Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w03 4/15 kur. 3-4
  • Watu Wanayaonaje Maadili ya Kiroho Leo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Watu Wanayaonaje Maadili ya Kiroho Leo?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wengi Hawajishughulishi Sana na Dini
  • Maoni ya Watu Kuhusu Maadili Yamebadilika Sana
  • Mchanganyiko wa Imani Mbalimbali
  • Waumini Wako Wapi?
    Amkeni!—1996
  • Kanisa Linalobadilika Katika Ufaransa
    Amkeni!—1993
  • Vijana Hupendezwa na Dini Kadiri Gani?
    Amkeni!—1998
  • Thamani Zinazobadilika Wakati Historia Inapopita
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
w03 4/15 kur. 3-4

Watu Wanayaonaje Maadili ya Kiroho Leo?

“Watu 30 wanaotaka kufunga ndoa wanahudhuria mkutano wa jioni wa [Kanisa Katoliki] ili kupata mashauri kuhusu ndoa. Kati ya watu hao 30, ni 3 tu wanaodai kuwa na imani.”—La Croix, gazeti la Kanisa Katoliki la Ufaransa.

MAADILI yanayofundishwa na dini hayatiliwi maanani tena. Gazeti la kimataifa la Newsweek la Julai 12, 1999, liliuliza hivi kwenye jalada: “Je, Mungu Amekufa?” Gazeti hilo lilisema kwamba inaelekea watu wanaoishi Ulaya magharibi wanaamini hivyo. Gazeti la Le Monde la Ufaransa lilisema hivi kuhusu mkutano wa Kanisa Katoliki uliofanywa huko Roma, Oktoba mwaka huohuo: “Inazidi kuwa vigumu kwa Kanisa kuhubiri ujumbe wake katika jamii ambayo inachukizwa na ujumbe huo. . . . Wakatoliki nchini Italia wana imani mbalimbali. . . . Ubishi kuhusu kuwapo kwa vituo vya mashauri ya kutoa mimba nchini Ujerumani unamtenga papa na watu walio na uhuru wa kuamua na wasiotaka kuambiwa wanayopaswa kufanya. Watu fulani wanasema kwamba raia wa [Uholanzi] wamekubali maadili mapya na mauaji ya huruma kwa sababu watu wengi wa nchi hiyo wameacha kuwa Wakristo.”

Ndivyo ilivyo katika sehemu nyinginezo. Mwaka wa 1999, Askofu Mkuu wa Kanisa la Canterbury, George Carey, alionya kwamba “baada ya kizazi kimoja, Kanisa la Anglikana litakuwa limetoweka.” Katika makala yenye kichwa “Mwisho wa Ukristo Barani Ulaya,” gazeti la Ufaransa Le Figaro lilisema hivi: “Ndivyo ilivyo kila mahali. . . . Watu wanaendelea kutilia shaka maoni kuhusu maadili na mafundisho.”

Wengi Hawajishughulishi Sana na Dini

Idadi ya watu wanaoenda kanisani huko Ulaya inapungua sana. Idadi ya Wakatoliki nchini Ufaransa ambao huhudhuria Misa kila Jumapili inapungua kwa asilimia 10, na ni asilimia 3 hadi 4 tu ya Wakatoliki wanaoishi Paris ambao huenda kanisani kwa ukawaida. Nchini Uingereza, Ujerumani, na katika nchi za Skandinavia, hudhurio ni hilohilo au hata ni chini zaidi.

Viongozi wa dini wanahangaika sana kwa sababu kuna upungufu wa watu wanaotaka kuwa makasisi. Miaka 100 hivi iliyopita kulikuwa na makasisi 14 kwa watu 10,000 nchini Ufaransa, lakini leo kuna kasisi 1 tu kwa watu 10,000. Barani Ulaya, makasisi wanazidi kuzeeka, na upungufu huo umeathiri nchi ya Ireland na Ubelgiji pia. Vilevile, idadi ya watoto wanaohudhuria madarasa ya katekisimu inapungua, na hiyo inasababisha wasiwasi kuhusu kuendelea kuwapo kwa Kanisa Katoliki.

Watu wamepoteza imani katika dini. Ni asilimia 6 tu ya Wafaransa wanaoamini kwamba “kweli inaweza kupatikana katika dini moja tu,” ikilinganishwa na asilimia 15 katika mwaka wa 1981 na asilimia 50 katika mwaka wa 1952. Watu wanazidi kupoteza upendezi katika dini. Idadi ya watu wanaosema kwamba wao si wafuasi wa dini yoyote imeongezeka kutoka asilimia 26 mwaka wa 1980 hadi asilimia 42 mwaka wa 2000.—Les valeurs des Français—Évolutions de 1980 à 2000 (Maadili ya Wafaransa Kuanzia Mwaka wa 1980 Hadi 2000).

Maoni ya Watu Kuhusu Maadili Yamebadilika Sana

Mabadiliko katika maoni ya watu kuhusu maadili yanaonekana pia katika mwenendo wao. Kama ilivyotajwa mapema, watu wengi wanaoenda kanisani kwa ukawaida wanakataa kufuata kanuni za maadili zinazofundishwa kanisani. Hawakubali kwamba viongozi wa dini wana haki ya kuwawekea kanuni za mwenendo. Watu walewale wanaounga mkono msimamo wa papa kuhusu haki za binadamu hukataa kumtii anapozungumzia mambo yanayohusu maisha yao. Kwa mfano, msimamo wake kuhusu kupanga uzazi unapuuzwa na watu wengi, hata na Wakatoliki wengi waliofunga ndoa.

Wafuasi wa dini na watu wasio wa dini katika tabaka mbalimbali ya jamii wana mwelekeo huo. Mazoea yanayokatazwa waziwazi katika Maandiko Matakatifu yanakubaliwa. Miaka 20 iliyopita, asilimia 45 ya raia wa Ufaransa walichukizwa na ngono kati ya watu wa jinsia moja. Leo asilimia 80 ya raia hao wanaona zoea hilo kuwa sawa. Ijapokuwa wengi wao wanapendelea uaminifu katika ndoa, ni asilimia 36 tu wanaoshutumu uzinzi.—Waroma 1:26, 27; 1 Wakorintho 6:9, 10; Waebrania 13:4.

Mchanganyiko wa Imani Mbalimbali

Katika nchi za Magharibi, watu wameanza kuwa na mwelekeo wa kujiamulia wenyewe kile wanachotaka kuamini. Imani fulani inakubaliwa huku nyingine ikikataliwa. Watu fulani hujiita Wakristo huku wakiamini fundisho la kuzaliwa upya katika mwili wa kiumbe mwingine, na wengine wao hukubali mafundisho ya dini mbalimbali. (Mhubiri 9:5, 10; Ezekieli 18:4, 20; Mathayo 7:21; Waefeso 4:5, 6) Kitabu Les valeurs des Français kilisema waziwazi kwamba waumini wengi leo wanaacha kabisa imani inayofundishwa na dini ambazo zimekuwapo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, mwelekeo huo wa kujiamulia unachotaka kuamini unaweza kuwa hatari. Jean Delumeau, mwanahistoria wa masuala ya kidini na mshiriki wa Taasisi ya Ufaransa anasema kwamba mtu hawezi kujianzishia dini yake mwenyewe bila kutegemea dini zilizopo. “Imani haiwezi kudumu isipokuwa na msingi katika dini fulani.” Maadili mazuri ya kiroho yanapaswa kuonekana wazi katika ibada ya mtu. Mambo hayo yanaweza kupatikana wapi katika jamii inayokumbwa na mabadiliko mengi?

Biblia inatukumbusha kwamba Mungu ndiye anayeamua kanuni zinazofaa za mwenendo na maadili, ingawa anawaruhusu wanadamu waamue kama wanataka kuzifuata au la. Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wanatambua kwamba kitabu hicho ambacho kimeheshimiwa kwa muda mrefu kinafaa leo, na kwamba ni ‘taa ya miguu yao na mwanga wa njia yao.’ (Zaburi 119:105) Waliufikiaje mkataa huo? Jambo hilo litazungumziwa katika makala inayofuata.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki