Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 2/15 uku. 3
  • “Enzi ya Pupa”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Enzi ya Pupa”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Imeenea Kadiri Gani?
  • Pupa Itakomeshwa
  • Wazia Ulimwengu Usio na Pupa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Fanikiwa Katika Kuepuka Mtego wa Pupa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Endeleeni Kuepuka Mtego wa Pupa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Unaweza Kutoka Kwenye Mitego ya Shetani!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2021
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 2/15 uku. 3

“Enzi ya Pupa”

IKIWA binadamu ana shida ya kukomesha mafua, awezaje kukomesha maradhi ya pupa yaliyo ya kutatanisha zaidi?

Yaonekana kwamba hata si lazima watu wajifunze upa na ubinafsi—ni wazi yapo tangu utotoni. Waweza kuona hivyo kwa kutazama wadema (watoto wanaoanza kutembea) wawili wakichezea wanasesere wao.

Pupa ya wanadamu mmoja mmoja ipo kwa wingi na ni mbaya vya kutosha, lakini mamilioni huathiriwa vibaya na pupa ya kitaifa au kimataifa. Kielelezo ni biashara ya kimataifa ya dawa za kulevya. Gazeti moja la Kihispania ladai kwamba hii ndiyo biashara kubwa zaidi ulimwenguni—ya dola milioni 300 elfu kwa mwaka. Maisha za mamilioni huharibiwa, na vifo vya mapema husababishwa na utumizi mbaya wa dawa za kulevya. Ni nini kisababishi halisi cha vuvumko hili kubwa lenye kuogopesha sana la biashara ya dawa za kulevya? Bila shaka, ni pupa.

World Press Review yakazia matilaba hii ya pupa. Yanukuu Cambio 16 ambalo ni gazetihabari la Madrid, ambalo lathibitisha kwamba “huwa ni vigumu nchi zifanyizaji kupata hata asilimia 10 hadi 20 ya faida zote zipatikanazo kutokana na mauzo ya dawa za kulevya. Asilimia 10 nyingine hurudishwa ndani ya mfumo wa uchuuzi kwa kuingizwa tena katika maabara, magari, na silaha. . . . Kiasi kinachosalia huingia katika nchi zinazonunua vitu hivyo na katika mbinu za kodi za mfumo wa benki wa ulimwengu.”

Hiyo yakanusha oni la kwamba uhitaji ndiyo husababisha pupa, kwamba pupa ni tabia ya maskini au wenye mapendeleo machache tu. Kwa uwazi, pupa ni kosa la ubinadamu lililoenea kwa mapana ambalo lahusisha ndani msururu mzima wa jamii, kutia na wale wasio na uhitaji kamwe. Moja ya tabia ngeni za pupa ni kwamba ni yenye hila—hata watu ambao kwa kawaida huridhika na kura yao maishani hudhihirisha pupa wakipewa fursa bila kuitarajia.

Mwanasafu Meg Greenfield aomboleza hivi: “Ni jambo la kushusha moyo sana kufungua karatasi-habari siku yoyote ile na kusoma kuhusu mabaraza mashuhuri ya waamuzi na waongozi maalumu wa mashtaka, miito yenye kutilika shaka, pirikapirika, ulanguzi na hadaa. Hata ikikubaliwa kwamba baadhi ya mashtaka yenye kutajwa huwa hayana msingi na mengine hutiliwa chumvi, kwangu inakuwa wazi kwamba mara kwa mara watu waliruhusiwa kuponyoka walipofanya mambo ambayo hayangalipasa kamwe kuruhusiwa. . . . Hii ndiyo kadiri tuliyofikia: hata kadiri kubwa ya kupenda wengine ni kwa kujianisi, ni kwa pupa.”

Imeenea Kadiri Gani?

Pupa si jambo jipya miongoni mwa ainabinadamu, ingawa bila shaka imechapuka sana kwa sababu ya misongo ya maisha ya karne ya 20. Pupa imeenea kwa mapana sana hivi kwamba tahariri moja katika The Christian Century yagawia mwongo wa miaka ya 1980 jina ambalo yahisi lina ulinganifu na majina kama vile “Enzi ya Wasiwasi” ya miaka ya 1950 au ile ya “Mwongo wa Mimi Kwanza” wa miaka ya 1970. Yaibandika miaka ya 1980 “Enzi ya Pupa”!

Leo, pupa yaweza kuonwa katika kila eneo ambamo watu hukusanyika pamoja—kazini, shuleni, na katika jumuiya kwa ujumla. Uvutano wayo wenye kufisidi umepenya ndani ya biashara, siasa, na hata katika dini kubwa-kubwa za ulimwengu.

Sana-sana, pupa husitawi ikawa ufisadi usio halali au ukopi. Mathalani, The Canberra Times laihesabia Australia sifa mbaya ya kuongoza ulimwengu katika ukopi wa bima ya magari. Law Society Journal la Australia laonekana kuwa launga mkono jambo hilo, likitaarifu hivi: “Madai/taarifa za ukopi ambazo hufanywa na watu wenye bima husababisha kila mwaka hasara ya mamilioni ya dola kwa kampuni za bima na watu wasio na bima ya moja kwa moja.” Jarida hilo laongezea kwamba “ni tatizo zito zaidi, hasa kuhusu uteketezaji ovyo wa mali, kupora magudi, na bima ya magari na vilivyomo nyumbani.”

Kwa hiyo ni rahisi kuelewa ni kwa ninj watu wengi hulicheka lile wazo la kwamba siku moja pupa itakomeshwa. Naam, wao wahisi kwamba pupa itakuwa nasi sikuzote na kwamba kuwa na ulimwengu usio na pupa ni ndoto isiyowezekana.

Pupa Itakomeshwa

Dai hilo lenye kusikika kuwa lisilowezekana laweza kufanywa kwa msingi gani? Msingi walo ni uhakika wa kwamba tayari kuna ufanisi wa maisha yasiyo na pupa. Ingawa ufanisi huu si mkamilifu, waonyesha jambo liwezalo kufanywa kukiwa na elimu na hamasisho ifaayo. Makala inayofuata itaonyesha jinsi hasa kwaweza kuwako ulimwengu mzima usio na pupa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki