Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 8/8 kur. 26-27
  • “Tupeleke Kadi”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Tupeleke Kadi”
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kutengeneza Kadi Zako Mwenyewe
  • Ujumbe Unaofaa
  • Pindi za Kupeleka Kadi
  • Je, Napaswa Kuchukua Kadi ya Mkopo?
    Amkeni!—1999
  • Je, Unatumia Vizuri Kadi za Mawasiliano za JW.ORG?
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Uandalizi Mpya wa Kutusaidia Kujiepusha na Damu
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 8/8 kur. 26-27

“Tupeleke Kadi”

“HUO ulikuwa mwisho-juma wenye kufurahisha kama nini!” Mkirudi nyumbani baada ya kuwatembelea marafiki wenu, mnakumbuka wakati huo wenye kuburudisha kwa furaha. Jinsi wakaribishaji wenu walivyokuwa wakarimu! Ili kuonyesha uthamini wenu, unaelezea familia yako: “Tupeleke kadi [ya shukrani].”

Basi unaenda madukani kununua kadi. Unapata kadi nyingi sana lakini zenye kukuzubaisha. ‘Nichague kadi gani?’ ‘Ni ipi iliyo na maneno yanayofaa?’ Bila shaka si kazi rahisi kuchagua! Basi mbona usitengeneze kadi yako mwenyewe?

Kutengeneza Kadi Zako Mwenyewe

Kazi hiyo ni rahisi kuliko unavyowazia kwanza. Vitu unavyohitaji tu ni karatasi isiyo na maandishi au kadi nyembamba, kalamu, na bila shaka, ujumbe. Unaweza kuongeza umaridadi wako kwa mapambo unayopenda. Kwa njia gani? Kuna madokezo mawili.

(1) Chagua picha unayopenda. Inaweza kuwa mandhari kutoka kwenye gazeti unayoweza kukata na kushikanisha kwenye kadi yako. Mke mmoja alishtusha mume wake kwa kadi mpya ya kusherehekea mwaka wao wa 25 tangu arusi yao. Alikata picha ndogo mbili za mume wake na yeye mwenyewe na kuzishikanisha katika kadi sahili kuonyesha furaha kwa ajili ya maisha yao waliyoshiriki.

(2) Tumia maua. Tayari yamepambwa vizuri. Baada ya kuyafinya na kuyakausha, uyashikanishe kwa kadi yako ili yaongezee raha na ladha.—Ona sanduku.

Hata uchague umaridadi gani, kwa kweli ni ujumbe ndio wa maana zaidi. Kutengeneza kadi zako mwenyewe kunakupa fursa ya kutunga maneno yanayoonyesha hisia zako kikweli.

Ujumbe Unaofaa

Mfalme Sulemani wa kale ‘alitafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.’ (Mhubiri 12:10) Uchaguzi wa maneno wa namna hiyo utafanya ujumbe wako ulioandikwa uwe “kama machungwa katika vyano vya fedha” kwa mwenye kuupokea.—Mithali 25:11.

Chagua maneno yatakayofurahisha. Unaweza kutia ndani baadhi ya maneno yenye pumzi ya Mungu ili kuwasilisha hisia zako za moyo mweupe. Hayo yatafurahiwa sana.

Jinsi unavyoandika maneno hayo katika kadi inaweza pia kuwasilisha ujumbe fulani. Kuyafanya maandishi yako yawe nadhifu na yenye kusomeka kunaonyesha mambo mengi juu yako, wewe mpelekaji.

Pindi za Kupeleka Kadi

Nyakati za arusi ni vipindi vya furaha ambavyo waume na wake zao wanaweza kualika marafiki na watu wao wa ukoo. Ikiwa watakuwa na mapokezi baadaye, wanaweza kuonyesha kujali hali za wale wanaozuru kutoka mbali kwa kutia katika mwaliko huo wakati yatakapoanza na kumalizika.

Kuzaliwa kwa mtoto kunaweza kuwa pindi nyingine ya kupeleka kadi. Kufanya hivyo kunafanya wazazi wa mtoto huyo wajue kwamba unashiriki furaha yao.

Kwa kuongezea pindi kama hizo, ni jambo linalofaa kama nini kuonyesha shukrani kwa fadhili ambazo watu wamekuonyesha. Unaweza pia kufariji wagonjwa na wale ambao wako hospitalini, ukiwahakikishia upendo wako na hangaiko lako. Salamu zako changamfu na picha inayopendeza ambazo kadi yako inaleta inaweza kusaidia kupunguza mshuko wa moyo na wasiwasi. Kweli, ni kama vile mithali moja ya kale inavyosema, “neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!”—Mithali 15:23.

Unapokuwa mbali sana au hata karibu, wasilisha masikitiko yako kwa wale ambao wamepoteza mpendwa wao katika kifo. Ukumbusho juu ya tumaini zuri ajabu la ufufuo ambalo Biblia hutoa unaweza kufaa.

Basi, wakati wowote unapohisi kuwasilisha hisia zako kwa wengine, mbona usipeleke kadi? Bila shaka, hiyo haichukui mahali pa mazungumzo ya moja kwa moja na mtu huyo ikiwezekana. Badala ya hivyo, ni fursa zaidi ya kuonyesha fadhili.

[Sanduku katika kurasa za 26, 27]

Umaridadi wa Pekee

Kutia umaridadi kwa kutumia maua yaliyofinywa kunaweza kuongeza uzuri wa kadi zako. Hii ni njia sahili na ambayo si ghali ya kutia kadi zako umaridadi wa pekee. Unahitaji vifaa vichache sana.

Kukusanya Maua

◻ Hakikisha kwamba una ruhusa ya kuchuma maua unayotaka.

◻ Epuka kuchuma maua katika mvua.

◻ Usichume maua au matawi mazee.

◻ Usitumie vibaya maua.

Maua mengine hayawezi kufinywa vizuri ikiwa ni manono (njugasamawi, lili, ochidi) au kama yana umbo ambalo ni gumu kulainisha (dafodili, liliki, mawaridi makubwa-makubwa, mibaruti).

Kuyafinya Maua Hayo

◻ Weka maua kati ya karatasi za kukaushia wino ambazo zimefinywa kati ya vipande viwili vya playiwudi. Kuongezea tabaka kadhaa za gazeti kutasaidia kufyonza umajimaji. Kaza vigango hivyo kila siku kadiri maua hayo yanavyokauka.

◻ Ngojea kwa angalau juma moja kabla ya kufungua hivyo vigango.

◻ Tazama kifupi kuona kwamba maua hayo yamefinywa vizuri, na ikihitajika uyaweke tena vizuri katika karatasi kavu.

◻ Funga tena kwa nguvu hivyo vigango, na uviache mahali penye joto la wastani na palipo pakavu kwa angalau majuma mawili au matatu kabla ya kuondoa maua.

Kuyaweka Maua

◻ Tumia gundi kidogo sana.

◻ Tumia maua hayo kwa uangalifu, labda kwa kutumia vibano.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki