Nufaika na Video No Blood—Medicine Meets the Challenge
Unajua mengi kadiri gani kuhusu matibabu mbalimbali yasiyohusisha damu? Je, unajua matibabu au dawa zinazoweza kutumiwa badala ya damu na jinsi zinavyofanya kazi? Tazama video hii na utahini ujuzi wako kwa maswali yafuatayo.—Kumbuka: Video hii ina sehemu fupi zinazoonyesha upasuaji, kwa hiyo, wazazi wanapaswa kutumia busara wanapoamua kama watoto wao wadogo wataitazama au la.
(1) Ni kwa sababu gani kuu Mashahidi wa Yehova hukataa kutiwa damu mishipani, na kanuni hiyo inapatikana wapi katika Biblia? (2) Tungependa matibabu ya aina gani? (3) Wagonjwa wana haki gani ya msingi? (4) Kwa nini ni jambo la hekima kukataa kutiwa damu mishipani? (5) Mtu anapopoteza damu nyingi, ni mambo gani mawili ambayo madaktari wanapaswa kufanya haraka? (6) Kuna hatari gani za kiafya zinazohusiana na kutiwa damu mishipani? (7) Taja baadhi ya vifaa ambavyo wapasuaji wanaweza kutumia ili mgonjwa asipoteze damu nyingi wakati wa upasuaji? (8) Ungependa kujua nini kuhusu matibabu au dawa zinazoweza kutumiwa badala ya damu? (9) Je, upasuaji mkubwa na mgumu unaweza kufanywa bila kutumia damu? (10) Madaktari wengi wako tayari kuwafanyia Mashahidi wa Yehova nini, na huenda hatimaye wagonjwa wakatibiwa kwa kutumia njia gani?
Kukubali matibabu yoyote yaliyoonyeshwa katika video hii ni uamuzi wa mtu binafsi unaotegemea dhamiri.—Ona gazeti la Mnara wa Mlinzi la Juni 15, 2004, uku. wa 22-24, 29-31, na Mnara wa Mlinzi la Oktoba 15, 2000, uku. wa 30-31.