Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 1/06 uku. 7
  • Video Kuhusu Mbinu Muhimu za Matibabu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Video Kuhusu Mbinu Muhimu za Matibabu
  • Huduma ya Ufalme—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Video Inayoonyesha Njia Muhimu ya Matibabu
    Huduma Yetu ya Ufalme—2003
  • Je, Unaahirisha?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2008
  • Je, Uko Tayari Kukabiliana na Matibabu ya Dharura?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2012
  • Je, Unaahirisha Kuijaza?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2010
Pata Habari Zaidi
Huduma ya Ufalme—2006
km 1/06 uku. 7

Video Kuhusu Mbinu Muhimu za Matibabu

Wanasheria na wataalamu wa afya wanazingatia zaidi na zaidi maoni na haki za wagonjwa. Jitihada zao zimetokeza mbinu mpya za matibabu zinazoweza kutumiwa kwa wagonjwa ambao ni Mashahidi wa Yehova. (Mdo. 15:28, 29) Hayo ndiyo mambo yanayozungumziwa katika video Transfusion-Alternative Health Care—Meeting Patient Needs and Rights. Itazame video hiyo, kisha upitie mambo ambayo umejifunza.—Taarifa: Kwa kuwa video hiyo ina picha za watu wanaofanyiwa upasuaji, wazazi wanapaswa kutumia busara wakiamua kuitazama pamoja na watoto wao.

(1) Kwa nini wahudumu fulani wa afya wanabadili maoni yao kuhusu kutia damu mishipani? (2) Taja aina tatu za upasuaji mgumu unaoweza kufanywa bila kumtia mgonjwa damu. (3) Ni madaktari wangapi duniani ambao wamekubali kuwatibu au kuwafanyia wagonjwa upasuaji bila kuwatia damu? Kwa nini wamekubali kufanya hivyo? (4) Uchunguzi uliofanywa majuzi katika hospitali mbalimbali umeonyesha nini kuhusu matumizi ya damu? (5) Kutiwa damu mishipani kunaweza kusababisha matatizo gani ya afya? (6) Wataalamu fulani wamekata kauli gani kuhusu manufaa ya matibabu yasiyohusisha damu? (7) Ni nini kinachosababisha upungufu wa damu? Mtu anaweza kupungukiwa damu kadiri gani na bado asiwe mahututi? Mtu mwenye upungufu wa damu anaweza kusaidiwaje? (8) Mwili wa mgonjwa unaweza kuchochewaje utengeneze haraka zaidi chembe nyekundu za damu? (9) Ni mbinu gani zinazotumiwa na madaktari ili kumzuia mgonjwa asitokwe damu nyingi wakati anapofanyiwa upasuaji? (10) Je, mbinu za matibabu zisizohusisha damu zinaweza kutumiwa kwa mafanikio kwa watoto wachanga au wakati wa dharura? (11) Matibabu mazuri yanahusisha kanuni gani muhimu? (12) Kwa nini ni muhimu sisi Wakristo tuamue mapema tungependa matibabu gani yasiyohusisha damu? Tunaweza kufanyaje uamuzi huo?

Kuchagua baadhi ya matibabu yaliyoonyeshwa katika video hiyo ni uamuzi wa mtu binafsi unaotegemea dhamiri yake inayoongozwa na Biblia. Je, umeamua ni matibabu gani yasiyohusisha damu ambayo wewe na watoto wako mngependa? Watu wa familia yako ambao si Mashahidi wanapaswa kuelewa vizuri uamuzi wako na sababu yako ya kuufanya.—Ona “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” katika Mnara wa Mlinzi la Juni 15, 2004, na Oktoba 15, 2000.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki