Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 11/15 kur. 3-4
  • Je, Wafu Wanaweza Kutuona?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wafu Wanaweza Kutuona?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Wazazi Wetu wa Kale Wako Wapi?
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
  • Wafu Wako Wapi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Roho Zisizoonekana—Je! Zinatusaidia? Au Zinatuumiza?
    Roho Zisizoonekana—Je! Zinatusaidia? au Zinatuumiza?
  • Je, Uhofu Wafu?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 11/15 kur. 3-4

Je, Wafu Wanaweza Kutuona?

MWANAMKE mmoja amuua mume wake. Miaka saba baadaye anatishwa na ndoto ambayo anaamini ni ishara ya ghadhabu ya mume wake aliyekufa. Ili kutuliza “roho” yake, amtuma binti yake kumimina matoleo ya kinywaji juu ya kaburi lake.

Binti hajui jinsi ya kusema na roho ya baba yake, maana toleo limetoka kwa mama yake aliyemuua. Kutoka mahali pa kujificha, ndugu yake aangalia. Ajitokeza, naye pamoja na dada yake wamtolea sala baba yao ili awasaidie kulipiza kisasi juu ya mauaji yake.

Mandhari hii imetoka kwa The Libation Bearers, mchezo wa Kigiriki ulioandikwa zaidi ya miaka 2,400 iliyopita. Katika sehemu fulani za ulimwengu, hasa katika Afrika, dhabihu kama hizo hutolewa kando ya kaburi hata leo.

Kwa mfano, fikiria ono la Ibe, anayeishi katika Nigeria. Akiwa amepoteza watoto watatu katika kifo, amwendea mchawi, anayemwambia Ibe kwamba vifo haviji bila sababu—baba ya Ibe aliyekufa amekasirika kwa sababu mazishi yake hayajafanywa kwa njia inayofaa.

Akitenda kulingana na shauri la mchawi huyo, Ibe atoa dhabihu ya mbuzi na kumimina toleo la gin na divai juu ya kaburi la baba yake. Aita roho ya baba yake, akiomba msamaha, akithibitisha upendo wake, na kuomba baraka.

Ibe hana shaka kwamba baba yake anaweza kumwona na kumsikia. Yeye haamini kwamba baba yake hana uhai na kwamba alipokufa “alivuka upande mwingine” kutoka ulimwengu uonekanao mpaka kwenye ulimwengu usioonekana. Ibe anaamini kwamba baba yake ametoka katika ulimwengu wa mwili na damu mpaka kwenye ulimwengu wa roho, makao ya mababu waliokufa.

Ibe asababu hivi: ‘Ingawa baba hayupo tena katika ulimwengu huu, bado ananikumbuka na ananitakia mema. Na kwa sababu sasa yeye ni roho na ana uwezo ulioongezeka, yumo katika hali nzuri zaidi ya kunisaidia kuliko alivyokuwa akiwa mwanadamu duniani. Zaidi ya hayo, anaweza kumfikia Mungu moja kwa moja kwa niaba yangu, kwa maana Mungu ni roho pia. Baba aweza kuwa amekasirika sasa hivi, lakini nikimstahi ifaavyo, atanisamehe na kunibariki.’

Katika Afrika imani ya kwamba wafu huona watu duniani na kuathiri maisha zao ni ya kawaida miongoni mwa wale wanaozoea dini za Kiafrika. Pia ni jambo lililo wazi miongoni mwa wale wanaodai kuwa Wakristo. Kwa mfano, baada ya mwanamke kuolewa kanisani, ni jambo la kawaida kwake kwenda nyumbani kwa wazazi wake kupokea baraka ya kidesturi. Huko mababu wanaombwa, nao humiminiwa toleo la kinywaji. Watu wengi huamini kwamba kukosa kufanya hivi huletea ndoa msiba.

Inafikiriwa kwamba mababu, au roho za mababu waliokufa, huhakikisha kuishi na kusitawi kwa familia zao hapa duniani. Kulingana na maoni haya, wao ni marafiki wenye uwezo sana, wawezao kuleta mavuno mazuri, kuendeleza hali njema, na kulinda watu kutokana na madhara. Wao huomba kwa niaba ya mwanadamu. Hata hivyo, wakipuuzwa au kuudhiwa, wao huleta msiba—magonjwa, umaskini, hata kifo. Kwa sababu hiyo, kupitia dhabihu na desturi, watu hujitahidi kudumisha uhusiano mzuri pamoja na wafu.

Je, wewe waamini kwamba wafu wanahusika sana katika maisha ya watu wanaoishi? Umewahi kusimama kwenye kaburi la mpendwa wako na kujikuta ukizungumza maneno machache, ukidhani huenda akakusikiliza? Basi, kama waliokufa hutuona na kutusikia au sivyo hutegemea lile hutokea wakati wa kifo. Ebu tuchunguze yale Biblia husema kuhusu habari hii ya maana.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki