HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 27-28
Yakobo Apata Baraka Aliyostahili
Isaka alitimiza unabii alipombariki Yakobo.
27:28—Yehova aliwapa wazao wa Yakobo nchi yenye rutuba “inayotiririka maziwa na asali.”—Kum 26:15
27:29—Waisraeli (wazao wa Yakobo) wakawa wenye nguvu zaidi ya Waedomu (wazao wa Esau).—Mwa 25:23; 2Sa 8:14
27:29—Kwa chuki waliokuwa nayo kuelekea Waisraeli, Waedomu walilaaniwa na hatimaye taifa hilo likaangamizwa.—Eze 25:12-14