Wewe Una Maoni Gani Kuhusu Amri Kumi?
WATU huwa na maoni mbalimbali kuhusu Amri Kumi za Biblia. Waadventi wa Siku ya Saba husema kwamba Amri Kumi zinafunga watu wote katika wajibu wa kuzifuata. Walutheri huziona kuwa ndilo “fungu bora zaidi la sheria ambazo zimepata kutolewa ambazo mtu aweza kuzitumia atengeneze maisha yake.” “Kwa kueleweka ifaavyo,” aeleza mneni mmoja Mkatoliki, “Amri Kumi zingali zaandaa msingi wa maisha ya Kikristo.”
Hivyo, ingawa vikundi fulani vya kidini huamini kwamba twapaswa kuzitii Amri Kumi kwa kufuatilia sana kila nukta iliyoandikwa humo, vingine huzifikiria kuwa mwongozo tu wa mwenendo timamu wa kiadili. Kweli kweli, kulingana na Encyclopcedia of Religion and Ethics, “labda hakuna hati yoyote ya kibinadamu ambayo imekuwa na uvutano mkubwa zaidi juu ya maisha ya kidini na ya kiadili kuliko lile Fungu la Maneno Kumi [Amri Kumi].” Kwa nini iko hivyo? Kwanza fikiria zasema nini. Hizo ni fupi, zenye kueleza mengi, na zenye kani nyingi. Lakini yakupasa wewe uwe na maoni gani kuhusu Amri Kumi? Zina maana gani kwako wewe?
[Sanduku katika ukurasa wa 3]
AMRI KUMI
1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia . . .
3. Usilitaje bure jina la Bwana [Yehova, NW], Mungu wako . . .
4. Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; . . . usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako . . .
5. Waheshimu baba yako na mama yako
6. Usiue [kuua mtu kimakusudi, NW].
7. Usizini.
8. Usiibe.
9. Usimshuhudie jirani yako uongo.
10. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.—Kutoka 20:3-17.