Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 5/95 uku. 7
  • Kwa Nini Uweke Rekodi ya Wasiokuwepo Nyumbani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Uweke Rekodi ya Wasiokuwepo Nyumbani?
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Watu Wasipopatikana Nyumbani
    Huduma ya Ufalme—2007
  • Timiza Huduma Yako Kikamili
    Huduma Yetu ya Ufalme—1988
  • Kampeni ya Pekee Oktoba 16–Novemba 12!
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Je, Una Eneo la Kibinafsi?
    Huduma ya Ufalme—2006
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1995
km 5/95 uku. 7

Kwa Nini Uweke Rekodi ya Wasiokuwepo Nyumbani?

1 Mume na mke Mashahidi walikuwa kwenye utumishi mapema katika siku. Baadaye siku hiyo, walirudi ili washughulikie wasiokuwepo nyumbani katika eneo hilo. Mwanamume mmoja aliwakaribisha na kuwasikiliza kwa makini. Alichukua kitabu Kuishi Milele na akaomba Mashahidi hao warudi. Hakuwa amepata kuongea na Mashahidi wa Yehova kabla ya hapo naye alikuwa na maswali mengi aliyotaka yajibiwe; funzo la Biblia likaanzishwa. Mume na mke hawa walikuwa na shangwe zaidi kupata mtu mwingine mwenye mfano wa kondoo. Je, ungependa kuwa na lililoonwa kama hilo? Kuweka rekodi nzuri ya wasiokuwepo nyumbani na kurudi mara hiyo huenda kukakuwezesha kufanya hivyo.

2 Tumekuwa tukisihiwa mara nyingi tuweke rekodi sahihi ya wasiokuwepo nyumbani na turudi tena karibuni. Kama lililoonwa lililo juu lionyeshavyo, ziara nyingine siku hiyohiyo yaweza kuleta matokeo bora zaidi. Ingawa huenda tukakusudia kutimiza eneo tulilogawiwa, labda hatuna juhudi katika kuweka rekodi ya wale wasiokuwepo nyumbani. Huenda wengine wakasema: ‘Sisi huhubiri eneo letu kila majuma mawili au matatu; hakuna haja ya kuweka rekodi kama hiyo kwa sababu tutarudi upesi hata hivyo.’ Lakini jambo hilo latupa sababu zaidi ya kuweka rekodi. Mahali ambapo eneo latimizwa mara nyingi, kufuatia wasiokuwepo nyumbani hutuwezesha tutafute kabisa wanaostahili. Jinsi gani hivyo?

3 Katika maeneo mengi, asilimia 50 au zaidi ya wakazi hawawi nyumbani wakati wa siku. Hivyo kwa kweli, twafanya eneo kubwa lipatikane kwa kushughulika zaidi na wasiokuwepo nyumbani. Hata kama eneo halifanywi mara nyingi, twaweza kuboresha matokeo jitihada ifanywapo ya kufikia kila mtu kabla ya kutia alama eneo kuwa limefanywa.

4 Kuzuru wasiokuwepo nyumbani mara nyingi kwaweza kupangiwa siku nyingine, hasa mnamo juma hilo. Wengi wanaona ikifaa kurudi siku fulani na wakati tofauti na ile ziara ya kwanza. Unaweza kuchagua kutumia wakati fulani Jumamosi au Jumapili ili kufuatia wasiokuwepo nyumbani wakati wa juma. Kisha tena, makutaniko mengi huona kwamba kufanya marudio hayo saa za mapema za jioni kumekuwa na matokeo mazuri. Huenda wakapata zaidi ya nusu ya wakazi nyumbani.

5 Unapaswa kuweka orodha ya ziara za kurudia katika rekodi zako za kibinafsi. Ukishindwa kurudi mahali ambapo hapakuwa na mtu nyumbani, rekodi yako ya wasiokuwepo nyumbani yapaswa kupewa ndugu anayeshughulikia kikundi, kwa matumizi ya kikundi kitakachofuata katika eneo hilo.

6 Kutoa uangalifu wa karibu kwa upande huu wa huduma yetu kwaweza kuongeza matokeo yetu pamoja na shangwe yetu. Kwaweza kutupatia utoshelezo unaotokana na kujua kwamba tunatafuta kikamili na kujali walio mfano wa kondoo.—Eze. 34:11-14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki