Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w11 5/1 uku. 7
  • Unabii wa 4. Watu Hawatakuwa na Upendo wa Asili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unabii wa 4. Watu Hawatakuwa na Upendo wa Asili
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Msaada kwa Wanaotendewa kwa Jeuri Nyumbani
    Habari Zaidi
  • Kwa Nini Wanaume Huwapiga Wanawake?
    Amkeni!—2001
  • Jeuri Iathiripo Nyumbani
    Amkeni!—1993
  • Ni Nini Husababisha Jeuri ya Nyumbani?
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
w11 5/1 uku. 7

Unabii wa 4. Watu Hawatakuwa na Upendo wa Asili

“Watu watakuwa . . . wasiowapenda wa kwao.”—2 TIMOTHEO 3:1-3, Union Version.

● Chris anafanya kazi na kikundi cha kuwasaidia watu wanaokabili jeuri nyumbani, huko Wales Kaskazini. “Ninakumbuka mwanamke mmoja ambaye alikuwa amepigwa vibaya sana hivi kwamba nisingeweza kumtambua ingawa nilikuwa nimemwona hapo awali,” anasema Chris. “Wanawake wengine huathiriwa sana kihisia kiasi kwamba hawawezi kuinua macho yao kukutazama.”

MAMBO YA HAKIKA YANAONYESHA NINI? Katika nchi moja barani Afrika, inakadiriwa kwamba mwanamke 1 kati ya kila wanawake 3 alilalwa kinguvu akiwa mtoto. Uchunguzi uliofanywa katika nchi hiyo ulionyesha kwamba zaidi ya asilimia 33 ya wanaume wanaona kwamba ni sawa kuwapiga wake zao. Hata hivyo, si wanawake tu wanaokabili jeuri nyumbani. Kwa mfano, nchini Kanada, karibu wanaume 3 kati ya kila wanaume 10 wamepigwa au kutendewa vibaya na wanawake wanaoishi nao.

NI KIPINGAMIZI GANI KINACHOTOLEWA MARA NYINGI? Jeuri inayotokea nyumbani si jambo jipya, imekuwako sikuzote. Lakini wakati huu inatangazwa zaidi kuliko hapo zamani.

JE, KIPINGAMIZI HICHO KINA MSINGI? Katika miaka ya hivi karibuni, jeuri inayotokea nyumbani imetangazwa sana. Lakini je, jambo hilo limefanya visa vya jeuri inayotokea nyumbani vipungue? Hapana. Watu wasio na upendo wa asili wanazidi kuongezeka.

UNA MAONI GANI? Je, andiko la 2 Timotheo 3:1-3 linatimia? Je, watu wengi wanakosa upendo kwa familia zao, sifa ambayo kiasili wanapaswa kuwa nayo?

Unabii wa tano unaotimia sasa unahusu dunia, makao yetu. Ona yale ambayo Biblia inasema kuhusu jambo hilo.

[Blabu katika ukurasa wa 7]

“Jeuri inayotokea nyumbani ni mojawapo ya mambo yanaripotiwa mara chache sana katika jamii. Mwanamke atashambuliwa mara 35 hivi na mwanamume anayeishi naye kabla ya kuripoti jambo hilo kwa polisi.”​—MSEMAJI WA KITUO CHA KUWASAIDIA WATU WANAOTENDEWA JEURI NYUMBANI NCHINI WALES.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki