Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/12 uku. 7
  • Sarafu Mbili Zenye Thamani Ndogo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sarafu Mbili Zenye Thamani Ndogo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2012
  • Habari Zinazolingana
  • Maisha Katika Nyakati za Biblia—Pesa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Yehova Huwapenda Watoaji Wachangamfu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Mfano wa Kuigwa—Yule Mjane Maskini
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Ametumbukiza Zaidi ya Wote
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2012
km 4/12 uku. 7

Sarafu Mbili Zenye Thamani Ndogo

Njia moja muhimu ya kutegemeza mambo ya Ufalme ni kwa kutoa michango kwa ajili ya kazi ya kuhubiri ya ulimwenguni pote. Namna gani ikiwa hatuna pesa nyingi?

Pindi moja, Yesu alimwona mjane mmoja maskini akitoa mchango wa sarafu mbili zenye thamani ndogo katika sanduku la hazina hekaluni. Upendo kwa Yehova ulimsukuma mjane huyo kutoa “kutokana na uhitaji wake, . . . vyote alivyokuwa navyo, riziki yake yote.” (Marko 12:41-44) Kwa kuwa Yesu alitambua jambo hilo, ni wazi kwamba mchango wa mjane huyo ulikuwa wenye thamani kubwa machoni pa Mungu. Vivyo hivyo, Wakristo wa karne ya kwanza hawakuona daraka la kuitegemeza kifedha huduma kuwa pendeleo la Wakristo matajiri tu. Mtume Paulo alitaja mfano wa ndugu wa Makedonia ambao licha ya ‘umaskini mkubwa, waliendelea kuomba kwa kusihi sana wapate pendeleo la kutoa kwa fadhili.’—2 Kor. 8:1-4.

Hivyo basi, ikiwa tunaweza tu kutoa mchango wa ‘sarafu mbili zenye thamani ndogo,’ tunapaswa kukumbuka kwamba mchango huo mdogo ukijumlishwa na mwingine unaweza kuwa kiasi kikubwa. Tunapotoa kutoka moyoni, tunamfurahisha Baba yetu wa mbinguni aliye mkarimu, kwa kuwa “Mungu humpenda mtoaji mchangamfu.”—2 Kor. 9:7.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki