Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 3/1 uku. 22
  • Yehova Amthawabisha Kijana Mwaminifu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova Amthawabisha Kijana Mwaminifu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Kufurahisha Mioyo ya Wazazi Wako
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Tunawafurahia Vijana Wanaotembea Katika Njia ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Kutoa Ushahidi Huzaa Tunda Nyumbani na Shuleni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Je, Unamsaidia Mtoto Wako Kumchagua Yehova?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 3/1 uku. 22

Wapiga Mbiu ya Ufalme Waripoti

Yehova Amthawabisha Kijana Mwaminifu

VIJANA waaminifu ni wenye thamani sana machoni pa Yehova. Ono linalofuata la kijana mmoja mwaminifu lapasa kuwatia moyo vijana wengine washike uaminifu wao wa kimaadili wanapomtumikia Yehova.

Katika Argentina mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 11 na ndugu yake mchanga zaidi walijifunza kitabu Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele pamoja na nyanya yao. Mara moja, wazazi wa wavulana hao wakaonyesha upinzani, na kuwakataza wavulana hao wasiende mikutanoni kwenye Jumba la Ufalme. Kwa muda fulani, ili wakahudhurie mikutano, wavulana waliponyoka kupitia dirisha la bafu, kuruka kwenye varanda, na kutoka hapo walipanda ukuta kuingia varanda ya jirani yao na kuendelea hadi Jumba la Ufalme. Halafu mtu fulani akamwambia mama yao kwamba walikuwa wakihudhuria mikutano ya Mashahidi wa Yehova. Mama yao akatisha kuwapiga, na hilo likamwogopesha yule mvulana mchanga zaidi, ambaye akaacha kujifunza. Lakini yule mkubwa zaidi aliendelea tu. Kwa miaka mitano aliweza kuhudhuria mikutano bila wazazi wake kujua.

Alipofika umri wa miaka 16, alitaka kufanya mtaala katika shule ya upili ambao haukutolewa katika mji wake wa nyumbani. Kuwa mbali na nyumbani kungempa uhuru zaidi wa kufuatia kweli. Wazazi wake walikubali aende, na mambo yalikuwa mazuri kwa miezi mitatu. Kisha mwalimu mkuu wa shule akawajulisha wazazi wake kwamba mwana wao hakuwa anasalimu bendera wala kuimba wimbo wa taifa. Mbele ya mwalimu mkuu, wazazi wake, karani, wakili, na maprofesa kumi, yule kijana aliweza kutoa ushahidi bora sana juu ya ni kwa sababu gani asingeweza kwa kudhamiria kufanya vitendo hivyo. (Kutoka 20:4, 5) Wazazi walikasirika sana. Mama alijitwalia bastola, akikusudia kumpiga risasi nyanya, ambaye alifikiri kuwa ndiye mwenye kusababisha hilo. Lakini hakuweza kamwe kumpata akiwa peke yake.

Baadaye, kwa dokezo la rafiki mmoja wa familia na kwa kibali cha mwalimu mkuu wa shule, wazazi waliamua kumweka kijana huyo katika kliniki ya walio na ugonjwa wa akili, wakifikiri kwamba utibabu wa daktari wa magonjwa ya mawazo ungemfanya aache imani yake. Wafanyakazi wa kliniki walimpeleka mvulana huyo kilometa 100 kutoka hapo kwa gari na kumpiga sindano za vipimo vikubwa vya insulini na dawa nyinginezo mpaka akapoteza fahamu. Alipoamka, hakuwa anajua mahali alipo hata kidogo, hakuwa anajua mtu yeyote, na akapatwa na kutoweza kukumbuka kwa kadiri fulani. Baada ya uchunguzi mwingi wenye uangalifu madaktari hawakuweza kupata ugonjwa wowote wa akili kwake. Lakini kliniki hiyo iliendelea na utabibu wayo. Alipokuwa na fahamu, mvulana huyo alikuwa akisali daima kwa Yehova asimwache na kumwomba ampe nguvu ya kuvumilia. Yehova alimlinda, na hatimaye aliachiliwa kutoka kliniki hiyo.

Katika pindi moja mwalimu mkuu wa shule alimwuliza mvulana huyo kama alikuwa tayari kujikania maneno ya kwanza. Aliposema la, mwalimu mkuu aliwaambia wazazi wamrudishe kwenye kliniki kwa sababu alikuwa mwenye kichaa zaidi ya kabla ya hapo. Wazazi wakampeleka kwenye nyumba ya bweni na kumwambia mwanamke mwenye nyumba hiyo ahakikishe kwamba mvulana huyo haendi kwenye mikutano ya Mashahidi wa Yehova. Wazazi walipoondoka, mvulana huyo alipata mshangao ulioje! Wenye nyumba hiyo ya bweni walikuwa Mashahidi wa Yehova! Hatimaye wazazi wakamwachisha utibabu wa ugonjwa wa mawazo, wakisadiki kwamba madaktari walikuwa wamewaambia uwongo. Wakati ule ule Mahakama Kuu Zaidi ya Argentina iliamua kwamba watoto wa Mashahidi wa Yehova wasingeweza kufukuzwa shuleni kwa ajili ya kutosalimu bendera.

Je! majaribu hayo yalimnufaisha kijana huyo mwaminifu? Ndiyo. Yeye ataarifu hivi: “Niliweza kuwatolea ushahidi wenye kuenea sana madaktari, maprofesa, wanafunzi wenzangu, wazazi, na watu wa ukoo, kwa hakika, jiji lote. Wazazi wangu wamepoa kwa kadiri fulani wakawa na wazo bora zaidi juu ya Mashahidi. Sasa, ninapokumbuka wakati wa utoto wangu, naona jinsi Mungu wetu alivyo mzuri ajabu na mwororo katika kushughulikia mtu anayebaki mwaminifu-mshikamanifu kwake. Ni sawa na vile mtunga zaburi alivyosema kwenye Zaburi 27:10: ‘Baba yangu na mama yangu wameniacha, bali BWANA [Yehova, NW] atanikaribisha kwake.’”

Kijana huyo sasa ni mwenye umri wa miaka 23, ameoa, na ni mwenye bidii sana katika utumishi wa Yehova. Kwa kweli, uwezo wa Yehova wa kutegemeza hauna mipaka.—Zaburi 55:22.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki