Ni Matibabu Gani Bora Zaidi?
“Mgonjwa yeyote anayefanyiwa upasuaji bila kutiwa damu, ndiye anayepokea matibabu bora zaidi.” Ndivyo alivyosema Dakt. Michael Rose, msimamizi wa tiba na mtaalamu wa unusukaputi. Ni mbinu gani au ni matibabu gani ya badala yanayoweza kutumiwa katika upasuaji usiohusisha damu? Unahitaji kujua mbinu hizo ili ufanye uamuzi mzuri kuhusu matibabu na upasuaji. Tazama video No Blood—Medicine Meets the Challenge. Baada ya kufanya hivyo, jaribu kuona kama umeelewa kwa kujiuliza maswali yafuatayo.—Taarifa: Kwa kuwa video hiyo ina maonyesho fulani ya upasuaji, wazazi wanapaswa kutumia busara wanapoitazama pamoja na watoto wao.
(1) Ni sababu gani kuu ambayo huwafanya Mashahidi wa Yehova wakatae kutiwa damu mishipani? (2) Kuhusiana na matibabu, Mashahidi wa Yehova hupendekeza wafanyiwe nini? (3) Mgonjwa ana haki gani ya msingi? (4) Kwa nini kuchagua matibabu ya badala yasiyohusisha kutiwa damu mishipani ni jambo la akili? (5) Mtu anapopoteza damu nyingi sana, madaktari wanapaswa kufanya mambo gani mawili haraka? (6) Taja kanuni nne za matibabu ya badala yasiyohusisha damu. (7) Madaktari wanaweza (a) kupunguzaje kupotea kwa damu, (b) kuhifadhi chembe nyekundu za damu jinsi gani, (c) kuharakishaje mwili kutokeza damu, na (d) kuzuiaje damu inayovuja isipotee? (8) Fafanua mbinu zinazojulikana kama (a) uzimuaji wa damu (hemodilution) na (b) uokoaji wa chembe za damu (cell salvage). (9) Ungependa kujulishwa nini kuhusu matibabu ya badala? (10) Je, upasuaji mgumu unaweza kufanywa bila kumtia mgonjwa damu mishipani? (11) Madaktari wameanza kuwa na mtazamo gani mpya?
Baada ya kutazama baadhi ya matibabu yaliyoonyeshwa katika video hii, mtu atajifanyia uamuzi wa kibinafsi kupatana na dhamiri yake mwenyewe iliyozoezwa na Biblia ikiwa anataka kuyakubali. Je, umeamua ni matibabu gani ya badala utakayokubali kwa ajili yako na watoto wako? Washiriki wa familia yako ambao si Mashahidi wanapaswa kujulishwa vilevile kuhusu maamuzi yako na sababu za kufanya maamuzi hayo.—Ona “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” katika Mnara wa Mlinzi la Juni 15, 2004, na la Oktoba 15, 2000.