HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YOHANA 3-4
Yesu Amhubiria Mwanamke Msamaria
Ni nini kilichomwezesha Yesu ahubiri isivyo rasmi?
4:7—Alianzisha mazungumzo kwa kuomba maji badala ya kuzungumzia Ufalme au kujitambulisha kuwa Masihi
4:9—Hakumbagua mwanamke Msamaria kwa sababu hakuwa Myahudi
4:9, 12—Hakukengeushwa kutoka kwenye ujumbe wake hata mwanamke huyo alipozusha mambo ambayo yangeweza kutokeza mabishano.—cf 77 ¶3
4:10—Alianza kwa kutumia mfano uliohusu maisha ya kila siku ya mwanamke huyo
4:16-19—Ingawa aliishi maisha mapotovu kiadili, Yesu alimtendea kwa heshima
Simulizi hili linaonyeshaje umuhimu wa kutoa ushahidi isivyo rasmi?