya kushinda”? (b) Ni uhakika gani ulio sehemu ya maana sana ya imani yetu?

5 Akiwasemea washindi wote hao, mtume Paulo anatangaza hivi: “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! ni dhiki, au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? .  .  . Katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.” Halafu, akitaja kwamba tunausadiki bila kuyumbayumba upendo usiotenganika ambao Yehova anatupenda, ulio sehemu ya maana sana ya imani yetu, anasema: “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na Upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”​—⁠Rum. 8:35, 37-39.

MSHINDI ALIYE KIELELEZO

6. Ushindi wa Yesu ulikuwa na msingi gani?

6 Alipokuwa duniani Yesu mwenyewe alionyesha namna tunavyoweza kuumaliza ushindi huo kwa imani. Yeye alilijua Neno la Mungu. Alilifurahia Neno hilo, akawa fundi wa kulitumia kama ‘upanga wa roho.’ (Efe. 6:17) Alipokuwa akijaribiwa na Shetani jangwani, mara tatu alimpinga mpinzani huyo, akisema, “Imeandikwa.” Ushindi wake ulitegemea kushikamana na Neno la Mungu. Basi lazima wetu ulitegemee pia.​—⁠Mt. 4:3-11.

7. Yesu alianzaje shughuli yake ya ushindi?

7 Kazi ya Yohana Mbatizaji ilipofikia mwisho, Yesu aliondoka akaifanye shughuli (kazi) yake kuu ya ushindi. “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na husema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” (Mt. 4:17) Ujumbe wenye kushtua watu loo! Hakika ufalme wa Mungu ulikuwa karibu, maana Yesu mtiwa mafuta mwenyewe alikuwa hapo. Katika Galilaya yote, katika jimbo ya Kirumi la Perea na moja kwa moja kuuingia Yerusalemu wenyewe, Yesu alizihubiri habari za furaha akiwa mshindi wa ulimwengu na Masihi. Maelfu walisikiliza. Wengi wakawa wafuasi wake. Lakini jamii ya watawala, na hasa viongozi wa dini, wakawa wapinzani wake wenye uchungu.

8. Ni jambo gani linaloonyesha kwamba Yesu hakuyumbayumba katika ushindi wake?

8 Yesu hakuyumbayumba katika ukamilifu wake, kwa maana alijua lazima awe mshindi mpaka mwisho. Alipoelekeana na kifo mwishowe juu ya mti wa mateso naye liwali wa Kirumi akamtolea ulizo la mashaka juu ya ufalme wake, angeweza kujibu hivi: “Wewe mwenyewe unasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa ajili ya hilo mimi nimezaliwa, na kwa ajili ya hilo nimekuja ndani ya ulimwengu, ili niitolee ile kweli ushuhuda. Kila mtu aliye upande wa ile kweli hunisikiliza sauti yangu.” (Yohana 18:37, NW) Kwa uaminifu, aliendelea kuishuhudia kweli ya Ufalme. Mpaka mwisho yeye hakusita-sita kulijulisha jina la Baba yake, naye alilitakasa jina hilo lenye thamani hata alipotupiwa mashutumu ya kila namna na Shetani. Hivyo, akiwa mshindi wa ulimwengu, Yesu angeweza kupaza sauti kwa kukata pumzi kwamba: “Imekwisha [yaani, kazi ya Mungu]”!​—⁠Yohana 19:30; 17:6, 20.

IMANI INAYOSONGEZA MILIMA

9. Wanafunzi wa Yesu wangeweza kuwa na imani ya namna gani, nao walipataje kuwa nayo?

9 Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” (Mt. 17:20) Hivyo ndivyo ingewatukia wanafunzi wake? Eh, ndiyo! Na sana sana siku ya Pentekoste mwaka 33 W.K. Kwa maana huo ndio wakati, siku ya hamsini tangu kufufuliwa kwa Yesu kwenye uzima wa roho, mwujiza ulipotokea kati ya wanafunzi wake 120 waliokuwa wamekusanyika katika nyumba fulani Yerusalemu. Roho ya Yehova ilimiminwa juu yao, ikawapa uwezo wa kunena kwa lugha nyingi juu ya “matendo makuu ya Mungu.”​—⁠Matendo 2:1-11.

10, 11. (a) Wanafunzi wa Yesu walianzaje kushiriki katika ushindi wake? (b) Kwa sababu gani imani yao ilikuwa imani ishindayo mambo yote?

10 Roho ilimpa Petro pia uwezo wa kueleza maana ya hayo yote kwa kutumia Neno la Mungu. Yesu alikuwa amepewa thawabu ya ushindi wake kwa kuinuliwa kwenye mkono wa kuume wa Mungu mbinguni. Sasa lilikuwa pendeleo lao kuushiriki ushindi wake. Walianza kuushiriki kwa kulipa ushuhuda mwingi sana kundi la watu lililokusanyika, wakiwahimiza sana watubu, wabatizwe na kuzikubali ahadi tukufu za Ufalme walizotolewa kupitia kwa Neno la Mungu. “Siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu,” nao wakaendelea kufanywa wenye nguvu katika imani kupitia kwa mafundisho ya kila siku yaliyotolewa katika eneo la hekalu lenye nafasi kubwa, na vilevile katika nyumba za watu wenyewe.​—⁠Matendo 2:14-47.

11 Je! viongozi wa dini walipendezwa na wonyesho huu wa wazi wa imani? Wapi! Kinyume chake, waliwakamata Petro na Yohana, wakadai kwa nguvu wakome kuhubiri na kufundisha kwa jina la Yesu. Likawarudia jibu la mitume hao lenye kujaa imani: “Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.” Hawangeacha cho chote kiizuie imani yao yenye kushinda vyote. Walipofunguliwa waliendelea kuutoa ushuhuda kwa nguvu nyingi!​—⁠Matendo 4:18-21, 33.

12. (a) Ni tegemezo gani la malaika lililodumisha ushindi wa wanafunzi hao? (b) Kuwa kwao na roho takatifu kulitegemea nini?

12 Kwa kujawa na wivu, kuhani mkuu na kundi lake sasa wakaagiza mitume wote watupwe gerezani. Jambo hilo likahitaji hatua ya kimungu. Usiku malaika wa Yehova aliwatoa nje tena akawaambia wakaendelee ‘kuwaambia watu maneno yote ya Uzima huu.’ Kulipopambazuka, ndio hao tena, wakifundisha katika eneo la hekalu! Kwa mara nyingine wakakamatwa wakapelekwa ndani ya jumba la Sanhedrin, na humo kuhani mkuu akatamka hivi: “Je! hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina [la Yesu], nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu.” Jibu la mitume hao likasikika kwa ushujaa: “Imetupasa kumtii Mungu [kama mtawala, NW]— kuliko wanadamu. .  . . Sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na [roho takatifu ambayo] Mungu amewapa wote wamtiio [kama mtawala, NW]—.” (Matendo 5:17-32) Ndiyo, kuwa kwao na roho takatifu kulitegemea kuendelea kwao kutoa ushuhuda kwa juhudi juu ya Enzi Kuu ya Yehova!

13. Katika siku hizo za mwanzo-mwanzo wa Ukristo, imani ishindayo ilipata kushindaje?

13 Viongozi hao wa dini walitaka kuwaulia mbali mitume, lakini Mpaji wa roho takatifu aliongoza mambo akayaelekeza katika njia tofauti. Gamalieli mwalimu wa Torati mwenye kuheshimiwa alinena maneno haya: “Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.” Kwa hiyo wakawapiga mitume na basi, wakawaambia wache kuhubiri kisha wakawaacha waende zao. Je! hapo imani ishindayo ilikuwa inashinda? Hakika ilikuwa inashinda, kwa maana maandishi yanaendelea kusema hivi: “Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.”​—⁠Matendo 5:33-42.

USHINDI UNAOENDELEA KWA IMANI

14. Yajapokuwako mateso, unabii wa Yesu katika Matendo 1:8 ulitimizwaje?

14 Ushuhuda huo ulio kamili haukupasa uache kutolewa. Ilikuwa lazima utolewe kwa kadiri ambayo Yesu mwenyewe alitabiri​—⁠“katika Yerusalemu na katika Yudea yote na Samaria na kwenye sehemu ya mbali zaidi ya dunia.” (Matendo 1:8, NW) Mateso yalisaidia kueneza ushuhuda tu, kwa maana “wale waliokuwa wametawanyika walikwenda wakapita katika nchi wakizitangaza habari njema za lile neno.” (Matendo 8:1, 4, NW) Baada ya muda mfupi mtesi Sauli akawa mtume Paulo, nao Mataifa wa kwanza wakaipokea zawadi ya roho takatifu. Habari njema zilienea kama moto-mwitu zikaingia katika maeneo mapya mengi zaidi na zaidi. Paulo na wenzi wake walipokuwa wakiingia Ulaya, wapinzani huko walipaza sauti wakisema, “Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako.” (Matendo 17:6) Hivyo, baada ya kupita yapata miaka 3 ya kuutolea Ufalme ushuhuda, habari njema ‘zilihubiriwa katika uumbaji wote ulio chini ya mbingu.’ ​—⁠Kor. 1:23, NW.

15. Wale walioyumbayumba katika imani yao walisaidiwaje na kutiwa moyo?

15 Walakini, mwisho wa taratibu ya mambo ya Kiyahudi ulipokuwa ukikaribia, inaonekana kwamba wengine Wa Wakristo hao walianza kuchoka. Waliacha kesha lao la kiroho wakaanza kuyumba-yumba katika ushindi wao wa kutumia imani. Lakini hawakuwa bila msaada. Wazee waaminifu katika kundi la Kikristo waliwapa kipa-moyo walichohitaji. Mmoja wao, mtume Paulo, aliendelea kuwahimiza wavumilie katika imani. Aliwatia moyo walifanye tumaini lao la Kikristo liwe “nanga ya nafsi, iliyo hakika na imara pia.” (Ebr. 6:19, NW) Alitamka hivi: “Sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa [nafsi] zetu.” (Ebr. 10:39) Walipaswa wamalize ushindi wao wa Kikristo vyo vyote iwavyo! Wale walioshikamana sana na imani yao waliokoka wakati “taratibu ya mambo” ya Kiyahudi ilipopotelea mbali mwaka 70 W.K.

MAJARIBU ZAIDI YA IMANI

16. (a) Mtume Yohana alivumilia katika ushindi wake kwa imani kwa muda gani? (b) Yeye alitoa onyo juu ya kitu gani?

16 Walakini, majaribu zaidi ya imani yalikuwa bado yatakuja kuwapata Wakristo washikamanifu. Yohana, aliyetumikia kama mtume wa Yesu Kristo zaidi ya miaka ipatayo 68, anayataja majaribu hayo. Katika mbili za barua zake, Yohana anaonya juu ya “mpinga Kristo” anayetokea katika “wakati wa mwisho,” naye amtambulisha kuwa ndiye “yeye amkanaye Baba na Mwana.” Halafu Yohana anamhusianisha huyo “mpinga Kristo” na “manabii wa uongo wengi [ambao] wametokea duniani.” (1 Yohana 2:18; 22; 4:1-3) Bila shaka huyo mpinga Kristo alibisha kwamba hakukuwa na haraka ya kuzihubiri “habari njema” akajaribu kugeuza Wakristo wazielekee njia za ulimwengu za utafutaji wa mali na anasa.

17. Lazima Wakristo wavumilie kwa namna gani na kwa sababu gani katika imani yao?

17 Wakristo wenye kushika ukamilifu walikuwa ‘wamemshinda yule mwovu,’ lakini sasa, hata baada ya muda mwingi kupita, imani yao ilitiwa hatarini kutokea upande mwingine. Mtume aliwaandikia hivi kwa maneno ya wazi: “Msiwe mkiupenda ama ulimwengu ama vitu vilivyomo katika ulimwengu. Ikiwa ye yote aupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake; kwa sababu kila kitu kilichomo katika ulimwengu-tamaa ya mwili na tamaa ya macho na mtu kujionyesha mali zake​—⁠hakitokani na Baba, bali chatokana na ulimwengu. Tena zaidi ya hapo, ulimwengu unapitilia mbali na ndivyo na tamaa yake, lakini yeye afanyaye mapenzi ya Mungu abaki milele.” (1 Yohana 2:13, 15-17, NW) Kwa kweli, hayajawa hata kidogo mapenzi ya Mungu Wakristo wachangamanike katika njia za ulimwengu wa Shetani za ufisadi na utafutaji wa mali. Bali, lazima wavumilie katika kushinda kwa kutumia imani.

18. Sisi tunatimizaje ushindi wetu kwa kutumia imani?

18 Katika barua iyo hiyo, Yohana anaeleza kifungo kinachofungamanisha Wakristo wote ulimwenguni pote katika umoja usioweza kugawanywa, akisema: “Ye yote afanyaye ungamo kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu, Mungu abaki katika umoja na mtu huyo na yeye katika umoja na Mungu. Na sisi wenyewe tumepata kujua nasi tumeuamini upendo ambao Mungu anao katika habari yetu. Mungu ni upendo, na yeye abakiye katika upendo abaki katika umoja na Mungu na Mungu abaki katika umoja na huyo.” (1 Yohana 4:15, 16, NW) Lo! namna lilivyo pendeleo kubwa kuwa na umoja na Mwenye Enzi Kuu wa ulimwengu wote kupitia kwa Mwanawe, Yesu Kristo, Yule ambaye damu yake “yatusafisha dhambi yote”! (1 Yohana 1:7) Humo ndimo mlimo ushindi wetu wa kutumia imani, yaani: Kuendelea kumpenda Mungu na Kristo, kuwa wafanya kazi wenzao katika ile kazi ya mavuno ya ulimwenguni pote ambayo sasa inakaribia kumalizika mbio-mbio. ​—⁠1 Kor. 3:9.

19. Ni kitu gani kinachotambulisha washindi wa ulimwengu kwa imani?

19 Yohana anaendelea kusema hivi: “Huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake.” (1 Yohana 5:3) Kwa habari hiyo Yesu aliwaambia wafuasi wake hivi: “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.” (Yohana 13:34) Hiyo ilipata kweli kweli kuwa alama yenye kutambulisha Wakristo siku za Yohana, nayo imekuwa alama ya kuwatambulisha ajabu katika siku zetu! Kwa maana katika historia yote ya wanadamu hakujapata kuwako duniani watu walio sawa kabisa na mashahidi Wakristo wa Yehova​—⁠wenye umoja katika kifungo cha upendo unaovishinda vizuizi vyote vya lugha, kabila na taifa.

20. Katika wakati huu wa mwisho wa ulimwengu, wewe unaweza kujionyeshaje kuwa mshindi wa ulimwengu?

20 Vilevile, kwenye mwisho wa taratibu hii ya mambo, kuna ile amri iliyo katika unabii wa Yesu kwamba “habari njema hizi za ufalme zitahubiriwa katika dunia yote inayokaliwa na watu kwa ushuhuda kwa mataifa yote; na ndipo ule mwisho utakapokuja.” (Mt. 24:14, NW) Ushuhuda huo mkubwa, ambao sasa unafikia upeo wake duniani pote, umesaidia kutambulisha wale ambao wameushinda ulimwengu. Kwa habari ya watumishi wote hao wa Mungu wenye kushika ukamilifu, mtume anaandika hivi: “Na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu, ni Mwana wa Mungu?” Kuamini hivyo kwamba Yesu ndiye Mwana wa Mungu kwaweza kuonyeshwa hata leo hii kwa kuitii kwa bidii amri ambayo Yesu aliwapa wafuasi wake akiwaaga: “Kwa hiyo nendeni mkafanye wanafunzi wa watu wa mataifa yote.” Kwa hiyo, je! wewe unajionyesha hivyo kwamba wewe u mshindi wa ulimwengu?​—⁠1 Yohana 5:4, 5; Mt. 28:19, NW.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki