Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb17 Februari uku. 8
  • Wasaidie Watoto Wako Wasitawishe Imani Thabiti Katika Muumba

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wasaidie Watoto Wako Wasitawishe Imani Thabiti Katika Muumba
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
  • Habari Zinazolingana
  • Chunguza Uthibitisho
    Amkeni!—2021
  • Msaada Zaidi Kwa Ajili ya Familia
    Amkeni!—2018
  • Unaweza Kupata Msaada
    Amkeni!—2020
  • Walifaulu Kuushinda Ubaguzi
    Amkeni!—2020
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
mwb17 Februari uku. 8

MAISHA YA MKRISTO

Wasaidie Watoto Wako Wasitawishe Imani Thabiti Katika Muumba

Uumbaji unatangaza utukufu wa Yehova. (Zb 19:1-4; 139:14) Hata hivyo, ulimwengu wa Shetani unafundisha nadharia zinazomshushia Mungu heshima kuhusu chanzo cha uhai. (Ro 1:18-25) Unaweza kulindaje akili na mioyo ya watoto wako isiathiriwe na nadharia hizo? Wasaidie tangu utotoni wasitawishe imani kwamba Yehova yupo na anawajali wao kibinafsi. (2Ko 10:4, 5; Efe 6:16) Wasaidie wajieleze kwa uhuru kuhusu mambo wanayofundishwa shuleni, na utumie vifaa vinavyopatikana ili uguse mioyo yao.—Met 20:5; Yak 1:19.

Baba akiwafundisha watoto wake kuhusu uumbaji; mageuzi yakifundishwa darasani; Vijana Wenzako Wanasema Nini—Kumwamini Mungu

TAZAMA VIDEO VIJANA WENZAKO WANASEMA NINI—KUMWAMINI MUNGU, KISHA UCHUNGUZE MASWALI YAFUATAYO:

  • Ni maoni gani yaliyoenea kuhusu imani katika Mungu?

  • Ni nini kinachofundishwa shuleni kwenu?

  • Ni nini kinachokusadikisha kwamba Yehova yupo?

  • Ni nini kinachoweza kukusaidia kumsadikisha mtu kwamba Mungu aliumba vitu vyote?

VIFAA VINGINE VINAVYOPATIKANA:

• Mfululizo kwenye JW.ORG “Masomo Yangu ya Biblia” (Umri usiozidi miaka 3)

• Video Uwe Rafiki ya Yehova—“Yehova . . . Aliumba Vitu Vyote”

• Mfululizo kwenye Amkeni! “Je, Ni Kazi ya Ubuni?”

• Daftari la JW.ORG “Kwa Nini Ninamwamini Mungu?”

• Mfululizo kwenye JW.ORG “Uumbaji au Mageuzi?” (sehemu nne)

• Mfululizo wa video za JW Broadcasting “Maoni Kuhusu Chanzo cha Uhai”

• Video Maajabu ya Uumbaji Yanafunua Utukufu wa Mungu

• Broshua Uhai—Ulitokana na Muumba?

• Kitabu Je, Kuna Muumba Anayekujali?

Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai

Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai

Broshua hii ilitayarishwa hasa kuwasaidia vijana Mashahidi wanaofundishwa kuhusu mageuzi shuleni. Pia watu wanaotaka kupata uthibitisho wenye kina wa kwamba kuna Muumba wanaweza kupewa broshua hii.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki