Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 3/15 kur. 12-18
  • “Funguo za Ufalme” na “Mkutano Mkubwa”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Funguo za Ufalme” na “Mkutano Mkubwa”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KUFUNGULIA “MKUTANO MKUBWA” NJIA
  • “Mungu Hana Ubaguzi”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
  • “Funguo” za Serikali Kuu Zaidi Zatumiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Ule Umati Mkubwa Kuishi Mbinguni? Au Duniani?
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • “Furahini, Enyi Mataifa, Pamoja na Watu Wake”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 3/15 kur. 12-18

“Funguo za Ufalme” na “Mkutano Mkubwa”

1. Kwa sababu ya kuhama kwa mwisho kwa Filipo kwenda Kaisaria, ni maulizo gani yanayotokea juu yake kuhusiana na mwaka 36 W.K.?

KATIKA mwaka 36 W.K. tukio lenye kutokeza katika historia ya Ukristo lilitokea katika Kaisaria upande wa mashariki mwa ufuo wa Bahari ya Kati (Mediterranean). Kama Filipo mwinjilisti alikuwa amekwisha kuchukua makao hapo kufikia mwaka huo hatujui kwa hakika. Iwapo alikuwa amekwisha kufanya hivyo, basi sababu gani hakutumiwa kwa habari ya afisa mmoja wa kijeshi wa jeshi la askari wa Italia ambalo wakati huo makao yake yalikuwa huko? Filipo alikuwa amemtangulia mtume Petro katika utendaji wa Kikristo katika Samaria, sababu gani sasa asifanye hivyo katika Kaisaria katika mwaka 36 W.K.? Maandiko yaliyoongozwa kwa roho yanatupa sababu.

2. Agano la Torati ya Musa lilifutwa wakati gani, na hata hivyo upendeleo wa pekee kwa Wayahudi waliotahiriwa uliendelea kwa muda gani?

2 Agano la Torati ambalo Musa alikuwa amepatanisha kati ya Yehova Mungu na Israeli kwenye Mlima Sinai katika Uarabu lilifutwa juu ya msingi wa Yesu Kristo, mzao wa Ibrahimu na Mfalme Daudi. Hiyo ilikuwa miaka mitatu na nusu tangu kubatizwa kwa maji na kutiwa mafuta kwa roho kwa Yesu hapo nyuma katika mwaka 29 W.K. Hata hivyo, Yehova aliendelea kuwatendea kwa upendeleo Wayahudi wa asili na Wasamaria vilevile wakati wa kipindi hiki kwa miaka mitatu na nusu, zaidi, ili kutimiza unabii wa Danieli 9:24-27a. “Juma” hili au kipindi cha miaka saba lilimalizika mwezi wa saba (Tishri) wa mwaka 36 W.K. Kuanzia wakati huo na kuendelea wazao Waisraeli wa Ibrahimu wangewekwa kwenye hali ile ile ya kiroho na watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi, Mataifa wasiotahiriwa. Baada ya hilo hakuna kutendewa kwa upendeleo kwa Wayahudi na Mungu wa Ibrahimu! Jambo hili lilionyeshwaje katika mwaka 36 W.K.?

3. (a) Mtume Petro alikuwa wapi wakati huo na sababu gani? (b) Sababu gani Petro alilaumiwa Wayahudi Wakristo waliotahiriwa huko Yerusalemu kwa ajili ya tendo lake lisilo la kawaida?

3 Yapata wakati huu, baada ya ombi la haraka kutoka kwa kundi la Kikristo katika mji wenye bandari wa Yafa, Petro alikuwa amekuja na kumfufua Myahudi Mkristo aliyekuwa mwenye ukarimu Dorkasi. Huko alikaa siku chache na Simoni mtengenezaji wa ngozi. (Matendo 9:36-43) Wakati huo Mtaifa asiyetahiriwa alikuwa asiyetakiwa kama mwenzi wa Myahudi, kwa kadiri ile ile, hakika, kama mtu aliyetengwa na kundi la watu wa Mungu. (Mt. 18:17) Kwa hiyo, kufikia wakati huu, Myahudi-Mkristo Petro hakuwa amepata kuingia kwa kusukumwa na moyo wake mwenyewe kwenye nyumba ya Mtaifa asiyetahiriwa. (Bila shaka ilikuwa vivyo hivyo kwa mwinjilisti Filipo vilevile.) Kama matokeo, wakati, baadaye, Wayahudi Wakristo waliotahiriwa huko Yerusalemu waliposikia kwamba Petro hatimaye alikuwa ameingia nyumba ya Mtaifa, walimlaumu, wakisema kwamba ‘alikuwa ameingia kwa watu wasiotahiriwa akala nao.’​—Matendo 11:3.

4. Mtume Petro aliyekuwa Myahudi Mkristo aliyaelezaje maono yake ya ndani baada ya kukanyaga nyumba ya Mtaifa katika Kaisaria?

4 Hata Petro, ijapokuwa alikuwa amekuwa mtume Mkristo kwa miaka kadha sasa, alimwambia hivi mwenye nyumba ambaye katika nyumba yake katika Kaisaria alikuwa amesita kuweka mguu wake ndani: “Mwajua vema jinsi isivyokuwa halali kwa Myahudi kujishikamanisha au kumkaribia mtu wa taifa jingine.” (Matendo 10:28, NW; Jerusalem Bible; The New English Bible) Mataifa walionwa kuwa najisi au wachafu.

5, 6. Ni mambo gani ya hakika aliyotoa Petro katika kutetea tendo lake katika Kaisaria lililolaumiwa?

5 Katika kujitetea, Petro alilazimika kutaja mambo ya hakika kwa mitume na Wayahudi wengine Wakristo huko Yerusalemu. Mambo hayo ya hakika yalikuwa nini? Haya: Kwamba Petro hakuwa amelianzisha tendo hili kwa kupenda kwake mwenyewe. Yeye alikuwa ametenda kwa kumtii Yehova Mungu.

6 Petro alipokuwa nyumbani mwa Simoni mtengeneza ngozi katika Yafa, Mungu alimpelekea Petro njozi ya kujulisha vitu ambavyo sasa Mungu alikuwa amefanya kuwa safi Petro hakupaswa kuendelea kuviita vichafu. Kisha wanaume watatu ambao walikuwa wametumwa na akida Mwitalia Kornelio wa Kaisaria walitembelea nyumba hiyo wakitaka habari juu ya Petro. Sasa Mungu akamwambia mtume huyu aliye Myahudi-Mkristo aende pamoja nao, “usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma.” Sita kati ya Wayahudi Wakristo waliotahiriwa wa kundi la Yafa walikwenda pamoja na Petro mpaka pwani ya bahari huko Kaisaria. Siku iliyofuata, walipoingia nyumba ya akida Mtaifa Kornelio, alieleza kwamba malaika wa Mungu alikuwa amemtokea na kumwambia amwite Petro kutoka Yafa, “atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote.”​—Matendo 10:1-33; 11:14.

7. Petro alifika wapi katika hotuba yake kwa Mataifa katika nyumba ya akida Mwitalia Kornelio?

7 Bila kufahamu ni jambo gani karibuni lingetokea, Petro aliendelea kutoa ujumbe juu ya huduma ya kidunia ya Yesu Kristo, kifo chake na kufufuliwa kwake kutoka kwa wafu kwa uwezo wa Mungu mwenye nguvu zote. Katika hotuba yake alifikia kusema: “Huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa wahai na wafu. Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.”​—Matendo 10:34-43.

8. Petro alipokuwa angali akizungumza, Mungu alitoa uthibitisho gani kwamba sasa yeye alikuwa akiruhusu Mataifa wenye kuamini wasiotahiriwa kwenye kundi lililozaliwa kwa roho?

8 Kufikia hapa Yehova Mungu alitoa uthibitisho kwamba yeye sasa alikuwa akikubali Mataifa wenye kuamini, wajapokuwa hawajatahiriwa, kwenye kundi la Wakristo waliozaliwa kwa roho, kwa kuwa twasoma hivi: “Petro alipokuwa akisema maneno hayo [roho takatifu i]kawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha [roho takatifu]. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu.”​—Matendo 10:44-46.

9. Katika masimulizi yake kule Yerusalemu, Petro alisimuliaje tendo la roho takatifu kule Kaisaria, naye alililinganisha na nini?

9 Alipokuwa akitoa masimulizi yake mwenyewe ya jambo hili huko Yerusalemu, Petro alisema hivi: “Ikawa nilipoanza kunena, [roho takatifu i]kawashukia kama [i]livyotushukia sisi mwanzo [wakati wa Pentekoste, mwaka 33 W.K.]. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa [roho takatifu]. Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?​—Matendo 11:15-17.

10. Sasa Petro aliamuru jambo gani lifanywe kwa Mataifa hawa wasiotahiriwa, na sababu gani?

10 Kwa hiyo Petro alifanya nini sasa? “Ndipo Petro akajibu, Ni nani [kati ya wale Wayahudi Wakristo sita walioambatana na Petro] awezaye kukataza maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea [roho takatifu] vile vile kama sisi [Wayahudi Wakristo waliotahiriwa]? Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo.”​—Matendo 10:46-48.

11. (a) Kuanzia wakati huo na kuendelea, waamini wa Mataifa waliozaliwa kwa roho walikuwa huru kutenda katika cheo gani? Sababu gani? (b) Tendo la roho takatifu lilikuwa sawa namna gani katika pindi tatu, kwa vikundi vitatu mbalimbali?

11 Hivyo ‘Mungu kwa mara ya kwanza akawaangalia mataifa [wasiotahiriwa] ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.’ (Matendo 15:14) Katika pindi hii, katika nyumba ya akida asiyetahiriwa Kornelio katika Kaisaria, Petro alitumia mwingine wa zile “funguo za ufalme wa mbingu,” ufunguo wa tatu. Kuanzia wakati huo kuendelea, wanafunzi wa Yesu waliotiwa mafuta kwa roho wangeweza kuwa mashahidi wake “hata mwisho wa nchi.” (Matendo 1:8) Kile ambacho Mungu alikuwa amefungua kupitia kwa mwenye funguo Petro kiliendelea kuwa kimefunguliwa kwa ajili ya kutolewa ushuhuda wa duniani pote. Kwa kupatana na jambo hili, roho takatifu ya Mungu ‘ilishukia’ (Kigiriki: epipipto) jamii tatu tofauti za waamini, (1) juu ya wanafunzi 120 waliobatizwa na, baadaye Wayahudi waliongolewa wapata 3,000, wote hawa katika Pentekoste ya mwaka 33 W.K.; (2) juu ya Wasamaria waliobatizwa, walakini baada tu ya kufika na utumishi wa mitume Petro na Yohana; na (3) juu ya Mataifa waamini waliokusanyika katika nyumba ya Kornelio katika Kaisaria, katika mwaka 36 W.K.​—Matendo 1:15; 2:1-4, 38, 41; 8:15-17; 10:44, 45; 11:15, 16.

KUFUNGULIA “MKUTANO MKUBWA” NJIA

12. Tangu wakati huo Yehova amekuwa akichukua jamii gani kutoka kwa akina nani?

12 Kwa karne nyingi tangu wakati huo Yehova amekuwa akijichukulia watu “kwa ajili ya jina lake” kutoka miongoni mwa Wayahudi waliotahiriwa, Wasamaria waliotahiriwa na Mataifa wasiotahiriwa. (Amosi 9:12) Hawa watu kwa ajili ya jina la Yehova hesabu yao yapaswa kuwa 144,000 tu, ambao wataungana na Yesu katika ufalme wake wa kimbinguni.​—Ufu. 7:4-8; 14:1-3.

13. Kitabu Food for Thinking Christians na kitabu The Divine Plan of the Ages vilionyesha nini juu ya asili na wokovu unaohusika?

13 Katika Septemba wa mwaka 1881 kitabu cha Sosaiti Food for Thinking Christians (Chakula kwa ajili ya Wakristo Wenye Kufikiri) kilitolewa. Baadaye, katika mwaka 1886, kitabu The Divine Plan of the Ages (Mpango wa Kimungu wa Vizazi Vyote) kilitolewa. Vitabu hivi viwili vilionyesha kwamba asili ya kiroho na asili ya kibinadamu au ya kidunia ni tofauti na ni aina mbalimbali. Kwa hiyo wokovu wa kundi lililozaliwa kwa roho la 144,000 kwenda mbinguni ungekuwa tofauti na ule wa wanadamu waliokombolewa kwenye uzima juu ya dunia iliyo paradiso. Hata hivyo, dhabihu ya ukombozi ya Yesu Kristo ndiyo msingi kwa huu wokovu wa namna mbili.

14. Hotuba ya watu wote iliyotolewa katika Los Angeles, California, Jumapili, Februari 24, mwaka 1918, ilikazia nini?

14 Katika Februari 24, mwaka 1918, katikati ya Vita ya Kwanza ya Ulimwengu, J. F. Rutherford akiwa msimamizi wa Watch Tower Bible and Tract Society alitoa hotuba ya watu wote katika Los Angeles, Califomia, U.S.A. Kichwa chake kilikuwa “Mamilioni Wanaoishi Sasa Huenda Wasife Kamwe.” Baada ya Vita ya Kwanza ya Ulimwengu hotuba hii yenye kustaajabisha ilichapwa katika namna ya kitabu. Habari hii ilikazia kwamba kungekuwako watu wenye maelekeo ya haki duniani ambao wangeokolewa wakiwa hai wakati wa siku inayokuja ya ghadhabu ya Mungu. Wangeokoka na kuingia kwenye taratibu mpya ya Mungu na kupata nafasi ya kutokufa katika dunia iliyogeuzwa kuwa paradiso.

15. Hotuba katika mwaka 1923 huko Los Angeles, juu ya mfano wa Yesu wa kondoo na mbuzi, ilitokeza nini?

15 Kwa mara nyingine tena katika Los Angeles, katika mwaka 1923, kusanyiko lilifanywa na msimamizi wa Sosaiti alizungumza juu ya mfano wa Yesu wa kondoo na mbuzi. Kwa kutumia Maandiko alithibitisha kwamba “kondoo” wa mfano huu ni wale ambao sasa, wakati wa huu “wakati wa mwisho,” wanafanyia mema katika njia mbalimbali ndugu za Yesu wa kiroho au ‘waliozaliwa tena.’ Kama thawabu yao watu hao wanaofanya mema wangehifadhiwa hai katika vita inayokuja ya Har–Magedoni, na “Mwana wa Adamu” aliyetukuzwa, Mfalme Yesu Kristo wa kimbinguni, atawaingiza kwenye makao ya kidunia ya ufalme wake wa miaka elfu moja. (Mt. 25:31-46) Jambo hili liliangaza matumaini ya kidunia kwa watu wengi wenye mfano wa kondoo ambao walifanyia mema “ndugu” za Kristo kama kwamba walikuwa wakimfanyia yeye moja kwa moja.

16, 17. Wakati upeo katika kuendelea huku katika ufahamu wa Biblia ulipokuja miaka 12 baadaye, sababu gani haikuwa pindi ya kawaida?

16 Hata hivyo, upepo wa jambo hili la kuendelea katika ufahamu wa Biblia ulikuja miaka 12 baadaye. Hii haikuwa pindi ya kawaida tu katika historia ya ya kibinadamu. Kule kuharibika sana kwa uchumi wakati huu kulikuwa katika mwaka wake wa sita. “Mwaka Mtakatifu” wa Rumi Katoliki wa 1933 ulishindwa kuleta “amani na fanaka” iliyoahidiwa. Kwa ajili ya mabishano na Milki ya Ethiopia, Italia ya Kifasisti ilikuwa ikijitayarisha kwa ajili ya vita na katika Oktoba 3, mwaka 1935, majeshi ya Italia yaliivamia Milki hiyo. Adolf Hitler alikuwa katika mwaka wa tatu wa utawala wake akiwa mwenye mamlaka peke yake juu ya Ujeremani, naye alikuwa akiwatesa kinyama Mashahidi wa Yehova. Katika Oktoba 4, mwaka 1934, alikuwa ameonywa kwa mamia ya simu kutoka duniani pote kwamba, iwapo asingeacha kuwatesa, Yehova angemharibu yeye na chama chake cha Nazi. Walakini kwa ukaidi aliazimia kufagilia mbali kutoka Milki ya Ujeremani hawa Wakristo wasiojiweza, wasiokuwa wa kisiasa.

17 Wakati wa mwaka 1935, rais wa Amerika, Franklin D. Roosevelt, alikuwa akipata matatizo kuhusiana na chama alichokuwa ameanzisha, cha NRA (National Recovery Administration), na serikali hiyo ya kitaifa ilikuwa ikishindwa na mkazo wa Tendo la Katoliki. Urusi ilikuwa chini ya utawala wa “bwana mkubwa” Joseph Stalin. Japan ya Kibepari, ikiwa mpinzani mwenye uadui wa Ukomunisti, ilikuwa ikielekea kwenye “Mapatano ya Watatu” yenye kupatwa na msiba pamoja na Italia ya Kifasisti na Ujeremani ya Nazi, ili kufanyiza Mamlaka zenye Kuongoza. Vita ya Pili ya Ulimwengu ilikuwa imeanza kutokezwa!

18. Mashahidi wa Yehova walifanyia wapi kusanyiko katika masika ya mwaka 1935, nayo mazungumzo ya hotuba ya watu wote yalikuwa nini?

18 Ingawa mambo ya serikali yalikuwa yenye hatari sana ulimwenguni pote katika mwaka 1935, ulipata kuwa wakati wenye kusisimua kipekee kwa Mashahidi wa Yehova. Walifanya kusanyiko katika sehemu iliyo na makao makuu ya serikali ya Amerika, Washington, D.C., katika Mei 30 mpaka Juni 3. Hotuba ya watu wote iliyotolewa Jumapili, Juni 2, ilikuwa yenye kichwa “Serikali” nayo ilitangazwa kwa radio katika Uingereza, Ulaya, Afrika na visiwa vya bahari.​—Tazama toleo la Agosti 29, 1935, la gazeti The Golden Age.

19. Ijumaa alasiri, Mei 31, ni washiriki wa jamii gani waliotambulishwa, nalo ni jambo gani lingepata jamii hii kuhusiana na “dhiki ile iliyo kuu”?

19 Mapema, Ijumaa alasiri, Mei 31, hotuba yenye kusisimua ilitolewa kwa wahudhuriaji wa kusanyiko hilo. Kwa ajili ya umuhimu wayo, ilitangazwa wakati ule ule katika vituo viwili vya radio. Watu wenye mfano wa kondoo wenye kupendezwa na uzima wa milele duniani katika hali ya paradiso walialikwa hasa wahudhurie kusanyiko hilo. Kupendezwa kwa wahudhuriaji wote wa kusanyiko kulivutwa na kichwa ambacho kufikia wakati huo kilikuwa kimeeleweka vibaya, yaani, “mkutano mkubwa” ulioonwa katika njozi na mtume Yohana kulingana na Ufunuo 7:9-17. Kwa furaha hasa ya wasikilizaji wenye kuonekana na wasioonekana, washiriki wa huo “mkutano mkubwa” walitambulishwa. Wao si wa jamii yenye kuelekea mbinguni, ‘iliyozaliwa tena’ ya Wakristo. Wao ni wa jamii ya kidunia ya “kondoo” wa mfano wa Yesu ulioandikwa katika Mathayo 25:31-46. Wanaokoka duniani na katika njia hii “wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu.”​—Ufu. 7:14.

20. Wale waliotaka kuwa washiriki wenye taraja wa “mkutano mkubwa” walipaswa kujitoaje, na, baada ya kuthibitisha waziwazi jambo hili, wasingetazamia roho kufanya nini?

20 Hawa wanakuja chini ya takwa la kujitoa wenyewe kwa Mchungaji Mwema wa Yehova, Yesu Kristo. Wanaonyesha kujitoa kwao kwa kujiweka wakf wenyewe kwa Yehova kupitia kwa Kristo. Kupatana na Maandiko kujiweka wakf huko kwapaswa kuthibitishwa kwa ubatizo wa maji katika jina la Baba, la Mwana na la roho takatifu. (Mt. 28:19, 20) Kwa hiyo, iwapo wo wote watamani kuwa washiriki wenye kutarajia wa huo “mkutano mkubwa,” ni jambo la akili kwamba wajiweke wakf wenyewe sasa na kuonyesha wakf wao kwa ubatizo wa maji. (The Watchtower, Agosti 15, 1934, uku. 250, fu. 34) Isingetazamiwa kwamba, kufuatia ubatizo wao, roho ya Mungu ‘ingewashukia’ na kuwazaa kwenye uzima wa kimbinguni ambao hawakuwa wakitafuta.

21. Kwa ufunuo huu, mamia walichochewa kufanya nini siku iliyofuata, nao waliingia kwenye “zizi” gani?

21 Ufunuo huu ulikuwa wenye kusisimua, sana sana kwa wale wenye mfano wa kondoo ambao walikuwa wakitamani ufahamu kamili wa msimamo wao katika mpango wa Yehova. Kwa hiyo walichochewa kwenye utendaji na kutambulishwa kwa “mkutano mkubwa.” Siku iliyofuata, Jumamosi, Juni 1, ilipangwa ili itoe nafasi ya ubatizo wa maji. Ilikuwa furaha kubwa kwa wenye kubatizwa 840, ambao wengi wao walibatizwa wakiwa na tumaini la kuwekwa na Yehova katika jamii moja ya wenye kutarajia kuwa “mkutano mkubwa.” Lilipata kuwa tukio lenye kutokeza la ubatizo. Ilikuwa kama kwamba malango ya maji yalikuwa yamefunguliwa, makutano mengi waliingia kwenye uhusiano ulioungamwa waziwazi pamoja na Yehova, na kuingia katika “kundi moja” la Mchungaji Mwema ili washirikiane na “ndugu” zake wa kiroho.​—Yohana 10:16; Mt. 25:34.

22. (a) Ni “ufunguo” gani uliokuwa umetumiwa, na kwa matokeo gani? (b) Fikira zao zilielekezwa kwenye serikali gani siku iliyofuata, na ilikuwa juu yao kushangilia kwa wao kuwa nini?

22 Ilikuwa kama kwamba jamii ya “mtumwa mwaminifu mwenye akili” ilikuwa imetumia “ufunguo wa maarifa” (Mt. 24:45-47; Luka 11:52) na kufungua mlango kwa washiriki wenye taraja wa “mkutano mkubwa” wapate kuingia kwenye mapendeleo ya ajabu. Kuyashika haya kungewafanya ‘watoke katika ile dhiki iliyo kuu’ na kuingia kwenye dunia iliyosafishwa chini ya serikali yake mpya kupitia kwa Kristo. Fikira zao zilielekezwa kwenye serikali hiyo katika siku iliyofuata kupitia kwa hotuba ya watu wote juu ya mazungumzo “Serikali,” mazungumzo ambayo yalifaa sana hali ya ulimwengu iliyokuwako wakati huo. Kwa hesabu kubwa ya wasikilizaji wenye kuonekana na kwa wasikilizaji wa radio wengi zaidi waliotapakaa, hotuba hiyo ilitoa onyo la mapema la uharibifu unaozikaribia serikali zote za kidunia za wanaume wa kilimwengu katika vita ya Mungu kwenye Har–Magedoni. Pamoja na hayo, hotuba hiyo ilitukuza serikali ya Yehova ya kitheokrasi kupitia kwa Kristo kuwa tumaini pekee la wanadamu wote. Hii ndiyo iliyokuwa serikali ya kimungu kwa “mkutano mkubwa,” au “kundi kubwa,” kushangilia kama tumaini lao tukufu!a

23. (a) Kwa “ufunguo wa maarifa” kutumiwa, je! mlango kwa waamini wafaao kwa ajili ya ufalme wa kimbinguni ulifungwa? (b) Ni jambo gani liwezalo kutolewa kama ushuhuda kuhusiana na hili?

23 Hata hivyo, kwa kutumia hivyo “ufunguo wa maarifa” je! mlango unaoruhusu waamini wafaao kwenye ufalme wa kimbinguni ulikuwa umefungwa wakati ule ule? Sivyo, kwa kuwa Yesu Kristo Ndiye aliye na “ufunguo wa Daudi” naye peke yake ndiye awezaye kufunga mlango huo. Kuruhusiwa kungali kulikuwa kwawezekana kwa watu fulani kulingana na mapenzi ya Mungu. Kama ushuhuda wa jambo hili, washiriki fulani wa mabaki watiwa mafuta wa Mashahidi wa Yehova walibatizwa katika maji katika miaka iliyofuata ufunuo huo wa muhimu sana juu ya “mkutano mkubwa” katika masika ya mwaka 1935 na kuchapwa kwa ufunuo huo katika makala ya Agosti 1 na 15, 1935, ya gazeti la Watchtower.​—Ufu. 3:7; Luka 11:52; Mt. 23:13.

24. (a) Ni kitu gani kitakachozuia kuingia kwa wengine zaidi kwenye lile “kundi moja” chini ya Mchungaji Mwema? (b) Mchungaji huyo anaruhusu “kondoo” kwenye hilo “kundi moja” akiwa na cheo gani?

24 Ni kuanza tu kwa “dhiki kubwa” kuwezako kufunga njia ya wanadamu kuingia kwenye cheo cha wenye mfano wa kondoo ambao watakuwa washiriki wa “mkutano mkubwa,” au “kundi kubwa.” Njia ya kuepukia uharibifu pamoja na taratibu hii iliyohukumiwa maangamizi itakuwa wakati huo nafasi ya wokovu iliyopotezwa. Kwa miaka yote hii tangu mwaka 1935 mlango kwenye “kundi moja” la Mchungaji Mwema umeendelea kuwa wazi. Inaripotiwa kwamba, zaidi ya watu milioni mbili wameingia ndani. Mchungaji Mwema Yesu Kristo, alisema: “Mimi ndimi mlango wa kondoo.” (Yohana 10:7-9) Akiwa hivyo, yungali anaruhusu rafiki za “ndugu” zake wa kiroho na anawabagua kutoka kwa “mbuzi” ambao hawataokoka kamwe “dhiki ile iliyo kuu” na “vita” yake kwenye Harmagedoni. Wale wote ambao sasa wataka, ebu na wasikilize “sauti” ya Mchungaji Mwema inapotolewa kupitia kwa “ndugu” zake wa kiroho ambao wangali duniani. (Yohana 10:16) Ee pendeleo lao ni kubwa kama nini la kufurahia usalama wa “kundi moja” chini ya huyo “mchungaji mmoja!”

—Kutoka The Watchtower Okt. 1, 1979.

[Maelezo ya Chini]

a Mamia ya mashahidi waliobatizwa karibuni walijiunga na itikio la wasikilizaji wenye kuonekana wakati msemaji wa watu wote alipotoa azimio mwishoni mwa hotuba yake na kusema: “Na sasa rafiki zangu wema wa wasikilizaji hawa, wasioonekana na wanaoonekana pia, napendekeza kwamba kila mmoja wenu anayetamani serikali ambayo katika hiyo amani, fanaka na furaha vitakuja kwa wote wanaotii, asimame na kusema Ndiyo.”

Kuhusu yaliyofuata pendekezo hili, gazeti la Washington Herald lilisema hivi:

“Kama vile wimbi makutano hayo mengi katika na kuzunguka jumba hilo yalisimama kwa miguu yao. Mikono ikiwa imeinuliwa juu, Mashahidi wa Yehova kama ambavyo mapafu yao yaliweza kuruhusu waliinua sauti juu ndiyo. Madirisha kwenye jumba hilo yalitikisika mshindo wa sauti ulipoyagonga, na sauti ya makutano hayo, polisi walikadiri, ingeweza kusikiwa kwa urahisi kwa umbali wa maili moja.”

Tamasha kama hizo zilifanywa wakati ule ule katika London, Belfast, Glasgow, Copenhagen na mamia ya sehemu nyingine katika sehemu nyingi za dunia.​—The Golden Age, toleo la Juni 19, 1935, uku. 598; tazama pia Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova (Kiingereza) cha mwaka 1936, uku. 62, fu. 3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki