Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 2/15 kur. 30-31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Juma Lililobadili Ulimwengu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Akiwa Bethania, Katika Nyumba ya Simoni
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kule Bethania, Katika Nyumba ya Simoni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Nisani 14—Siku ya Kukumbukwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 2/15 kur. 30-31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

■ Katika Yohana 6:53, je, Yesu alikuwa akimaanisha Wakristo wapakwa mafuta tu wakati alipoeleza hivi: “Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu”?

Kwa miaka mingi tumeyaeleza maneno haya kuwa yanawahusu Wakristo wapakwa mafuta peke yao, ambao watapelekwa mbinguni wakatawale pamoja na Yesu Kristo. Lakini, .uchunguzi zaidi wa jambo hili unapendekeza kuwe na matumizi mapana zaidi ya Yohana 6:53;

Kwa muda wa miaka iliyopita maoni yetu juu ya andiko hilo yamekuwa yakitegemea mistari mingine inayotumia maneno yanayofanana na ya andiko lenyewe. Kwa mfano, kifungu kinachohusu kuwa na “uzima ndani yenu” kinafanana na maneno ya Yesu katika Yohana 5:26, yaliyowahusu Yehova na Yesu peke yao. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa kwenye kurasa 11 na 12 za gazeti hili, habari zinazozunguka Yohana 5:26 zinatokeza msingi wa kuyafahamu maneno kuwa na “uzima nafsini mwake” katika mstari huo. Lakini maneno ya Yohana 6:53 yalitamkwa mwaka mmoja baada ya hapo, na habari zinazozunguka andiko hilo ni tofauti.

Jambo jingine lililofanya tuwe na maoni yale ya hapo kwanza kuhusu Yohana6:53 ni elezo la Yesu juu ya ‘kula mwili wake na kunywa damu yake.’ Elezo hilo lilikuwa na hali fulani zenye kufanana na maneno yaliyosemwa na Kristo alipokuwa akianzisha Chakula cha Jioni cha Bwana. Alipokuwa akikianzisha, alisema juu ya mwili na damu yake, akaelekeza kwamba mifano ya vitu hivyo (mkate na divai isiyochachwa) iliwe na kunywewa na wa fuasi wake ambao wangeingizwa ndani ya agano jipya na ndani ya agano kwa ajili ya ufalme. (Luka 22:14-22, 28-30) Lakini, hapa tena habari zinazolizunguka andiko la Yohana 6:53 zinahitajiwa kufahamiwa.

Wakati Yesu aliposema yaliyoandikwa katika Yohana 6:53, ulikuwa umebaki mwaka mmoja kabla hajaanzisha Chakula cha Jioni cha Bwana. Kati ya watu waliomsikia Yesu akisema hakuna wo wote walioelewa kwamba mwadhimisho wa kila mwaka ungefanywa kwa kutumia mifano ya vitu halisi vyenye kusimamia mwili na damu ya Kristo. Bali, kichwa cha habari ya Yesu, au hoja ya mazungumzo yake, katika Yohana sura ya 6 ilikuwa kwamba mwili wake ungeweza kulinganishwa na mana. Ingawa hivyo, palikuwa na tofauti. Mwili wake (kisha akaongeza kutaja damu yake pia) ulikuwa bora kuliko mana halisi kwa sababu mwili wake ulitolewa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu, ukafanya iwezekane kupata uzima wa milele​—Yohana 6:48-51.

Kwa hiyo, hivi majuzi uchunguzi zaidi umekazia jambo la kwamba palikuwa na tofauti ya mwaka mmoja kati ya maneno ya Yesu katika Yohana 5:26 na maelezo yake katika Yohana sura ya sita; kisha tofauti ya mwaka mwingine mmoja kabla hajaanzisha Chakula cha Jioni cha Bwana. Akili zaidi zimekazwa pia kwenye mistari inayokaribiana sana na Yohana 6:53. Hivyo, makala katika kurasa 15-20 za gazeti hili inatoa matumizi yaliyopanuliwa kuhusu Yohana 6:53, kutia ndani wale wanaoingizwa katika agano jipya kwa ajili ya uzima wa kimbingu na wale walio na taraja la kupata uzima usioisha katika dunia-paradiso.

■ Masimulizi ya Injili na vitabu vya marejezo yanaelekea kutofautiana kuhusu wakati ambao Yesu alikula nyumbani kwa Simoni mkoma katika Bethania kisha akapakwa mafuta yaliyotiwa marashi. Jambo hilo lilitukia wakati gani?

Inaelekea kuwa kwamba matukio haya yalitokea tarehe ya Nisani 9 kalenda ya Kiyahudi) ya mwaka 33 WK. Lakini kama vile inavyosemwa katika maelezo yanayofuata kuonyesha sababu za kukata shauri hivyo, utaona ni kwa nini kuendelea Kujifunza Neno la Mungu kunaweza kuleta maendeleo katika maarifa na ufahamu wako.

Maelezo marefu juu ya karamu hiyo yameonyeshwa katika tatu kati ya zile Injili nne. (Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9; Yohana 12:2-8) Mathayo na Marko wanaitaja karamu hiyo baada ya kueleza juu ya vile Yesu alivyopanda kwa ushindi kuingia Yerusalemu, juu ya kuulaani mtini usiozaa, na jibu lake kwa ulizo la mitume kuhusu umalizio wa mfumo wa mambo. Wote Mathayo na Marko wanafuatisha masimulizi juu ya karamu hiyo kwa kueleza jinsi Yuda alivyoshughulika na viongozi Wayahudi kwa habari ya kumsaliti Yesu. Mahali ambapo chakula hicho kimekuja kusimuliwa katika masimulizi hayo mawili pangedokeza kwamba kilifanyika Nisani 12, siku mbili tu kabla ya Yesu kusalitiwa na kuuawa Nisani 14 Kwa hiyo karamu hiyo imeonyeshwa kuwa ilifanyika Nisani 12 katika orodha nyingi zinazoonyesha matukio ya maisha ya Yesu, kutia na orodha nyingine zilizo katika vichapo vyetu vya wakati uliopita.

Katika Yohana sura ya 12 chakula kilicholiwa nyumbani kwa Simoni kinatajwa katika hali tofauti. Andiko la Yohana 12:1 (NW) linaripoti kwamba Yesu alifika Bethania karibu na Yerusalemu “siku sita kabla ya sikukuu ya Kupitwa,” na hiyo ingekuwa ni Nisani 8. Halafu mistari 2-8 inaeleza chakula cha jioni katika Bethania, na mistari 9-11 inatuambia kwamba Wayahudi waliosikia kwamba Yesu alikuwa karibu walikuja kumwona. Mistari 12-15 inasema kwamba “siku iliyofuata” Kristo aliingia Yerusalemu kwa ushindi. (Linganisha Matendo 20:7-11.) Kwa hiyo, andiko la Yohana 12:1-15 linaonyesha kwamba kile chakula kilicholiwa nyumbani kwa Simoni kilitukia Nisani 9 jioni, ambayo kulingana na kalenda ya Kiyahudi ingekuwa ndio mwanzo wa siku mpya, kisha ikafuatwa na kupanda kwa Yesu kuingia Yerusalemu katika kipindi chenye mwangaza cha siku hiyo (Nisani 9).

Kati ya hali hizo mbili zinazoweza kuwa zilitukia, ile ya pili ndiyo inayoelekea kuwa na uzito mwingi zaidi. Kwa sababu gani? Basi, na tulinganishe masimulizi yenyewe na habari zinayoyazunguka. Wala Mathayo wala Marko hatoi tarehe yo yote ambayo karamu hiyo ilifanyika katika nyumba ya Simoni. Ingawa hivyo, wanaonyesha kwamba kwenye karamu hiyo malalamiko yalitokea juu ya matumizi ya Mariamu ya mafuta ya bei kubwa, malalamiko ambayo Yohana anaonyesha yaliongozwa na pupa ya Yuda. (Mathayo 26:8, 9: Marko 14:4, 5; Yohana 12:4-6) Kama tulivyoona, wote Mathayo na Marko wanafuatisha mfululizo wa matukio ya karamuni kwa kumwonyesha Yuda akiwakaribia makuhani aone ni pesa ngapi anazoweza kulipwa ili amsaliti Kristo. Hivyo ingeweza kuwa kwamba kwa sababu zinazohusiana na habari wanayoizungumza, Mathayo na Marko wanaitaja karamu mahali walipoitaja, wakiunganisha ushuhuda mmoja wa kuonyesha Yuda alikuwa mwenye pupa pamoja na vile alivyokuja kuionyesha mwishowe.

Ingawa hivyo, Yohana anatoa tarehe ya waziwazi juu ya wakati karamu ilipofanyika, kuonyesha kwamba yeye aliitaja kulingana na mahali ilipopasa kuwa kulingana na utaratibu wa orodha za matukio. Jambo hilo linaunga mkono kukata shauri kwamba chakula cha jioni kwenye nyumba ya Simoni kilitukia baada ya Yesu kufika Bethania Nisani 8, 33 W.K. Zaidi ya hilo, kumbuka habari zinazoelezwa na Yohana kwamba Wayahudi ‘waliopata kujua kwamba Yesu sasa alikuwa katika Bethania’ walikuja kutoka Yerusalemu ili wamwone yeye na Lazaro, ambaye pia aliishi katika Bethania na ambaye dada zake walikuwa karamuni. Ziara hiyo ya Wayahudi ambao walikuwa wametoka tu ‘kupata kujua’ kwamba Yesu alikuwa Bethania ingeelekea zaidi kuwa ilitokea kabla ya yeye kuingia Yerusalemu, na inaweza i kuwa ilisaidia kufanya Kristo apokewe kwa shauku wakati alipopanda kuuingia mji huo “siku iliyofuata, mchana wa Nisani 9.

Uchunguzi zaidi uliofanywa kwa makini kisha ukaongoza kukata shauri hivyo unaonyeshwa katika kuchapishwa-chapishwa hivi majuzi kwa orodha inayosema “Matukio Makuu ya Maisha ya Yesu ya Kidunia,” kama vile katika chapa ya 1985 ya The Kingdom Interlinear Translation of the Greek Scriptures. Ingawa huenda hili likawa ni jambo linaloelekea kuwa dogo, linaonyesha jinsi sisi sote tunavyoweza kukua katika maarifa na ufahamu wa mambo madogo-madogo ya Neno la Mungu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki