Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb16 Oktoba uku. 8
  • Je, Unatumia Vizuri Kadi za Mawasiliano za JW.ORG?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Unatumia Vizuri Kadi za Mawasiliano za JW.ORG?
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Habari Zinazolingana
  • Kadi za Mkopo—Je, Zitakutumikia au Zitakutumikisha?
    Amkeni!—1996
  • Je, Napaswa Kuchukua Kadi ya Mkopo?
    Amkeni!—1999
  • “Tupeleke Kadi”
    Amkeni!—1993
  • Tumia Ukurasa wa Mwanzo wa JW.ORG Katika Huduma Yako
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2023
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
mwb16 Oktoba uku. 8

MAISHA YA MKRISTO

Je, Unatumia Vizuri Kadi za Mawasiliano za JW.ORG?

Shahidi wa Yehova akimpa mtu kadi ya mawasiliano ya jw.org

Kwa kuwa dhiki kuu inakaribia, kazi yetu ya kuhubiri inapaswa kufanywa haraka. (Met 24:11, 12, 20) Ili kuwasaidia watu, tunaweza kutumia kadi za mawasiliano kuwaelekeza kwenye Neno la Mungu na tovuti yetu. Kadi hiyo ina alama inayowaelekeza watu kwenye video Kwa Nini Ujifunze Biblia? na mwaliko wa kuomba habari zaidi au funzo la Biblia. Watu fulani hawakubali machapisho lakini wanakubali kutembelea tovuti yetu. Usisite kuwapa kadi ya mawasiliano. Hata hivyo, usiwaachie watu wasiopendezwa kadi ya mawasiliano.

Unapoendelea na shughuli zako za kila siku, unaweza kuchochea upendezi wa mtu kwa kusema: “Ningependa kukupa kadi hii itakayokuelekeza kwenye tovuti iliyo na habari na video kuhusu mambo mbalimbali. Habari zote katika tovuti hiyo zinapatikana bila malipo.” (Yoh 4:7) Kwa kuwa kadi za mawasiliano ni ndogo, unaweza kubeba chache ili uwape watu kila unapopata fursa.

UNAWEZA KUTOA KADI YA MAWASILIANO . . .

  • unapohubiri isivyo rasmi

  • unapohubiri eneo la biashara

  • mtu anaposikiliza ujumbe wetu lakini hakubali machapisho

Kadi ya mawasiliano ya jw.org ikionyesha Biblia iliyofunguliwa
Kadi ya mawasiliano ya jw.org ikionyesha Shahidi wa Yehova akimsomea mtu andiko
Kadi ya mawasiliano ya jw.org ikionyesha Shahidi wa Yehova akiongoza funzo la Biblia pamoja na familia
Upande wa nyuma wa kadi ya mawasiliano ya jw.org

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki