Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 9/14 uku. 3
  • Tumia Tovuti ya jw.org/sw Katika Huduma

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tumia Tovuti ya jw.org/sw Katika Huduma
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • Habari Zinazolingana
  • Tovuti Yetu Rasmi—Imetengenezwa ili Itunufaishe Sisi na Wengine
    Huduma Yetu ya Ufalme—2012
  • Tumia Tovuti Yetu Katika Huduma—“Majibu ya Maswali ya Biblia”
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • Tutapata Wapi Majibu ya Maswali Muhimu Maishani?
    Tutapata Wapi Majibu ya Maswali Muhimu Maishani?
  • Unaweza Kupata Msaada
    Amkeni!—2020
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2014
km 9/14 uku. 3

Tumia Tovuti ya jw.org/sw Katika Huduma

Tovuti yetu ni njia bora inayotusaidia kueneza habari njema “mpaka sehemu ya mbali zaidi ya dunia.” (Mdo. 1:8) Watu wengi hawaifahamu Tovuti ya jw.org/sw. Wanaijua baada tu ya kupata mwongozo kutoka kwa mhubiri.

Mwangalizi mmoja anayesafiri ameipakua na kuhifadhi kwenye simu yake video yenye kichwa Kwa Nini Ujifunze Biblia?, naye huionyesha kila anapopata fursa. Kwa mfano, anapohubiri nyumba kwa nyumba, yeye husema: “Ninawatembelea watu kwa muda mfupi ili kuwasaidia kupata majibu ya maswali matatu muhimu: Kwa nini ulimwengu una matatizo mengi sana? Mungu atayaondoaje? Na tunawezaje kukabiliana nayo kwa sasa? Video hii fupi inazungumzia maswali hayo.” Kisha, anamwonyesha mwenye nyumba video hiyo na kutazama itikio lake. Video hiyo inawavutia watu sana hivi kwamba wengi wao huitazama kwa makini kutoka mwanzo hadi mwisho. Kisha mwangalizi huyo husema: “Kama ulivyosikia, unaweza kutumia mtandao kuomba kujifunza Biblia. Kwa sababu nipo hapa, ninaweza kutumia muda mfupi kukuonyesha jinsi funzo hilo linavyofanywa.” Mwenye nyumba akikubali, anamwonyesha jinsi ya kujifunza kwa kutumia broshua Habari Njema. Ikiwa mwenye nyumba hana nafasi, anafanya mipango ya kufanya hivyo katika ziara inayofuata. Anapopumzika kwenye mkahawa, anaanzisha mazungumzo ya kirafiki na mtu aliyeketi kando yake halafu anatumia utangulizi kama huo. Je, unatumia Tovuti ya jw.org/sw katika huduma?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki