Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 9/98 uku. 1
  • Twaweza Kufanya Kazi Kubwa Zaidi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Twaweza Kufanya Kazi Kubwa Zaidi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1998
  • Habari Zinazolingana
  • ‘Kufanya Kazi Kwa Bidii na Kujikaza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • “Nifuateni, Nami Nitawafanya Kuwa Wavuvi Watu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • “Nendeni Mkafanye Wanafunzi”
    ‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
  • “Nendeni Mkafanye Wanafunzi Kutoka kwa Watu wa Mataifa Yote”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1998
km 9/98 uku. 1

Twaweza Kufanya Kazi Kubwa Zaidi

1 Kazi zenye kutokeza zilifanyiza huduma ya Yesu Kristo. Alifanya miujiza kwa kulisha maelfu ya watu, kuponya wengi, na kufufua wengine kutoka katika wafu. (Mt. 8:1-17; 14:14-21; Yn. 11:38-44) Utendaji wake ulinasa uangalifu wa taifa zima. Hata hivyo, jioni ya mwisho kabla ya kifo chake, aliwaambia wafuasi wake waaminifu hivi: “Yeye ambaye hudhihirisha imani katika mimi, huyo pia atafanya kazi ambazo mimi hufanya; naye atafanya kazi kubwa zaidi ya hizi.” (Yn. 14:12) Twaweza kufanyaje kazi “kubwa zaidi”?

2 Kwa Kuhubiri Eneo Kubwa Zaidi: Yesu alihubiri Palestina tu, ilhali wanafunzi wake wa mapema waliambiwa watoe ushahidi “hadi sehemu ya mbali zaidi sana ya dunia,” mbali zaidi kuliko alikohubiri Yesu. (Mdo. 1:8) Kazi ya kuhubiri aliyoanzisha duniani sasa imefika tufeni pote, katika nchi 232. (Mt. 24:14) Je, wewe washiriki kikamili kuhubiri eneo ambalo kutaniko lenu limegawiwa?

3 Kwa Kufikia Watu Wengi Zaidi: Yesu aliacha wanafunzi wachache kwa kadiri ili waendeleze kazi ya kuhubiri. Hata hivyo, kwa sababu ya kuhubiri kwao kwa bidii, kwenye Pentekoste 33 W.K., wale waliokubali kweli na kubatizwa siku hiyo walikuwa jumla ipatayo nafsi elfu tatu. (Mdo. 2:1-11, 37-41) Kukusanywa kwa ‘walio na mwelekeo ufaao kwa ajili ya uhai udumuo milele’ kumeendelea hadi wakati wetu, tunapobatiza wastani wa watu 1,000 kwa siku. (Mdo. 13:48) Je, wewe wafanya yote uwezayo ili uweze kufikia watu wenye mioyo ya haki popote wawezapo kupatikana na kufuata kupendezwa kulikoonyeshwa mara iwezekanapo?

4 Kwa Kuhubiri kwa Muda Mrefu Zaidi: Huduma ya Yesu ya kidunia ilikuwa ya miaka mitatu na nusu tu. Wengi wetu tumekuwa tukihubiri kwa muda mrefu zaidi ya huo. Bila kujali muda tutakaoruhusiwa tuendelee katika kazi hii, twashukuru kumsaidia kila mwanafunzi mpya apate njia iongozayo kwenye uhai. (Mt. 7:14) Je, una mengi ya kufanya kila mwezi katika kazi ya Bwana?—1 Kor. 15:58.

5 Twaweza kudumu tukiwa na uhakika kwamba kwa utegemezo wa Yesu, bado tutafanya kazi kubwa zaidi tukiwa wanafunzi wake wa kweli.—Mt. 28:19, 20.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki