DVD Yenye Sehemu Tatu
Diski ya DVD yenye kichwa Transfusion Alternatives—Documentary Series, ina sehemu tatu. Sehemu yenye kichwa Transfusion-Alternative Strategies—Simple, Safe, Effective ilirekodiwa kwa ajili ya madaktari na wanafunzi wa tiba, kwa hiyo, ina picha nyingi zinazoonyesha upasuaji na matibabu kuliko zile sehemu nyingine mbili. Sehemu yenye kichwa, Transfusion-Alternative Health Care—Meeting Patient Needs and Rights ilirekodiwa kwa ajili ya waandishi wa habari, maafisa wa tiba, wafanyakazi wa jamii, na mahakimu. Inazungumzia jinsi ya kushughulikia matibabu ya wagonjwa bila kupuuza haki zao za kisheria. Sehemu No Blood—Medicine Meets the Challenge ilirekodiwa kwa ajili ya watu wote. DVD hiyo ni ya Kiingereza, lakini lugha inaweza kubadilishwa hadi Kifaransa, Kihispania, Kiitaliano, Kijapani, Kijerumani, Kireno (cha Brazili), au Kirusi. Jisikie huru kumwonyesha au kumpa DVD hiyo daktari wako, wanafunzi wako wa Biblia, mwenzi wa ndoa, watu wako wa ukoo ambao si Mashahidi, walimu wako, wafanyakazi wenzako, au wanafunzi wenzako.