Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 12/15 uku. 24
  • Ujambazi Wazuiwa Katika Afrika Magharibi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ujambazi Wazuiwa Katika Afrika Magharibi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Majambazi Wenye Silaha Washambuliapo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Jinsi ya Kununua Gari Lililotumiwa
    Amkeni!—1996
  • Sanduku la Swali
    Huduma Yetu ya Ufalme—1990
  • Gari Lako—Kimbilio au Mtego?
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 12/15 uku. 24

Ujambazi Wazuiwa Katika Afrika Magharibi

Kama ilivyosimuliwa na Eunice Ebuh

“Majambazi wenye silaha walipanga shambulio lao siku ambayo sisi huwa na Funzo la Kitabu la Kutaniko nyumbani mwetu. Sisi huacha lango letu likiwa wazi kabisa kwa ajili ya ndugu na dada na watu wenye kupendezwa. Yaelekea majambazi walijua mazoea yetu na wakati wa mikutano. Twajua kwa hakika kwamba waliiba gari kwingineko na wakaja kutungojea kwenye lango letu siku na wakati wa funzo la kitabu.

“Ilitukia kwamba, juma walilokuja lilikuwa lile la ziara ya mwangalizi wa mzunguko. Badala ya kukutanikia nyumbani kwetu, tulikutanikia kwenye Jumba la Ufalme. Baada ya mkutano kumalizika, kulikuwa na mkutano wa wazee. Kwa kawaida, watoto nami tungekuwa tumeenda nyumbani, lakini mume wangu, ambaye ni mzee, alituomba tumngoje. Alisema asingekawia. Hivyo, tukangoja.

“Baadaye tuligundua kwamba gari halingeweza kuwaka. Mwangalizi wa mzunguko na mume wangu hawakuweza kulitengeneza. Mekanika tuliyemwita hakuweza pia.

“Watoto walilazimika kutembea kwenda nyumbani. Punde baadaye, nilienda nyumbani pia. Nilifika nyumbani yapata saa nne. Wala mimi wala watoto hakuna aliyeingia uani mwa nyumba kwa gari, jambo ambalo lingemaanisha kufungua lile lango kubwa.

“Nilipoingia chumba changu cha kulala, nilisikia mlio wa bunduki, wenye kishindo sana. Nilijiuliza kilichokuwa kikitendeka. Nilijaribu kupigia polisi simu, lakini simu haikufanya kazi. Nilishuka ngazi mbiombio na kufunga mlango wa chuma wa kuingilia, kisha nikaharakisha kufunga mlango wa katikati. Nilizima taa. Watoto wangu walipatwa na hofu ya ghafula, hivyo, nikawaambia watulie. Sote pamoja tulimwomba Yehova atulinde. Wakati uo huo, mume wangu alikuwa bado kwenye Jumba la Ufalme akijitahidi kuliwasha gari.

“Nilitazama nje dirishani nikaona mtu akiwa amelala barabarani nje ya lango. Ilionekana kana kwamba majambazi hao walikuwa tayari wameenda, hivyo, nilimweka mtu huyo aliyejeruhiwa ndani ya gari langu na kumkimbiza hospitalini. Hiyo ilikuwa hatari, lakini nilihitaji kufanya jambo fulani. Hata hivyo, kwa kusikitisha, alikufa siku iliyofuata.

“Ujapokuwa msiba huo, mambo yangeweza kuwa mabaya zaidi. Kuwa na ziara ya mwangalizi wa mzunguko kulimaanisha kutofanyia funzo letu la kitabu nyumbani mwetu. Kuharibika kwa gari letu kulimaanisha kwamba hatukusafiri kurudi nyumbani tukiwa familia. Mume wangu, ambaye wahalifu kwa hakika wangemkamata, alifika nyumbani akiwa amechelewa mno. Haya na mambo mengine yalikuwa kwa manufaa yetu usiku huo.

“Yehova ni ngome yetu na kimbilio letu. Ni kama vile andiko husema: ‘BWANA asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure.’”—Zaburi 127:1.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki