Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/03 uku. 4
  • Video Inayoonyesha Njia Muhimu ya Matibabu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Video Inayoonyesha Njia Muhimu ya Matibabu
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Video Kuhusu Mbinu Muhimu za Matibabu
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Je, Unaahirisha?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2008
  • Je, Uko Tayari Kukabiliana na Matibabu ya Dharura?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2012
  • Je, Unaahirisha Kuijaza?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2010
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2003
km 12/03 uku. 4

Video Inayoonyesha Njia Muhimu ya Matibabu

Wataalamu wa sheria na wa afya wanaendelea kuzingatia masuala ya kimaadili na haki za wagonjwa. Jambo hilo limetokeza njia mpya za matibabu ambazo zinaweza kuwanufaisha Mashahidi wa Yehova. (Mdo. 15:28, 29) Njia hizo zinaonyeshwa katika video Transfusion-Alternative Health Care—Meeting Patient Needs and Rights. Itazame kisha upitie mambo uliyojifunza.—Tahadhari: Video hiyo inaonyesha wagonjwa fulani wakifanyiwa upasuaji, kwa hiyo wazazi wanapaswa kuwa waangalifu wanapoitazama pamoja na watoto wao wachanga.

(1) Kwa nini wataalamu wa tiba wanabadili maoni yao kuhusu kutia damu mishipani? (2) Taja aina tatu za upasuaji mgumu zinazofanywa bila kumtia mgonjwa damu. (3) Ni madaktari wangapi ulimwenguni pote ambao wanakubali kuwatibu na kuwafanyia wagonjwa upasuaji bila kuwatia damu mishipani? Kwa nini wanakubali kutotumia damu? (4) Uchunguzi uliofanywa majuzi unaonyesha nini kuhusu matumizi ya damu? (5) Kutiwa damu mishipani kunaweza kusababisha matatizo gani ya afya? (6) Wataalamu wengi wameona faida gani za kutumia dawa au matibabu ya aina nyingine badala ya damu? (7) Ni nini kinachosababisha upungufu wa damu? Mtu anaweza kupungukiwa damu kadiri gani? Mtu ambaye amepungukiwa damu anaweza kutibiwaje? (8) Ni dawa gani zinazoweza kutumiwa ili mwili wa mgonjwa utengeneze chembe nyekundu za damu haraka zaidi? (9) Madaktari hutumia mbinu gani ili kuzuia damu isitoke kwa wingi wakati wa upasuaji? (10) Je, dawa hizo na njia hizo zinazotumiwa badala ya damu zinaweza kutumiwa kuwatibu watoto na watu walio mahututi? (11) Jambo moja muhimu linalohusu matibabu mazuri ni lipi? (12) Kwa nini ni muhimu kwa Mkristo kuamua mapema ni matibabu gani yasiyohusisha damu atakayokubali? Tunawezaje kufanya jambo hilo?

Kuchagua baadhi ya matibabu yaliyoonyeshwa katika video hii ni uamuzi wa mtu binafsi ukitegemea dhamiri iliyozoezwa na Biblia. Je, umeamua ni matibabu gani yasiyohusisha damu ambayo wewe na watoto wako mngependa? Watu wa familia yako ambao si Mashahidi wanapaswa kujua uamuzi wako na sababu ya kuamua hivyo.—Ona “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” katika Mnara wa Mlinzi la Juni 15 na Oktoba 15, 2000.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki