Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 5/1 uku. 27
  • Wachanga Watangaza Habari Njema Katika Afrika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wachanga Watangaza Habari Njema Katika Afrika
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kutii Maonyo ya Mwili
    Amkeni!—1992
  • “Kutoka Kinywani mwa Watoto Wachanga”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Watoto wa Shule wa Naijeria Wabarikiwa kwa Ajili ya Uaminifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Filipo Ambatiza Ofisa Mwethiopia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 5/1 uku. 27

Wapiga-Mbiu wa Ufalme Waripoti

Wachanga Watangaza Habari Njema Katika Afrika

MUDA MFUPI baada ya ufufuo wa Yesu, mtu mmoja Mwafrika alikuwa akizuru Yerusalemu. Biblia haitaji jina lake. Yeye ajulikana tu kuwa mtu “mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi (“Ethiopia,” NW), aliyewekwa juu ya hazina yake yote.” Kwa nini anatajwa katika Biblia? Kwa sababu malaika alimwelekeza mweneza-evanjeli Mkristo Filipo kumtangazia “habari njema za Yesu.” Mwethiopia huyo alikuwa ndiye Mwafrika wa kwanza katika maandishi kuwa mshiriki wa kutaniko la Kikristo.—Matendo 8:26-39.

Leo, kuna mamia ya maelfu ya Mashahidi wa Yehova katika Afrika. Wao hutumia kila fursa kueleza wengine habari njema za Yesu. Maono yafuatayo yaonyesha kwamba hata wachanga katika Afrika wana fungu la kutimiza.

◻ Sandy na Priya, wasichana wawili wenye umri wa miaka 11 katika Nairobi, Kenya, walikuwa majirani. Wao walifurahia kucheza pamoja na kubadilishana vitabu vya hadithi. Wazazi wa Priya wakaanza kujifunza Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova. Sasa Priya akawa na vitabu vipya aongezee vitabu vyake, kutia ndani kimoja hasa alichokuja kupenda sana, Kumsikiliza Mwalimu Mkuu, kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society. Alishiriki kitabu chake cha Mwalimu Mkuu pamoja na rafiki yake Sandy, na wasichana hao wawili wakaanza kukisoma kwa ukawaida.

Lakini, mama ya Sandy, Una, alikuwa akihudhuria Kanisa Anglikana naye hakutaka binti yake asome vitabu vya Mashahidi wa Yehova. Ajapopingwa na mama yake, funzo hilo liliendelea. Siku moja Sandy alimsihi mama yake asikilize mazungumzo yao mara moja tu. Sura ambayo wasichana hao walisoma siku hiyo ilikuwa na kichwa “Watu Wawili Walioadhimisha Ukumbusho wa Siku ya Kuzaliwa.” Una alisikiliza akavutiwa sana. Upesi akamwendea mama ya Priya akiwa na maswali mengi ya Biblia.

Mama ya Priya akafanya mpango ili Shahidi mmoja ajifunze Biblia pamoja na Una. Upesi Una mwenyewe alikuwa akielezea wengine mambo aliyokuwa akijifunza pamoja na mfanyakazi mwenzake Dolly. Na wakati uo huo, Priya mwenye umri wa miaka 11 aliendelea kufanya maendeleo na kuamua kuonyesha wakfu wake kwa Yehova Mungu kwa ubatizo wa maji katika mkusanyiko wa wilaya wa Mashahidi wa Yehova. Katika mkusanyiko uo huo, kwa furaha kubwa ya Priya, Una na Dolly walibatizwa pia!

◻ Kuna nchi fulani za Kiafrika ambako kazi ya Mashahidi wa Yehova haijaandikishwa rasmi. Katika mojayapo nchi hizo, kuna hali ya ujumla ya kuachilia utendaji wa kidini na itikadi za Mashahidi. Katika shule moja katika nchi hiyo, mvulana mmoja mwenye umri wa miaka saba na nduguye mwenye miaka sita—watoto wa Mashahidi—waliruhusiwa kuondoka darasani wakati wa sala za kidini.

Siku moja mwalimu mpya alisisitiza kwamba wavulana hao wajiunge na sala pamoja na watoto wengine. Mvulana mkubwa alikataa naye akapigwa na mwalimu. Ndugu yake mdogo, Shadrack, mwenye miaka sita, akasisitiza kumwona mwalimu mkuu katika ofisi yake. Mwalimu mkuu pamoja na mwalimu mpya wakamwuliza ni kwa nini hakutaka kujiunga na wengine. Walimwuliza kama aliogopa kupigwa na wazazi wake. Yeye alijibu katika Kiarabu sanifu sana: “La, Mungu ninayemwabudu si Mungu wa machafuko bali wa utaratibu. Siwezi kuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova nyumbani na niwe katika dini nyingine shuleni!” Matokeo yakawa kwamba aliruhusiwa kuondoka.

Baada ya kubatizwa, yule Mwethiopia aliyetajwa katika kitabu cha Matendo “alikwenda zake akifurahi.” (Matendo 8:39) Ndivyo ilivyo leo, wapiga-mbiu wa Ufalme katika bara kubwa la Afrika hushangilia katika pendeleo la ‘kutangaza habari njema za Yesu.’—Matendo 8:35.y

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki