The Bible—A Book of Fact and Prophecy
Mankind’s Oldest Modern Book ni sehemu ya kwanza ya DVD yenye sehemu tatu inayoitwa The Bible—A Book of Fact and Prophecy. Baada ya kuitazama sehemu ya kwanza, jibu maswali yafuatayo:
(1) Biblia inapatana na sayansi ya siku hizi kwa njia zipi? (2) Tunawezaje kuwa na hakika kwamba Biblia zinazopatikana leo zina habari zilezile ambazo zilikuwa katika maandishi ya awali? (3) Hati za kale za Biblia ni za pekee kwa njia gani? (4) Watu kama vile John Wycliffe, Johannes Gutenberg, William Tyndale, John Hus, Martin Luther, Casiodoro de Reina, na Charles Taze Russell, walichangiaje usambazaji wa Neno la Mungu duniani kote, na kanisa liliipinga Biblia vikali kwa njia gani? (5) Ushauri wa Biblia umewasaidiaje watu kushughulikia matatizo mbalimbali kama vile zoea sugu la kucheza kamari (1 Tim. 6:9, 10), mume na mke kutengana na uzinzi (1 Kor. 13:4, 5; Efe. 5:28-33), magonjwa (Zab. 34:8), na tamaa ya kuwa na mali nyingi (Mt. 16:26)? (6) Kuna uthibitisho gani wa kwamba kanuni za Maandiko zinaweza kuwasaidia watu waache kuwachukia watu wa taifa, kabila, au jamii nyingine (Luka 10:27)? (7) Wewe umepataje furaha zaidi maishani kwa kufuata kanuni za Biblia? (8) Unawezaje kutumia DVD hii kuwasaidia wengine?—Ona Huduma Yetu ya Ufalme ya Februari 2006, ukurasa wa 8.