Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 9/1 uku. 30
  • Baba Aliye Tayari Kusamehe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Baba Aliye Tayari Kusamehe
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Alipotea na Kupatikana
  • Masomo Kwetu
  • Mwana Aliyepotea Arudi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Hadithi ya Mwana Mpotevu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Wakati Mwana Mpotevu Anapopatwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kupokea kwa Uchangamshi Wale Wanaorudi
    Kuokolewa Kuingia Katika Dunia Mpya
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 9/1 uku. 30

Walifanya Mapenzi ya Yehova

Baba Aliye Tayari Kusamehe

IMEITWA hadithi fupi iliyo maarufu zaidi ambayo imepata kuandikwa—kukiwa na sababu nzuri. Mfano wenye somo wa Yesu juu ya upendo wa baba kwa mwana wake aliyepotea ni kama dirisha ambalo kupitia hilo twapata mwono mtukufu wa huruma ya Mungu kuelekea watenda-dhambi wenye toba.

Alipotea na Kupatikana

Mtu fulani alikuwa na wana wawili. Yule kijana zaidi akamwambia hivi: ‘Nataka urithi wangu sasa, badala ya kungoja hadi ufe.’ Huyo baba akakubali, yaelekea akimpa thuluthi ya vyote alivyomiliki—fungu halali la aliye kijana zaidi kati ya wana hao wawili. (Kumbukumbu la Torati 21:17) Huyo kijana alikusanya mali zake haraka-haraka na kusafiri hadi nchi ya mbali ambako alitumia fedha zake zote akifuatia maisha ya ufasiki.—Luka 15:11-13.

Kisha njaa kali sana ikatukia. Kwa kukosa tumaini, mwanamume huyo kijana alikubali kufanya kazi ya kuchunga nguruwe—kazi ya kudharauliwa kwa Myahudi. (Mambo ya Walawi 11:7, 8) Chakula kilikuwa nadra sana hivi kwamba alianza kutamani matumba ya mkarobu yaliyokuwa chakula cha nguruwe! Hatimaye, mwanamume huyo alirudiwa na fahamu zake. ‘Watumishi wa baba yangu wanalishwa vizuri zaidi kuliko mimi!’ akafikiria. ‘Nitarudi nyumbani, nitubu dhambi zangu, na kuomba kuwa mmoja wa wanaume walioajiriwa wa baba yangu.’a—Luka 15:14-19.

Huyo mwanamume kijana akajikokota kurudi nyumbani. Bila shaka kuonekana kwake kulikuwa kumebadilika sana. Ingawa hivyo, baba yake alimtambua “alipokuwa angali mbali sana.” Akisukumwa na sikitiko, alimkimbilia mwanaye, akamkumbatia, na “kumbusu kwa wororo.”—Luka 15:20.

Kukaribishwa huko kwa shauku kulifanya iwe rahisi kwa yule mwanamume kijana kujiondolea mwenyewe mzigo wenye kulemea. “Baba,” akasema, “nimefanya dhambi dhidi ya mbingu na dhidi yako. Sistahili tena kuitwa mwana wako. Unifanye niwe kama mmoja wa wanaume wako walioajiriwa.” Huyo baba akawaita watumwa wake. “Upesi!” akawaamuru. “Leteni nje kanzu, iliyo bora zaidi, mmvike hiyo, na mtie pete mkononi mwake na makubazi miguuni mwake. Nanyi leteni fahali mchanga aliyenoneshwa, mchinjeni na acheni tule na kujifurahisha wenyewe, kwa sababu huyu mwana wangu alikuwa amekufa naye akaja tena kwenye uhai; alikuwa amepotea naye akapatikana.”—Luka 15:21-24.

Karamu kubwa ikaanza, kutia na muziki na kucheza dansi. Yule mwana mwenye umri mkubwa zaidi alisikia mvumo wa muziki na wa kucheza dansi alipokuwa akirudi kutoka shambani. Alipopata kujua kwamba ndugu yake alikuwa amekuja nyumbani na kwamba hiyo ndiyo iliyokuwa sababu ya karamu, akawa na hasira ya kisasi. ‘Nilikutumikia kwa miaka mingi, wala sikukosa kukutii kamwe, na bado hukunipa kamwe mwana-mbuzi nimfurahie pamoja na rafiki zangu,’ akamlalamikia babaye. ‘Lakini sasa mara tu mwana wako aliyepoteza bure utajiri wako arudipo, wamwandalia karamu.’ ‘Mtoto,’ babaye akamjibu kwa wororo, ‘sikuzote umekuwa nami, na vyote vilivyo vyangu ni vyako. Lakini ilitupasa kushangilia kwa sababu ndugu yako aliyekuwa mfu amekuja kwenye uhai. Alipotea kisha akapatikana.’—Luka 15:25-32.

Masomo Kwetu

Baba katika huo mfano wenye somo wa Yesu awakilisha Mungu wetu mwenye rehema, Yehova. Sawa na mwana aliyepotea, watu fulani huacha usalama wa nyumba ya Mungu kwa wakati fulani lakini hurudi baadaye. Yehova huwaonaje? Wale ambao humrudia Yehova wakiwa wenye toba ya moyo mweupe wanaweza kuhakikishiwa kwamba “yeye hatateta sikuzote, wala hatashika hasira yake milele.” (Zaburi 103:9) Katika huo mfano wenye somo, baba alikimbia ili kumkaribisha mwana wake. Vivyo hivyo, Yehova ana nia na ana hamu ya kusamehe watenda-dhambi wenye toba. Yu “tayari kusamehe,” naye husamehe “kabisa.”—Zaburi 86:5; Isaya 55:7; Zekaria 1:3.

Katika mfano wenye somo wa Yesu, upendo wa kweli wa baba ulifanya iwe rahisi kwa mwana kupata ujasiri wa kurudi. Lakini fikiria hili: Ni nini lingetukia ikiwa baba alikuwa amemkana huyo mvulana au katika mfoko wa hasira akamwambia asirudi kamwe? Yamkini mtazamo huo ungalimtenga mvulana huyo daima.—Linganisha 2 Wakorintho 2:6, 7.

Basi, kwa namna fulani, baba alimwekea mwana wake msingi wa kurudi wakati ambapo mwana wake aliondoka. Nyakati fulani, wazee Wakristo lazima waondoe watenda-dhambi wasiotubu kutoka kutanikoni. (1 Wakorintho 5:11, 13) Katika kufanya hivyo, wanaweza kuanza kutayarishia mtenda-dhambi njia ya kurudi kwa kumwonyesha kwa upendo hatua anazoweza kuchukua ili arudishwe wakati ujao. Baadaye kumbukumbu la kusihi huko kutoka moyoni kumewasukuma watu wengi waliopotea kiroho watubu na kumewachochea warudi nyumbani kwa Mungu.—2 Timotheo 4:2.

Huyo baba pia alimwonyesha mwana wake huruma aliporudi. Ilimchukua muda mfupi kuona toba ya moyo mweupe ya huyo mvulana. Kisha, badala ya kusisitiza kwamba huyo mwana asimulie ukiukaji wake kinaganaga, alijishughulisha na kumkaribisha, na akaonyesha furaha kubwa katika kufanya hivyo. Wakristo wanaweza kuiga kielelezo hiki. Wapaswa kushangilia kwamba aliyepotea amepatikana.—Luka 15:10.

Mwenendo wa baba ulionyesha wazi kwamba alitazamia kwa muda mrefu kurudi kwa mwana wake mkaidi. Bila shaka, huko kutazamia kwa baba ni kivuli tu cha tamaa ambayo Yehova anayo kwa wote ambao wameiacha nyumba yake. Yeye “hataki yeyote aangamizwe bali hutaka wote wafikie toba.” (2 Petro 3:9) Kwa hiyo wale ambao hutubu dhambi zao wanaweza kuwa na uhakika wa kwamba watabarikiwa kwa “majira ya kuburudisha . . . kutoka kwa utu wa Yehova.”—Matendo 3:19.

[Maelezo ya Chini]

a Ingawa mtumwa alionwa kuwa sehemu ya watu wa nyumbani, mtumishi wa kuajiriwa alikuwa mfanyakazi wa siku ambaye angeweza kufukuzwa wakati wowote. Huyo mwanamume kijana alisababu kwamba angekuwa tayari kukubali hata mahali pa chini zaidi katika nyumba ya baba yake.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki