Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 1/15 kur. 3-10
  • Sababu Gani Jumuiya ya Wakristo Haitaokoka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu Gani Jumuiya ya Wakristo Haitaokoka?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • TUMAINI LILILOWEKWA MAHALI PABAYA—KATIKA HIRIZI YA KIDINI
  • KUTOKA UTAKATIFU WA KIDINI MPAKA UCHAFU WA KIDINI
  • DHABIHU ZINAZOMPENDEZA YEHOVA MUNGU
  • Wakisema “Amani” Wakati Haipo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Katiwa Nguvu Kunena Maneno ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Njia ya Uzima au Njia ya Mauti—Njia Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Yehova—Tumaini Letu la Kuingia Taratibu Mpya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 1/15 kur. 3-10

Sababu Gani Jumuiya ya Wakristo Haitaokoka?

“Tazama, wamelikataa neno la [Yehova]; wana akili gani ndani yao? . . . tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.”​—Yer. 8:9, 10.

1. Kwa sababu gani si, ajabu kwamba Yerusalemu itakatisha tamaa kama kitu cha kuleta amani?

YERUSALEMU wa leo, mji unaotunukwa (unaoonwa kuwa wa thamani kubwa) na dini tatu kubwa za ulimwengu huu, unaelekea tena kuwa na sehemu kubwa katika mambo ya ulimwengu. Je! bado utajionyesha kuwa mji wa Mfalme wa Amani? Je! bado utajionyesha kuwa wa maana katika kuleta amani ya ulimwengu? Katika mambo haya utakatisha tamaa wale wanaoushikamanisha na thamani kubwa ya kidini. Hili halipaswi kuonekana kuwa jambo geni kwetu, kwa kuwa hata Yerusalemu wa kale ulimkosea Mungu yule yule ambaye hekalu lake lenye utukufu lilisimama kwa sifa juu ya Mlima Moria, mojawapo wa vilima vyake vyenye kujulikana sana.

2. (a) Twaweza kukosa nini kwa kuwasikiliza wanenaji wa Jumuiya ya Wakristo? (b) Yehova ametokeza nini ili kuionya Jumuiya ya Wakristo?

2 Na tusiwe kati ya wale ambao leo huchukua mwendo unaoongoza kwenye kukatisha tamaa kusikoepukika. Jumuiya ya Wakristo, ambayo huweka matumaini makubwa katika Yerusalemu wa kisasa, kwa muda mrefu imekuwa na sauti yenye kuamrisha katika mambo ya kidini na kisiasa. Ijapokuwa sifa yake, twaweza kupoteza uzima wa milele tunaotamani iwapo tunasikiliza yale ambayo wanenaji wake wanasema katika wakati huu wa hatari zaidi sana wa historia yote ya kibinadamu. Kulingana na Neno lisilokosea la Mungu ambaye Jumuiya ya Wakristo inadai kumwabudu, taratibu hiyo ya Ukristo wa kujidai, wa jina, imehukumiwa maangamizi, kama vile Yerusalemu wa siku za Yeremia. (Yer. 6:1-8) Kupitia kwa watu waliojiweka wakf kabisa kwa Mungu kama alivyokuwa Yeremia, Jumuiya ya Wakristo imekwisha kuonywa ipasavyo juu ya uharibifu hakika unaoingojea. Ndivyo, kama vile ilivyokuwa katika siku za mwisho za Yerusalemu katika siku za Yeremia, Yehova Mungu ametokeza mashahidi wake watiwa mafuta wawe jamii ya kisasa ya Yeremia. (2 Nya. 36:15, 16) Yehova amewatuma kwa ukawaida hawa mashahidi wake Wakristo kwa washiriki wa makanisa ya Jumuiya ya Wakristo kana kwamba ‘akiamka mapema kila siku, na kuwatuma.’ (Yer. 7:25, 13) Walakini yote imekuwa kazi bure!

3. Ni kiolezo (mfano) gani cha kuitika maonyo hayo ambacho “manabii” na “makuhani” wa Jumuiya ya Wakristo wamefuata?

3 Walakini, “manabii” na “makuhani” wa Jumuiya ya Wakristo wamekataa kusikiliza. Hawataki “kondoo” wao wakisumbuliwa. Kwa hiyo wanawapatia mahakikisho ya uongo ambayo yanaufanya unabii wa Mungu kuonekana kuwa wa uongo. Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Yeremia. Ndivyo ilivyokuwa katika siku za mitume wa Kristo. (Yer. 5:20, 21; Mt. 13:13-15; Matendo 28:25-27) Je! twataka kuwa kama watu hao walioongozwa vibaya na kukataa kusikiliza? Hapana!

TUMAINI LILILOWEKWA MAHALI PABAYA—KATIKA HIRIZI YA KIDINI

4, 5. (a) Watu wa Jumuiya ya Wakristo leo wanaweka tumaini leo katika taratibu ya namna gani? (b) Yeremia anawasimuliaje watu waliofanya kosa ilo hilo katika siku zake?

4 Leo mamilioni ya watu huweka tumaini lao katika taratibu ya kidini iliyohukumiwa maangamizi. Viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo wanashawishi washiriki wao wa kanisa wafanye hivyo. Watu wa Yerusalemu na wa nchi ya Uyahudi walifanya kosa kama hilo katika siku za Yeremia. Hatutaki kuwaiga. Yeremia aliamriwa na Yehova asimame katika lango la hekalu la Yerusalemu na kuwaambia waziwazi wale waliokuwa wakija humo hivi:

5 “Msitumainie maneno ya uongo, mkisema, Hekalu la [Yehova], Hekalu la [Yehova], Hekalu la [Yehova] ndiyo haya. . . . Angalieni, mnatumainia maneno ya uongo, yasiyoweza kufaidia. Je! mtaiba, na kuua, na kuzini, na kuapa kwa uongo, na kumfukizia Baali uvumba, na kuifuata miungu mingine ambayo hamkuijua; kisha mtakuja na kusimama mbele zangu katika nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, na kusema, Tumepona; ili mpate kufanya machukizo hayo yote? Je! nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, imekuwa pango la wanyang’anyi machoni penu? Angalieni, mimi, naam, mimi, nimeliona jambo hili, asema [Yehova].”​—Yer. 7:4:11.

6. Yesu alitumia maneno ya Yeremia kwa habari ya hekalu la Yerusalemu wakati wa tendo gani?

6 Yeremia hakupewa mamlaka ya kulisafisha hekalu kutokana na vitu vyote vyenye kuchafua vilivyowekwa humo na wale waliounganisha ibada ya Yehova na ibada ya kipagani ya kuabudu sanamu. (Yer. 7:20, 31) Walakini zaidi ya miaka 630 baada ya kuharibiwa kwa hekalu hilo Yesu Kristo, akiwa Mwana wa Mungu, alilisafisha pindi mbili hekalu lililojengwa upya la Yerusalemu. Alipokuwa akifanya hivyo, Yesu alitumia maneno aliyosema Yeremia. Twasoma hivi: “Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.” (Mt. 21:12, 13; tazama pia Yohana 2:15, 16) Hekalu hilo lililochafuliwa liliharibiwa katika mwaka 70 W.K.

7. (a) Wakati ule ule ambao wanadini wa Jumuiya ya Wakristo wanaendeleza ibada yao, wanabadili taratibu yao ya kidini kuwa nini? (b) Wanamwitaje Yesu Kristo, naye bado atawaitaje?

7 Sana sana tangu mwaka 1919 W.K. jamii ya Yeremia ya kisasa imekuwa ikivuta fikira za ulimwengu kwenye hali iliyochafuliwa ya Jumuiya ya Wakristo. Wakati ule ule washiriki wa kanisa wanapofanya ibada yao katika taratibu hii ya mambo inayojidai kuwa ya Kikristo, wanashiriki katika ‘kuiba, na kuua, na kuzini, na kuapa kwa uongo.’ Kwa njia ya kidini wanatoa dhabihu kwa miungu wengine (Mabaali, Mabwana) pamoja na kwa Yesu Kristo. Kwa njia ya mali wanageuza taratibu yao ya kidini kuwa “pango la wanayang’anyi.” (Yer. 7:9-11) Yajapokuwa mambo haya yote yanayomchukiza Yehova, wanadini wa Jumuiya ya Wakristo wanamtolea Yesu Kristo utumishi wa mdomo na kumwita yeye “Bwana.” Wanafikiri kwamba kwa sababu ya kufanya hili kila kitu ni sawa na kwamba ibada yao inakubaliwa na Mungu na Kristo. Walakini Yesu Kristo atawashangaza kwa kuwaita ‘watenda maovu,’ kwa sababu ya wao kutofanya mapenzi ya Baba yake.​—Mt. 7:21-23.

8. Ni kwa sababu gani wanadini wa Jumuiya ya Wakristo wanadhani kwamba taratibu yao ya kidini ina uzima wenye kulindwa na hirizi?

8 Kama vile Waisraeli wale ambao Yeremia aliwapa ujumbe wa Yehova, wanadini wa Jumuiya ya Wakristo huliona “hekalu” lao, wanaloliita kwa jina la Kristo, kama kwamba ni hirizi ya kuzuia msiba kutoka kwa Mungu. Wanaonyesha taratibu yao ya mambo iliyo kwa jina la Kikristo na kusema: “Hekalu la [Yehova] ndiyo haya.” (Yer. 7:4) Kanisa la Rumi Katoliki hudai kuwa la kimtume kwa kufanyiza nasaba (mfuatano) ya warithi wa kimtume kurudi nyuma mpaka kwa mitume kumi na wawili wa Kristo. Kanisa la Anglikana la Uingereza linafanya jambo kama ilo hilo kwa habari ya “maaskofu” (viongozi wa kidini wa kiaskofu). Wazee wa Makanisa ya Mashariki ya Orthodoksi hutegemea mfuatano wenye kuendelea wa kuwazia wa maaskofu wao kurudi nyuma mpaka wale mitume kumi na wawili, ambao, wanabisha, walikuwa na warithi wa kimtume. Upapa wa Rumi hushikilia kwamba msingi wake ni mtume Petro akiwa “mwamba huu” na kwa hiyo ‘milango ya hell’ haiwezi kuushinda. (Mt. 16:18, 19, Douay) Kwa sababu ya madai ya namna hiyo ya kuendelea kwa mambo kuanzia siku za Kristo mwenyewe, wanaiona Jumuiya ya Wakristo kuwa yenye maisha yanayolindwa na hirizi, yasiyoweza kuangamizwa.

9, 10. (a) Ni ulizo gani linalotokea juu ya waabudu wanaotumaini ‘uzima wenye hirizi’ wa Jumuiya ya Wakristo? (b) Yehova alimwambia Yeremia aseme nini juu ya Wayahudi waliolitumaini hekalu lao?

9 Hata hivyo, iwapo mtu anaweka tumaini lake katika ‘maisha yaliyo na hirizi’ ya Jumuiya ya Wakristo, je! hii inamhakikishia usalama kutokana na msiba na kuharibiwa kwayo? Mtume Paulo anaonya kwamba katika “siku za mwisho” watu wangekuwa “wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake;” akaongeza, “hao nao ujiepushe nao.” (2 Tim. 3:1-5) Hivyo, basi, wakati mtu anapohitimu katika mafunzo ya ki-nje-nje katika nyumba au chuo kinachodaiwa kuwa kimewekwa wakf kwa Mungu walakini wakati ule ule kimechafuliwa kwa kuchanganywa na ibada ya uongo na uulimwengu, je! hili linamhakikishia kulindwa kutokana na wonyesho wa haki wa Mungu wa kutopendezwa? Basi, Yehova alimwambia Yeremia awaambie nini Waisraeli waliotumaini “hekalu” lao? Sikiliza:

10 “Enendeni sasa hata mahali pangu palipokuwapo katika Shilo [yapata maili 20 (kilomita 32) kaskazini mwa Yerusalemu], nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone niliyopatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli. Na sasa, kwa sababu mmezifanya kazi hizi zote, asema [Yehova], nami nikasema nanyi, nikiamka mapema na kunena, lakini hamkusikia; nami nikawaita wala hamkuniitikia; basi, nitaitenda nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, mnayoitumainia, na mahali hapa nilipowapa ninyi na baba zenu, kama nilivyopatenda Shilo. Nami nitawatupa ninyi mbali na macho yangu, kama nilivyowatupa ndugu zenu wote, yaani, wazao wote wa Efraimu.”​—Yer. 7:12-15.

11. Katika siku za Samweli, ni nini kilichotukia Shilo ambacho kiliwashtua watu wenye kuchukua dini kwa wepesi wa Kiisraeli?

11 Jambo ambalo liliupata Shilo katika siku za nabii kijana Samweli liliwashtua watu wa kidini wenye kuchukua mambo kwa wepesi wa Kiisraeli. Walilitumaini sanduku takatifu la agano liwaokoe wasishindwe na Wafilisti. Kwa hiyo lilichukuliwa kutoka Patakatifu Zaidi pa hema lililokuwa Shilo, na makuhani wenye kuvunja sheria, wana wa kuhani mkuu Eli, walilichukua vitani. Walakini Sanduku hili halikuwalinda kutokana na matokeo ya kuvunja kwao sheria ya Yehova. Ole! wao, Sanduku hilo lilitwaliwa na Wafilisti Wapagani, wana wa kikuhani wa Eli, Hofni na Finehasi waliuawa, na, alipopata habari hizo za kuhuzunisha, kuhani mkuu aliyenenepa Eli alizimia akaanguka nyuma, akavunja shingo yake akafa. Waisraeli waliendelea kuonewa na Wafilisti, na Sanduku hilo, lililofananisha kuwapo kwa Yehova, halikurudi tena kamwe mahali pake katika hema takatifu katika Shilo, hata ijapokuwa lilirudishwa na Wafilisti wenye kuabudu sanamu waliopata pigo.​—1 Sam. 3:1 mpaka 7:2.

12. Yehova aliufanyaje Yerusalemu na nchi ya Yuda kama vile alivyokuwa ameufanya Shilo wenye kibali wakati mmoja?

12 Kupitia kwa Yeremia, Yehova alionya kwamba angeufanya Yerusalemu kama vile alivyoufanya Shilo uliokuwa na kibali wakati mmoja. Kwa hiyo aliwaruhusu Wababeli wauharibu Yerusalemu katika mwaka 607 K.W.K. Hata lile hekalu ambalo Mfalme Sulemani alikuwa amelijenga ambamo sanduku la agano liliwekwa liliharibiwa. Sanduku lenyewe lilitoweka (lilipotea) katika kumbukumbu lote, lilipo hapajulikani leo. Baada ya msiba huu juu ya Shilo, Wafilisti waliwaruhusu Waisraeli wakae hapo. Walakini baada ya Wababeli kuuharibu Yerusalemu na hekalu lake, waliwahamisha wengi wa Wayahudi waliookoka mpaka Babeli iliyokuwa mbali sana. Wayahudi wachache walioachwa waliiacha nchi hiyo mwishowe kwa woga mwingi na kukimbilia Misri. Hii ikaacha nchi yote ya Uyahudi pasipo wakaaji. Kwa njia hiyo Yehova aliwatupa Wayahudi hao wenye kuvunja agano kutoka mbele ya uso wake!

13. Twapaswa kujifunza somo gani kutoka kwa kisa hicho cha kuweka tumaini mahali pabaya?

13 Ebu leo na tujifunze somo kutokana na haya. Na tusiweke tumaini letu katika kile ambacho viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo wanadhani kitawaokoa kutokana na uharibifu. “Dhiki kuu” ambayo karibuni itakuja juu yake itakuwa mbaya zaidi ya ile iliyoupata Yerusalemu na hekalu lake miaka 37 baada ya Yesu kusafisha kile kilichokuwa kimegeuzwa kuwa “pango la wanyang’anyi,” hekalu lililochafuliwa la Yerusalemu.​—Mt. 24:1, 2, 21, 22.

KUTOKA UTAKATIFU WA KIDINI MPAKA UCHAFU WA KIDINI

14. Sababu gani hatupaswi kumwomba Mungu ahifadhi Jumuiya ya Wakristo?

14 Hakuna mtu anayempenda Mungu wa Biblia kweli kweli atakayeomba kwamba jambo hilo la ajabu lisiipate Jumuiya ya Wakristo. Yehova alimwamuru nabii wake Yeremia asisali kwamba Yerusalemu na hekalu lake najisi visipatwe na kufikilizwa kwa hasira Yake ya haki. Mfano wa Kisasa wa Yerusalemu, Jumuiya ya Wakristo, imejionyesha kuwa haiwezi kubadilika. Baada ya miaka hii yote ambayo Yehova ametuma mashahidi wake Wakristo kusudi wawaonye watu wa Jumuiya ya Wakristo, inaendelea katika uovu wake hata kufikia mahali isipoweza kusamehewa.​—Yer. 7:18-26; 5:7-9.

15, 16. (a) Jumuiya ya Wakristo haipaswi kuhurumiwa kwa sababu ya mwendo gani wa kuenenda? (b) Katika kutoa mfano wa jambo hili, Yehova alisema nini katika Yeremia 7:30, 31?

15 Hatupaswi kuihurumia Jumuiya ya Wakristo kwa sababu uharibifu wake utahusu uhai mwingi wa kibinadamu. Mwendo wake umeleta suto kubwa juu ya Mungu. Sababu gani tusimfikirie yeye kwanza? Yeye ni wa maana zaidi kuliko viumbe vyote vya kibinadamu. Ebu wazia namna Jumuiya ya Wakristo pamoja na mamia ya mamilioni ya washiriki wake wa kanisa imelete aibu juu ya jina lake nayo imewatesa mashahidi wake waaminifu amabo wametangaza maonyo yake na mashauri yake yenye kuokoa maisha. Je! tunawahurumia zaidi wanadamu wasiotii, wasiosikia kuliko jina la Mungu Aliye Juu Zaidi? Ni kweli, kuangamia kwao pamoja na Jumuiya ya Wakristo ni jambo la kusikitisha, walakini mwendo wao wa sasa wa kuenenda kidini wenye aibu unasikitisha. Katika kuonyesha mfano wa jambo hili, Yehova alisema hivi:

16 “Wana wa Yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu, asema [Yehova]; wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo, iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi. Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la Hinomu [nje ya ukuta wa kusini wa Yerusalemu], ili kuwateketeza [nani?] wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.”​—Yer. 7:30, 31; tazama Mambo ya Walawi 18:21; 20:2-5.

17. (a) Ni ulizo gani linalotokea juu ya huruma kuelekea kwa dhabihu za kibinadamu na wazazi waliozitoa? (b) Ni nani aliyeanzisha wazo hilo la dhabihu za kibinadamu?

17 Kwa hiyo, sasa, kwa habari ya kuhurumia, tunahurumia nani zaidi? Wale wazazi wenye kuabudu sanamu ambao walikuwa na hesabu ya kumtolea Yehova? Au wana na binti wenye kupiga yowe walipokuwa wakitolewa kama dhabihu za kibinadamu kwa mungu wa uongo Moleki (Mfalme), kwenye madhabahu ya juu katika Tofethi katika bonde la mwana wa Hinomu? (Yer. 32:35) Wazazi hao wasio na huruma wangewezaje kushirikisha ibada ya namna hiyo ya mungu-sanamu mkatili Moleki na ibada katika hekalu takatifu kaskazini tu mwa bonde hilo? Hawakuwa wanatolea mungu wa uongo dhabihu hizo za kibinadamu zenye uhai kwa amri ya Yehova. Wazo hilo la dhabihu za kibinadamu liliingia moyoni mwa waasi hao wa kidini huko nyuma, walakini halikuingia hata kidogo katika moyo wa Yehova Mungu. Watu wanaojaribu kuchanganya ibada ya namna hiyo na ibada ya Yehova wanastahili nini?

18. Kwa kupiga hesabu, dhabihu hizo za zamani zinakuwaje zikilinganishwa na zile zilizotolewa na Jumuiya ya Wakristo katika muda unaopungua karne moja sasa?

18 Pale nyuma, dhabihu za watoto zilizotolewa na “wana wa Yuda” wenye kuasi dini zinakuwa si kitu kwa habari ya hesabu zinapolinganishwa na dhabihu za wanadamu ambazo Jumuiya ya Wakristo imetolea miungu wake wasio wa Kikristo katika karne nyingi. Ijapokuwa inajifanya kuwa ufalme unaoonekana wa Mfalme wa Amani, imetoa kama dhabihu wana na binti wasiohesabika kwa mungu wa vita, Moleki wake au “Mfalme.” Sasa katika muda unaopungua karne moja, imetoa milioni nyingi za vijana walio washiriki wake wa kanisa walio bora zaidi katika vita viwili vyenye umwagaji mwingi zaidi wa damu katika historia yote ya kibinadamu, na katika vita vingi vidogo. Kwa kukufuru Jumuiya ya Wakristo inaliita jambo hili Ukristo. Inazihesabu dhabihu hizi kuwa “dhabihu kuu zaidi” inayowapa mara moja wale waliotolewa dhabihu cheti cha kusafiria cha kuwawezesha kuingia mahali alipo Kristo huko juu mbinguni!

DHABIHU ZINAZOMPENDEZA YEHOVA MUNGU

19. Kwa hiyo, basi, inamaanisha nini kwa Mkristo kutoa mwili wake kuwa “dhabihu iliyo hai, takatifu” kwa Mungu?

19 Hizo si ndizo namna ya dhabihu ambazo Yehova Mungu anataka kutoka kwa wafuasi wa Mwana wake Yesu Kristo. Mahali pake, katika Warumi 12:1, 2, NW alimwongoza mtume Paulo aandike hivi: “Nawasihi kwa huruma za Mungu, ndugu, mtoe miili yenu dhabihu iliyo hai, takatifu, yenye kukubalika kwa Mungu, utumishi mtakatifu pamoja na nguvu yenu ya akili. Na mwache kufanyizwa kulingana na mtindo wa taratibu hii ya mambo, bali mgeuzwe kwa kubadili akili zenu, ili mpate kujithibitishia wenyewe mapenzi ya Mungu yaliyo mema na yenye kukubalika na makamilifu.” Mkristo kutoa mwili wake kuwa “dhabihu iliyo hai, takatifu,” hakumaanishi ajiue au amwachilie kasisi wa kidini amwue na kumtoa juu ya madhabahu. Huo usingekuwa “utumishi mtakatifu pamoja na nguvu yenu ya akili.” Mahali pake, inamaanisha Mkristo kufuata mwendo wa maisha wa kujinyima kwa ajili ya utumishi wa Mungu, si kujifanya mfia imani makusudi ili ajionyeshe.

20. Kwa kuishi katika njia hiyo “yenye kukubalika kwa mungu,” Mkristo anaweza kumtolea Mungu dhabihu gani zenye uhai?

20 Kwa kuendelea kuishi katika njia “yenye kukubalika kwa Mungu,” Mkristo wa kweli anaweza kumtolea Mungu dhabihu zinazotajwa katika Waebrania 13:15, 16: “Kwa njia yake yeye [Kristo, Kuhani Mkuu wa Mungu], na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo [lilitangazalo waziwazi] jina lake. [Zaidi ya hayo] msisahau kutenda mema na kushirikiana [vitu na wengine]; maana sadaka hizi ndizo zimpendezazo Mungu.”

21. Kwa watu wake wateule, Yehova aliweka nini mbele ya kutoa kwao wanyama, na kwa hiyo namna gani juu ya dhabihu za kibinadamu?

21 Dhabihu hizo zilizoelezwa hazituruhusu tuchanganye ibada ya Yehova pamoja na kutoa wanadamu au wanyama kwa miungu wa uongo wa ulimwengu huu. (Isa. 42:8) Jambo la kwanza ambalo Mungu anataka kutoka kwa watu wake ni utii, kutii kwetu “mapenzi ya Mungu yaliyo mema na yenye kukubalika na makamilifu.” Yehova alipowaokoa watu wake kutoka kwa uonezi wenye kuleta kifo katika Misri ya kale, hakuweka kwanza, kama jambo la kwanza la maana, kumtolea dhabihu za wanyama: “Lakini naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile nitakayowaamuru, mpate kufanikiwa.” (Yer. 7:22, 23; 1 Sam. 15:22) Kwa hiyo ikiwa Yehova hakuwaamuru watu wake wateule watoe dhabihu za wanyama, asingewaomba watoe dhabihu za wanadamu. Wazo la dhabihu za wanadamu, kama zile zilizotolewa kwa Baali au Moleki, hata “halikuingia katika moyo [wake].”​—Yer. 7:31.

22, 23. (a) Jumuiya ya Wakristo, ikiwa na kumbukumbu lake lote la kumwaga damu ya wanadamu, imeshindwaje kutoa dhabihu zinazokubalika kwa Mungu? (b) Ni jambo gani lingepata mfano wake wa kizamani ili kuonyesha ikiwa itakosa kuadhibiwa?

22 Jumuiya ya Wakristo, lijapokuwa kumbukumbu lake lenye umwagaji wa damu ya kibinadamu, haijampa Mungu dhabihu zinazompendeza. Kumtii Mungu wa Biblia kumekosekana kwake. (Mik. 6:6-8) Mpaka siku hii haijautubia mwendo wake wa kutokutii, ili imtolee Mungu dhabihu inayofaa: “Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” (Zab. 51:17) Je! inastahili kutokuadhibiwa? Je! itakosa kuadhibiwa? Mfano wake wa zamani, Yerusalemu, ulipata adhabu wakati wake, kama vile Yehova alivyosema:

23 “Basi angalieni, siku zinakuja, asema [Yehova], ambazo katika hizo halitaitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali litaitwa, Bonde la Machinjo; maana watazika watu katika Tofethi, hata hapatakuwapo mahali pa kuzika tena. Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula kwa ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza. Ndipo katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, nitaikomesha sauti ya kicheko na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi; kwa maana nchi hiyo itakuwa ukiwa.”​—Yer. 7:32-34; 19:6-9.

24. Utimizo halisi wa unabii huo wa kidini ulitukia wakati gani?

24 Kufikilizwa kwa unabii huu wa kidini hakukutukia wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, ambaye alifanya kazi ya kuponda sanamu na mahali kulikokuwa kumetolewa kwa ajili ya ibada ya Moleki na miungu wengine wa kishetani. (2 Fal. 23:3-20) Kubadilishwa kwa Tofethi na bonde la Hinomu kuwa bonde la machinjo, lililotapakaa maiti za Wayuda, pasipo makaburi ya kuzuia ndege wenye kula nyama na wanyama wasizile, kulitukia katika mwaka 607 K.W.K., wakati Yerusalemu na Yuda zilipoachwa ukiwa kwa miaka 70.​—2 Nya. 36:17-21.

25. Kwa sababu ya yaliyotangulia,Jumuiya ya Wakristo haitaponyoka utimizo wa unabii gani wa Yeremia?

25 Jumuiya ya Wakristo ya leo yenye hatia ya damu, pamoja na mila zake za kipagani, mapokeo ya wanadamu, na mchanganyiko wa filosofia za watu wasio na dini pamoja na mafundisho ya Biblia, itapatwa na mabaya kama vile mfano wake wa kizamani. Haitaponyoka kushiriki katika utimizo wa unabii wa Yehova: “Tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia. Na waliouawa na [Yehova] siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi.” (Yer. 25:32, 33) Hapana! Jumuiya ya Wakristo haitaokoka “dhiki kubwa” inayokuja. (Mt. 24:1, 2, 21, 22) Zaidi ya hayo, sehemu nyingine yote ya milki ya uongo itaifuata karibu katika uharibifu huo!

[Sanduku katika ukurasa wa 3]

Unabii wa Biblia wa Yeremia unawaelekeza wapenda haki kwenye “njia ya uzima.” Vilevile unaeleza juu ya kufikiliza hukumu kwa Yehova Mungu juu ya dini ya uongo na juu ya mataifa yanayopinga mapenzi yake. Wakati huo umekaribia! Kwa hiyo, ni wakati unaofaa kwa “Mnara wa Mlinzi,” katika makala hii, na katika yale yatakayofuata, kuzungumza utimizo wa siku kisasa wa unabii wa Yeremia.

[Picha katika ukurasa wa 4]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki