Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 9/1 uku. 3
  • Uhai Baada ya Kifo Maswali Ambayo Hayajajibiwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uhai Baada ya Kifo Maswali Ambayo Hayajajibiwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Kuna Uhai Baada ya Kifo?
    Ni Nini Hutupata Tunapokufa?
  • Je, Kuna Uhai Baada ya Kifo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Uhai Baada ya Kifo—Watu Huamini Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Wafu Wako Wapi?
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 9/1 uku. 3

Uhai Baada ya Kifo Maswali Ambayo Hayajajibiwa

“MTU akifa, je! atakuwa hai tena?” (Ayubu 14:14) Swali hili, lililotokezwa karne kadhaa zilizopita na Ayubu mzee wa ukoo, limefikiriwa na watu katika kila jamii muda wa enzi zilizopita, na hakujapata kuwa na upungufu wa majibu yaliyopendekezwa.

Wagiriki wa kale walidai kwamba nafsi za wafu ziliendelea kuwa hai. Hizi zilivushwa mto Styx kwenda kwenye makao mapana sana ya chinichini ya ardhi yaitwayo ulimwengu wa chini. Huko mahakimu walizihukumu nafsi kwenye mateso katika gereza lenye kuta za kimo kirefu ama kwenye uraha-mustarehe katika nyanja za Elisia. Jamii nyingine za kale zilifikiri kwamba nafsi zilipata kuwa nyota au nyota-mkia. Na bado wengine walishikilia kwamba nafsi zilimulika nuru zikavutwa kupelekwa kwenye mwezi; kila mwezi wakati mwezi ulipokuwa mpevu, nafsi zilihamishwa kupelekwa kwenye jua.

Leo, nadharia zinazohusu uhai baada ya kufa zaendelea kuwa tele. Wahindu na Wabuddha huamini mgeuko-geuko wa nafsi kuwa maumbo mbalimbali. Waislamu hufundisha kwamba nafsi huendelea kuwa hai baada ya kifo cha mwili na kwamba kwenye hukumu ya mwisho zitaenda paradiso ama helo. Waprotestanti walio wengi hufundishwa kwamba nafsi huendelea kuishi baada ya kifo ili zikawe na uraha-mustarehe wa kimbingu au mateso katika miali ya helo. Nao Ukatoliki huongeza Limbo na purgatori kwenye masimulizi hayo.

Katika mabara fulani, imani zinazohusu zile zidhaniwazo kuwa ni nafsi za wafu huwa ni mchanganyiko wa mapokeo ya huko na Ukristo wa jina tu. Kwa kielelezo, ni desturi miongoni mwa Wakatoliki na Waprotestanti wengi katika Afrika Magharibi kufunika vioo mtu afapo ili mtu yeyote asiitazame roho ya mfu huyo. Siku 40 baada ya kifo cha mpendwa, familia na marafiki hula karamu kusherehekea kupaa mbinguni kwa nafsi hiyo. Baada ya hapo, kwa kawaida kwenye Krismasi au Siku ya Mwaka Mpya, watu wa ukoo huzuru uwanja wa makaburi na kumimina kileo juu ya kaburi. Wao hata huongea kwa yule mfu, wakiomba mapendeleo na kusimulia habari za familia.

Kwa wazi, mwafaka ni kidogo miongoni mwa dini za ulimwengu juu ya litukialo hasa baada ya kifo. Hata hivyo, katika ulimwengu mzima ni kama kuna mwafaka juu ya kazanio moja la msingi: kutokufa kwa nafsi ya kibinadamu. Mafundisho mengi yaliyoko juu ya uhai baada ya kifo ni namna zenye kutofautiana tu za wazo hili la msingi.

Hata hivyo, maswali kadhaa yenye kusumbua yajitokeza: Wazo la kwamba nafsi haifi latoka wapi hasa? Je! lafundishwa katika Andiko? Ikiwa ndivyo, kwa nini hata imani zisizo za Kikristo hulifundisha? Haya si maswali yapasayo kupuuzwa. Hata uwe unafuata dini gani, kifo ni uhakika ambao ni lazima ukabiliwe. Hivyo masuala hayo yakuhusisha wewe kwa njia iliyo ya kibinafsi sana. Kwa hiyo sisi twakualika uchunguze mambo hayo kwa akili iliyofunguka.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki