Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 8/15 kur. 3-4
  • Unaweza Kuishije Katika Ujirani Hatari?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unaweza Kuishije Katika Ujirani Hatari?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kudumisha Mtazamo Chanya
  • Ulimwengu Usio na Uvunjaji wa Sheria—Wewe Unautaka Kiasi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Pigano Linaloshindwa Kudhibiti Uhalifu
    Amkeni!—1998
  • Wakati Ambapo Hakukuwa na Uhalifu
    Amkeni!—1998
  • Wewe Unataka Uhalifu Umalizwe?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 8/15 kur. 3-4

Unaweza Kuishije Katika Ujirani Hatari?

“NILIKUWA nikiogopa kila wakati. Niliogopa nikiwa ndani ya lifti. Niliogopa nikiwa ndani ya gari langu. Niliogopa ndani ya nyumba yangu. Kulikuwa na uhalifu kila mahali. Watu walikuwa wakinyang’anywa vitu kila wakati,” asema Maria. Je, wewe unahisi kama mwanamke huyo Mbrazili, kuogopa unakoishi, hasa katika giza la usiku?

Kusoma hadithi za upelelezi huenda kukasisimua, lakini katika maisha halisi mara nyingi hakuna matokeo mazuri. Uhalifu fulani huenda usisuluhishwe. Au kwa habari ya mauaji ya kukusudia, mtu fulani analazimika kuendelea kuishi bila mume, baba, au mwana, bila mke, mama, au binti. Je, uhalifu wenye jeuri unazidi kuongezeka katika eneo lako? Je, wewe unatamani mahali penye utulivu ambapo familia yako ingeweza kuwa salama? Au, ikiwa unalazimika kulea watoto wako katika eneo lenye uhalifu mwingi, unaweza kufanya nini ili uendelee kuishi?

Kwa kweli, bado kuna majiji yasiyokuwa na uhalifu mwingi. Katika nchi nyingi, bado watu huishi katika sehemu za mashambani zilizo tulivu au katika vijiji vyenye starehe. Lakini mambo yanabadilika haraka hata katika maeneo yaliyokuwa hayana uhalifu mbeleni. Kwa kielelezo, katika Brazili miaka 50 iliyopita, asilimia 70 ya wakaaji waliishi sehemu za mashambani. Sasa asilimia 70 huishi majijini. Fursa ya kupata kazi imeleta ongezeko la matatizo kama vile uhalifu na jeuri mijini. Uwe unaishi katika eneo hatari au salama, bado ni lazima uende kazini au shuleni na kufanya mambo mengi mbali na nyumbani.

Akiutambua “ugonjwa wa woga mwingi,” ulioenea mkuu wa polisi katika Rio de Janeiro anataja ukosefu wa haki katika jamii na uhalifu wa magenge kuwa visababishi. Yeye pia anahisi kwamba magazeti na televisheni zinachangia hofu inayoongezeka, “zikiwavunja watu moyo kwa habari zenye msiba.” Uzoefu wa dawa za kulevya, mvunjiko wa familia, na elimu ya kidini yenye makosa pia inachangia uvunjaji wa sheria wenye kuongezeka. Na wakati ujao utakuwaje? Je, mfululizo wa maonyesho ya jeuri ukionyeshwa katika vitabu na filamu yakiwa vitumbuizo yatafanya watu wasijaliane? Je, maeneo yanayofikiriwa hayana uhalifu yatakuwa hatari pia?

Kwa kuwa jeuri huumiza sana mtu, tuna tamaa yenye nguvu ya kuwa salama. Si ajabu kwamba wakaaji wenye kujali wanadai kuwe na polisi wengi zaidi barabarani na vifungo vikali zaidi au hata adhabu ya kifo! Ijapokuwa ni hatari, watu wengine hununua bunduki kwa ajili ya kujilinda. Wengine wakitaka wenye mamlaka wadhibiti uuzaji wa bunduki. Lakini ingawa kuna habari mbaya kwamba jeuri inaongezeka, hakuna haja ya kukata tamaa. Kwa kweli, wakaaji wengi wa majiji makubwa kama Johannesburg, Mexico City, New York, Rio de Janeiro, na São Paulo hawajawahi kamwe kuibiwa. Ebu tuchunguze jinsi watu hukabili uhalifu katika ujirani hatari.

Kudumisha Mtazamo Chanya

Kuhusu eneo lililo na uhalifu mwingi sana, mwandikaji mmoja atoa maelezo juu ya “ujuzi na uvumilivu wa maelfu ya Wabrazili ambao wameweza kuishi kwa kadiri fulani ya heshima na uungwana zijapokuwa hali ngumu za kuishi.” Baada ya miaka 38 katika Rio de Janeiro, Jorge asema hivi: “Mimi huepuka barabara na visehemu fulani na kuepuka kuonyesha udadisi wowote. Pia mimi huepuka kutembea barabarani usiku na sidhihirishi hofu kupita kiasi. Ingawa najihadhari, mimi huona watu kuwa kama wanyoofu, nikiwatendea kwa staha na heshima.”

Ndiyo, epuka matatizo yasiyo ya lazima. Shughulika na mambo yako mwenyewe. Daima usipuuze uhakika wa kwamba hofu nyingi kupita kiasi yaweza kuathiri mfumo wako wa neva, ukifanya hata watu wenye adabu kutenda kwa upumbavu. Kuhusu kazi yake katika maeneo hatari, Odair aonelea hivi: “Mimi hujaribu kuwa na maoni chanya, bila kutia akilini mwangu hofu ya mambo mabaya ambayo huenda yakatokea kwa sababu jambo hilo hutokeza mkazo na hofu isiyo ya lazima. Mimi hujaribu kuonyesha heshima kwa watu wote.” Zaidi ya kuwa macho na kukaa mbali na watu anaoshuku, yeye hujiongezea msaada mwingine wa kuzuia hisia zake za moyoni: “Zaidi ya yote, mimi husitawisha uhakika katika Yehova Mungu, nikikumbuka kwamba hakuna kitu asichoweza kuona na chochote kifanyikacho ni kwa ruhusa yake.”

Hata hivyo, hakuna atakaye kuishi kwa hofu wakati wote. Zaidi ya hayo, ni nani atakana kwamba hofu na mkazo mwingi kupita kiasi ni wenye kudhuru hisia-moyo na afya ya kimwili? Hivyo basi, kuna tumaini gani kwa wale ambao huhofu kwamba huenda wakashambuliwa wakati wowote? Kwa kuwa wengi wanaogopa kwamba hali mbaya zaidi kuhusu uhalifu bado inakuja, je, kweli tutapata kuona mwisho wa ujeuri? Tunakukaribisha usome makala ifuatayo, “Hofu Itakwisha Lini?”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki