Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 9/15 kur. 3-4
  • Waweza Kupata Mali za Bei Kuliko Dhahabu!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Waweza Kupata Mali za Bei Kuliko Dhahabu!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Tafuta, Ukaone”
  • Ukweli Umechafuliwa
  • Washindwa Kumkamata
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Wao Washindwa Kumkamata
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • ‘Hakuna Mtu Mwingine Ambaye Amewahi Kuzungumza Hivyo’
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • “Mtafuteni Yehova, Mwendelee Kuishi”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 9/15 kur. 3-4

Waweza Kupata Mali za Bei Kuliko Dhahabu!

KWELI zilizo katika Biblia zingeweza kufananishwa na dhahabu, fedha, au hazina zilizofichika. Ingawa huenda wewe ukawa hujapata kamwe kutafuta-tafuta madini ya dhahabu au fedha halisi, yaelekea kwamba wang’amua kuwa kufanya hivyo hutaka kazi nyingi ngumu na udumifu. Na mara nyingi mtafutaji madini hukabili mambo ya kukatisha tamaa.

Hata hivyo, mambo hayo ya kukatisha tamaa hayatokei kamwe utafutapo hazina zilizofichika katika Biblia. Angalia uthibitisho huu wenye kutia moyo: “Ukiendelea kuitafuta kama fedha, na kama hazina zilizofichika wewe waendelea kuitafuta, katika kisa hicho utaelewa hofu ya Yehova, nawe utapata maarifa yenyewe ya Mungu.” (Mithali 2:4, 5, NW) Lakini ni lazima utafute.

“Tafuta, Ukaone”

“Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.” Huo ndio ushauri ambao Mafarisayo fulani Wayahudi wa karne ya kwanza walimpa Nikodemo, pia Farisayo. “Tafuta, ukaone.” Ushauri mzuri, kweli kwe-li.  Iliwezekana kuutafuta ukweli na kuupata—kitu ambacho thamani yacho yapita dhahabu kwa mbali.

Hata hivyo, katika kisa hicho hususa, wale waliotoa ushauri huo wa “tafuta, ukaone” walishindwa kutenda kulingana nao. Jinsi gani?

Wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametuma maofisa wakakamate Yesu Kristo. Kwa kuvutiwa sana na njia yake ya kufundisha, maofisa walirudi mikono mitupu. Basi, Mafarisayo wakawauliza: “Je! ninyi nanyi mmedanganyika?” Nikodemo alinena bila woga akasema: “Je! torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia [kusikia kutoka kwake, NW] kwanza, na kujua atendavyo?” Maneno hayo yakatokeza ule ushauri wa “tafuta, ukaone.”—Yohana 7:32, 45-52.

Makuhani na Mafarisayo walikuwa wameshindwaje? Wao hawakujua wala hawakukiri kwamba ingawa Yesu alilelewa katika Galilaya, alizaliwa katika Bethlehemu. Nabii Mika alikuwa ametabiri hivi: “Kutoka kwako wewe [Bethlehemu] atatoka aje kwangu yule ambaye atatawala katika Israeli.” (Mika 5:2, NW) Hivyo basi wanaume hao wenye kuongoza walishindwa kutafuta wakaone sifa za ustahiki wa Yesu kuwa nabii, mmoja ambaye angekuwa mtawala katika Israeli. Hiyo iliongoza kwenye msiba, na yatoa kielezi cha jinsi ilivyo muhimu kutafuta na kuupata ukweli wote juu ya mambo. Lakini mara nyingi ukweli huonwaje?

Ukweli Umechafuliwa

“Ukweli safi, kama dhahabu safi, umeonwa kuwa haufai kuenezwa, kwa sababu wanadamu wamegundua kwamba kuna mafaa zaidi kuuchafua ukweli kuliko wao kujitakasa wenyewe,” akasema mwandikaji mmoja wa karne ya 19. Maneno hayo yangali yenye kutoboa mambo sana kuhusu uwanja wa dini ya kilimwengu! Aliye nyuma ya tamasha za uchafuaji huu wa ukweli ni “baba wa uwongo,” Shetani Ibilisi. (Yohana 8:44, NW; Ufunuo 12:9) Yeye hutumia dini bandia kuchafua mafundisho ya kweli juu ya masuala muhimu kama haya: Mungu ni nani? Yesu ana uhusiano gani na yeye? Ni nini kitakachopata dunia na ainabinadamu mwishowe?

Makuhani na Mafarisayo wangaliweza kutafuta-tafuta ukweli na kuupata. Wangaliweza kupata mali za bei sana kuliko dhahabu. Naam, wangaliweza kuupata ukweli wote juu ya Yesu kwa ‘kusikia kutoka kwake na kujua alilokuwa akitenda,’ kama vile Nikodemo alivyodokeza. Kama wangalikuwa wenye moyo mweupe katika kufanya hivyo, bila shaka Yesu angaliwaeleza mambo, kama alivyofanyia wanafunzi wake. (Marko 4:34) Lakini ni wapi tuwezapo kupata ukweli ulio safi leo? Kwa kweli, je! kuna uthibitisho wowote kwamba twaweza kuutafuta ukweli wote na kuupata kwa mafanikio?

[Picha katika ukurasa wa 4]

Viongozi wa kidini wangaliweza kuupata ukweli wote juu ya Yesu kwa ‘kumsikia’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki