Watchtower—MAKTABA KU ENTERNETE
Watchtower
MAKTABA KU ENTERNETE
Kiswahili (Congo)
  • BIBLIA
  • VICHAPO
  • MIKUTANO
  • km 10/00 uku. 3-6
  • Programu ya shule ya huduma ya Kitheokrasi ya 2001

Hakuna video juu ya habari yenye umechagua.

Pole, kulikuwa kosa fulani wakati video ilikuwa inajaribu kusoma.

  • Programu ya shule ya huduma ya Kitheokrasi ya 2001
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2000
  • Vichwa Vidogo
  • Maagizo
  • PROGRAMU
Huduma Yetu ya Ufalme—2000
km 10/00 uku. 3-6

Programu ya shule ya huduma ya Kitheokrasi ya 2001

Maagizo

Mnamo 2001, Shule ya Huduma ya Kitheokrasi itaendeshwa kulingana na mipango ifuatayo.

VICHAPO: Migawo itatoka katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo [bi7-SW], Mnara wa Mlinzi [w-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], na Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko [rs-SW]

Shule ingepaswa kuanza PA WAKATI kwa wimbo, sala, na maneno mafupi ya ukaribishaji. Hakuna uhitaji wa kuonyesha kimbele yale yaliyo kwenye programu. Kadiri mwangalizi wa shule anavyotoa utangulizi wa kila sehemu, yeye atataja kichwa cha habari kitakachozungumziwa. Fuata utaratibu ufuatao:

MGAWO Na. 1: dakika 15. Huu ungepaswa kutolewa na mzee au mtumishi wa huduma, na habari yake itatokana na Mnara wa Mlinzi au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Wakati unapotokana na Mnara wa Mlinzi, mgawo huu unapaswa kutolewa kama hotuba ya maagizo ya dakika 15 bila kujikumbusha kwa mdomo; wakati unapotokana na kitabu “Kila Andiko,” huo unapaswa kutolewa kama hotuba ya dakika 10 hadi 12, ikifuatwa na kujikumbusha kwa mdomo kwa dakika 3 hadi 5 kwa kutumia maulizo yaliyochapwa katika kichapo. Lengo halipaswi kuwa tu kuzungumzia habari lakini kukaza uangalifu juu ya matumizi yenye kufaa ya habari inayozungumziwa, ikikazia lile litakalokuwa lenye kusaidia zaidi kutaniko. Kichwa kinachoonyeshwa kinapaswa kutumiwa.

Ndugu wanaogawiwa hotuba hii wanapaswa kuwa waangalifu ili kuheshimu wakati unaotolewa. Shauri la faraghani linaweza kutolewa ikiwa hilo linahitajiwa au ikiwa linaombwa na msemaji.

MAMBO MAKUU KUTOKA USOMAJI WA BIBLIA: dakika 6. Mgawo huu ungepaswa kutolewa na mzee au mtumishi wa huduma ambaye, kwa matokeo, atatumia habari kulingana na mahitaji ya kutaniko. Hakuna kichwa cha habari kinachohitajiwa. Huo haupaswi kuwa tu kifupi cha usomaji uliotolewa kuwa mgawo. Kusema kwa kifupi muda wa sekunde 30 hadi 60 mambo yote yaliyo katika sura zilizotolewa kuwa mgawo kunaweza kutiwa ndani. Hata hivyo, lengo kubwa ni kusaidia wasikilizaji waelewe kwa nini na namna gani habari hiyo ilivyo ya thamani kwetu. Kisha, mwangalizi wa shule ataambia wanafunzi waende katika madarasa yao mbalimbali.

MGAWO Na. 2: dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia wa habari iliyotolewa kuwa mgawo; itatolewa na ndugu, iwe kwamba mwanafunzi yuko katika shule ya kwanza au katika shule ya pili. Mara nyingi, migawo ya usomaji ni mifupi vya kutosha ili kuruhusu wanafunzi watoe habari fupi ya maelezo katika maneno ya utangulizi na ile ya umalizio. Hali ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho, na matumizi ya kanuni yanaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyotolewa kuwa mgawo inapaswa kusomwa bila kukatizwa. Bila shaka, mistari ya kusoma inapokuwa haifuatani, mwanafunzi anaweza kutaja mstari ambako usomaji unaendelea.

MGAWO Na. 3: dakika 5. Dada atagawiwa sehemu hii. Habari kwa ajili ya utoaji huu itatokana na kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko. Kikao kinaweza kuwa mahubiri ya vivi-hivi, ziara ya kurudia, au funzo la Biblia la nyumbani, nao wale wanaoshiriki wanaweza kukaa au kubaki wima. Mwangalizi wa shule atapendezwa hasa na jinsi mwanafunzi anavyozungumzia kichwa kilichotolewa kuwa mgawo na jinsi anavyosaidia mwenye nyumba afikiri juu ya maandiko. Mwanafunzi anayegawiwa sehemu hii anapaswa kujua kusoma. Mwangalizi wa shule atapanga kuwe msaidizi mmoja, lakini msaidizi wa ziada anaweza kutumiwa. Matumizi yenye matokeo ya Biblia yangepaswa kufikiriwa kwanza, si kikao.

MGAWO Na. 4: dakika 5. Habari kwa ajili ya mgawo huu itatokana na kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko. Ndugu au dada anaweza kupewa Mgawo Na. 4. Wakati ndugu ndiye anayegawiwa mgawo huo, unapaswa sikuzote kuwa hotuba. Wakati dada ndiye anayeugawiwa, huo unapaswa kutolewa kama inavyoonyeshwa kuhusu Mgawo Na. 3.

PROGRAMU YA USOMAJI WA BIBLIA: Kila mmoja katika kutaniko anatiwa moyo afuate programu ya kila juma ya usomaji wa Biblia, ambayo ni sawa na kusoma karibu ukurasa mmoja kila siku.

TAARIFA: Ili kupata habari ya ziada na maagizo kuhusu shauri, kuheshimu wakati, kujikumbusha kwa kuandika, na kutayarisha migawo, tafadhali ona ukurasa 3 wa Huduma Yetu ya Ufalme ya Novemba 1996.

PROGRAMU

Jan. 1 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 13-16

Wimbo Na. 62

Na. 1: Kitendo Kimoja cha Kusamehe Chafungua Njia kwa Ajili ya Wokovu (w99-SW 1/1 kur. 30-1)

Na. 2: 2 Wafalme 14:1-14

Na. 3: Utoaji-Mimba—Kwa Nini Unakatazwa? (rs-SW kur. 395-6 fu. 5)

Na. 4: Jinsi ya Kujibu Mtu Anayesema: ‘Nina Haki ya Kuamua Mambo Yanayohusu Mwili Wangu Mwenyewe’ (rs-SW uku. 396 fu. 6)

Jan. 8 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 17-20

Wimbo Na. 116

Na. 1: Shauri Lililo Rahisi Zaidi Kukubali (w99-SW 1/15 kur. 21-4)

Na. 2: 2 Wafalme 18:1-16

Na. 3: Adamu na Eva—Watu Halisi wa Kihistoria?

(rs-SW kur. 25-6 fu. 5)

Na. 4: Jinsi ya Kujibu Mtu Anayesema: ‘Dhambi ya Adamu Ilikuwa Mapenzi ya Yehova Mungu, Mpango wa Mungu’ (rs-SW uku. 27 maf. 1-2)

Jan. 15 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 21-25

Wimbo Na. 61

Na. 1: 2 Wafalme—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 74 maf. 33-6)

Na. 2: 2 Wafalme 21:1-16

Na. 3: Kwa Nini Kuabudu Wazazi wa Kale Waliokufa Ni Jambo la Bure? (rs-SW kur. 110-1 fu. 10)

Na. 4: Kwa Nini Kuabudu Wazazi wa Kale Waliokufa Kunamchukiza Yehova Mungu (rs-SW uku. 112 maf. 1-6)

Jan. 22 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 1-5

Wimbo Na. 16

Na. 1: 1 Mambo ya Nyakati—Utangulizi (si-SW kur. 75-6 maf. 1-7)

Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 1:1-27

Na. 3: Wapinga Kristo Ni Nani? (rs-SW kur. 212-3)

Na. 4: Jinsi ya Kutambua Waasi-Imani (rs-SW kur. 317-9 fu. 4)

Jan. 29 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 6-10

Wimbo Na. 73

Na. 1: Jinsi Unyenyekevu wa Kweli Unavyoweza Kuonyeshwa (w99-SW 2/1 kur. 6-7)

Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 9:1-21

Na. 3: Ni Nini Unapaswa Kuwa Mtazamo Wetu Kuelekea Waasi-Imani? (rs-SW uku. 320 maf. 1-7)

Na. 4: Kristo Hakujenga Kanisa juu ya Petro (rs-SW kur. 224-6 fu. 4)

Feb. 5 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 11-16

Wimbo Na. 65

Na. 1: Iweni Chanzo cha Kitia-Moyo (w99-SW 2/15 kur. 26-9)

Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 11:1-19

Na. 3: Funguo Ambazo Petro Alitumia Zilikuwa Nini?

(rs-SW uku. 226 fu. 5–uku. 229 fu. 3)

Na. 4: ‘Wale Waliochukua Nafasi ya Mitume’ Si Wakristo wa Kweli

(rs-SW uku. 229 fu. 4–uku. 231 fu. 7)

Feb. 12 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 17-23

Wimbo Na. 122

Na. 1: Jifungeni Hali ya Akili ya Kujishusha Chini

(w99-SW 3/1 kur. 30-1)

Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 18:1-17

Na. 3: Har–Magedoni Itapiganwa Wapi? (rs-SW kur. 86-8 fu. 7)

Na. 4: Ni Nani na Ni Nini Kitakachoharibiwa Kwenye Har–Magedoni? (rs-SW uku. 88 fu. 8–uku. 89 fu. 5)

Feb. 19 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 24-29

Wimbo Na. 119

Na. 1: 1 Mambo ya Nyakati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 78-9 maf. 22-5)

Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 29:1-13

Na. 3: Ni Nani Watakaookoka Har–Magedoni? (rs-SW uku. 89 fu. 6—uku. 90 fu. 3)

Na. 4: Har–Magedoni—Upendo wa Mungu Hautavunjwa

(rs-SW uku. 90 maf. 4-6)

Feb. 26 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 1-5

Wimbo Na. 168

Na. 1: 2 Mambo ya Nyakati—Utangulizi (si-SW kur. 79-80 maf. 1-6)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 1:1-17

Na. 3: Haitawezekana Kuchukua Msimamo wa Kutokuwamo Kwenye Har–Magedoni (rs-SW uku. 91 maf. 1-4)

Na. 4: Ni Uvutano wa Nani Unaosukuma Mataifa Kuelekea Har–Magedoni? (rs-SW uku. 91 maf. 5-6)

Machi 5 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 6-9

Wimbo Na. 103

Na. 1: Usishindwe na Hangaiko (w99-SW 3/15 kur. 21-3)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 8:1-16

Na. 3: Jinsi ya Kutambua Yule Babuloni wa Ufunuo (rs-SW uku. 35 maf. 1-2)

Na. 4: Ni Nini Lilifanya Babuloni wa Kale Ujulikane?

(rs-SW uku. 36 fu. 1–uku. 37 fu. 5)

Machi 12 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 10-15

Wimbo Na. 59

Na. 1: Ni Nani Ambaye Huongoza Kufikiri Kwako? (w99-SW 4/1 kur. 20-2)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 10:1-16

Na. 3: Kwa Nini Dini Zinazodai Kuwa za Kikristo Ni Sehemu ya Babuloni Mkubwa (rs-SW uku. 38 fu. 1–uku. 39 fu. 1)

Na. 4: Kwa Nini Ni Jambo la Haraka Kutoka Katika Babuloni Mkuu

(rs-SW uku. 39 maf. 2-7)

Machi 19 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 16-20

Wimbo Na. 69

Na. 1: Linda Moyo Wako Dhidi ya Ibada ya Baali (w99-SW 4/1 kur. 28-31)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 16:1-14

Na. 3: Ubatizo Ni Nini, na kwa Nini Waamini Hubatizwa

(rs-SW uku. 321 maf. 1-4)

Na. 4: Ubatizo wa Kikristo—Si kwa Kunyunyiza Maji, Si kwa Ajili ya Vitoto Vichanga (rs-SW uku. 321 fu. 5–uku. 322 fu. 5)

Machi 26 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 21-25

Wimbo Na. 212

Na. 1: Usijizuie Kuonyesha Shukrani (w99-SW 4/15 kur. 15-17)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 22:1-12

Na. 3: Ubatizo wa Maji Hausamehe Dhambi

(rs-SW uku. 322 fu. 6–uku. 323 fu. 2)

Na. 4: Ni Nani Wanaobatizwa kwa Roho Takatifu?

(rs-SW uku. 323 fu. 3–uku. 324 fu. 4)

Apr. 2 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 26-29

Wimbo Na. 49

Na. 1: Je, Mungu Hufanya Mambo kwa Njia ‘Zilizopotoka’? (w99-SW 5/1 kur. 28-9)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 28:1-15

Na. 3: Ubatizo wa Moto Ni Tofauti na Ubatizo kwa Roho Takatifu

(rs-SW uku. 324 fu. 5–uku. 325 fu. 3)

Na. 4: Sababu za Kutufanya Tuichunguze Biblia (rs-SW kur. 40-1 fu. 5)

Apr. 9 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 30-33

Wimbo Na. 1

Na. 1: Wanadamu Wanawezaje Kumbariki Yehova? (w99-SW 5/15 kur. 21-4)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 33:1-13

Na. 3: Uhakikisho Kutoka kwa Isaya na Yeremia Kwamba Biblia Iliongozwa na Mungu (rs-SW uku. 42 fu. 1–uku. 43 fu. 1)

Na. 4: Utimizo wa Unabii Unahakikisha Kwamba Biblia Iliongozwa na Mungu (rs-SW uku. 43 maf. 2-3)

Apr. 16 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 34-36

Wimbo Na. 144

Na. 1: 2 Mambo ya Nyakati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 84 maf. 34-6)

Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 36:1-16

Na. 3: Biblia Ni ya Kweli Kisayansi (rs-SW uku. 44 fu. 1–​uku. 45 fu. 1)

Na. 4:  aJinsi ya Kujibu Vipingamizi Kuhusu Biblia

(rs-SW uku. 46 fu. 2–uku. 49 fu. 4)

Apr. 23 Usomaji wa Biblia: Ezra 1-6

Wimbo Na. 90

Na. 1: Ezra—Utangulizi na kwa Nini Ni Chenye Mafaa

(si-SW kur. 85-6 maf. 1-7; uku. 87 maf. 14-18)

Na. 2: Ezra 4:1-16

Na. 3: Kwa Nini Wakristo Hawaadhimishi Ukumbusho wa Siku ya Kuzaliwa? (rs-SW kur. 356-8 fu. 2)

Na. 4: Kwa Nini Wakristo Hujiepusha na Damu? (rs-SW kur. 50-2 fu. 1)

Apr. 30 Kujikumbusha kwa Kuandika. Usomaji wa Biblia: Ezra 7-10

Wimbo Na. 203

Mei 7 Usomaji wa Biblia: Nehemia 1-5

Wimbo Na. 56

Na. 1: Nehemia—Utangulizi (si-SW uku. 88 maf. 1-5)

Na. 2: Nehemia 1:1-11

Na. 3: Kwa Nini Wakristo Hawakubali Kutiwa Damu Mishipani?

(rs-SW uku. 52 fu. 2–uku. 53 fu. 2)

Na. 4:  bJinsi ya Kujibu Maneno Kuhusu Kutiwa Damu Mishipani

(rs-SW uku. 54 fu. 1–uku. 56 fu. 1)

Mei 14 Usomaji wa Biblia: Nehemia 6-9

Wimbo Na. 155

Na. 1: Kutaniko la Kikristo Ni Chanzo cha Msaada Wenye Kutia Nguvu (w99-SW 5/15 kur. 25-8)

Na. 2: Nehemia 9:1-15

Na. 3: Inamaanisha Nini Kuzaliwa Mara ya Pili? (rs-SW kur. 150-1 fu. 6)

Na. 4: Wokovu Hautegemei “Kuzaliwa Mara ya Pili”

(rs-SW uku. 151 fu. 7–uku. 153 fu. 1)

Mei 21 Usomaji wa Biblia: Nehemia 10-13

Wimbo Na. 46

Na. 1: Nehemia—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 90-1 maf. 16-19)

Na. 2: Nehemia 12:27-43

Na. 3:  cJinsi ya Kujibu Maoni Mbalimbali Kuhusu Kuzaliwa Mara ya Pili (rs-SW uku. 153 fu. 3–uku. 154 fu. 1)

Na. 4: Kuungamia Mapadri—Kwa Nini Si Jambo la Kimaandiko?

(rs-SW kur. 365-6 fu. 3)

Mei 28 Usomaji wa Biblia: Esta 1-4

Wimbo Na. 38

Na. 1: Esta—Utangulizi (si-SW kur. 91-2 maf. 1-6)

Na. 2: Esta 1:1-15

Na. 3: Kuungama Dhambi Dhidi ya Mungu na Mwanadamu

(rs-SW uku. 367 fu. 4–uku. 368 fu. 3)

Na. 4: Kwa Nini Dhambi Zito Zinapaswa Kuungamwa kwa Wazee?

(rs-SW uku. 368 maf. 4-8)

Juni 4 Usomaji wa Biblia: Esta 5-10

Wimbo Na. 37

Na. 1: Esta—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 94 maf. 16-18)

Na. 2: Esta 5:1-14

Na. 3: Kwa Nini Ni Jambo la Akili Kuamini Uumbaji?

(rs-SW kur. 397-9 fu. 1)

Na. 4: Kuelewa Lile Simulizi la Biblia la Uumbaji

(rs-SW uku. 399 fu. 2–uku. 401 fu. 2)

Juni 11 Usomaji wa Biblia: Yobu 1-7

Wimbo Na. 84

Na. 1: Ayubu—Utangulizi (si-SW kur. 95-6 maf. 1-6)

Na. 2: Yobu 1:6-22

Na. 3: Kwa Nini Kuheshimu Msalaba Si Jambo la Kimaandiko?

(rs-SW kur. 217 maf. 1-7)

Na. 4: Kwa Nini Wanadamu Wanakufa? (rs-SW kur. 100-101 fu. 5)

Juni 18 Usomaji wa Biblia: Yobu 8-14

Wimbo Na. 192

Na. 1: Sauli—Chombo-Kichaguliwa kwa Bwana (w99-SW 5/15 kur. 29-31)

Na. 2: Yobu 8:1-22

Na. 3: Wafu Wako Wapi, na Hali Yao Ni Gani?

(rs-SW uku. 101 fu. 6–uku. 103 fu. 3)

Na. 4: Kwa Nini Mashahidi wa Yehova Hawashiriki Desturi za Kimapokeo za Kuomboleza Wafu? (rs-SW uku. 104 fu. 1–uku. 105 fu. 1)

Juni 25 Usomaji wa Biblia: Yobu 15-21

Wimbo Na. 81

Na. 1: Mungu Si wa Polepole kwa Habari ya Ahadi Yake (w99-SW 6/1 kur. 4-7)

Na. 2: Yobu 17:1-16

Na. 3:  dJinsi ya Kujibu Maoni Yasiyo ya Kweli Kuhusu Kifo

(rs-SW uku. 105 maf. 2-4)

Na. 4: Ndoto: Ni Zenye Kuongozwa na Mungu au Si Zenye Kuongozwa na Mungu (rs-SW kur. 247-8 fu. 5)

Julai 2 Usomaji wa Biblia: Yobu 22-29

Wimbo Na. 173

Na. 1: Je, Yakupasa Kupanua Maoni Yako? (w99-SW 6/15 kur. 10-13)

Na. 2: Yobu 27:1-23

Na. 3: Dawa za Kulevya—Wakati Ambapo Zinakatazwa kwa Wakristo (rs-SW kur. 56-8 fu. 2)

Na. 4: Kwa Nini Wakristo Wanaepuka Marijuana

(rs-SW uku. 58 fu. 3–uku. 59 fu. 2)

Julai 9 Usomaji wa Biblia: Yobu 30-35

Wimbo Na. 108

Na. 1: Sababu kwa Nini Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia (w99-SW 7/15 kur. 4-8)

Na. 2: Yobu 31:1-22

Na. 3: Kwa Nini Wakristo Wanaepuka Tumbaku?

(rs-SW uku. 60 fu. 1–uku. 61 fu. 4)

Na. 4: Kushinda Mazoea Mabaya—Namna Gani? (rs-SW uku. 62 maf. 1-4)

Julai 16 Usomaji wa Biblia: Yobu 36-42

Wimbo Na. 160

Na. 1: Ayubu—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 100 maf. 39-43)

Na. 2: Yobu 36:1-22

Na. 3: Mataifa Hayatazuia Kusudi la Mungu Kuelekea Dunia (rs-SW kur. 78-9 fu. 3)

Na. 4: Je, Mungu Ataiharibu Dunia kwa Moto?

(rs-SW uku. 79 fu. 4–uku. 81 fu. 1)

Julai 23 Usomaji wa Biblia: Zaburi 1-10

Wimbo Na. 5

Na. 1: Zaburi—Utangulizi (Sehemu 1) (si-SW uku. 101 maf. 1-5)

Na. 2: Zaburi 3:1–4:8

Na. 3: Washiriki wa Yerusalemu Mpya Hawatarudi Duniani Baada ya Waovu Kuharibiwa (rs-SW uku. 81 maf. 2-3)

Na. 4: Je, Kusudi la Kwanza la Mungu kwa Dunia Limebadilika?

(rs-SW uku. 82 fu. 1–uku. 83 fu. 1)

Julai 30 Usomaji wa Biblia: Zaburi 11-18

Wimbo Na. 48

Na. 1: Zaburi—Utangulizi (Sehemu 2) (si-SW uku. 102 maf. 6-11)

Na. 2: Zaburi 11:1–13:6

Na. 3: Tunawezaje Kutia Moyo Wagonjwa? (rs-SW kur. 106-7 fu. 2)

Na. 4: Tunawezaje Kutia Moyo Wale Waliofiwa? (rs-SW uku. 107 maf. 3-7)

Agosti 6 Usomaji wa Biblia: Zaburi 19-26

Wimbo Na. 117

Na. 1: Mawasiliano (Upashanaji-Habari) Yenye Kujenga—Ufunguo wa Kuwa na Ndoa Nzuri (w99-SW 7/15 kur. 21-3)

Na. 2: Zaburi 20:1–21:13

Na. 3: Kitia-Moyo kwa Wale Wanaonyanyaswa kwa Sababu ya Kufanya Mapenzi ya Mungu (rs-SW uku. 107 fu. 8–uku. 108 fu. 5)

Na. 4: Unawezaje Kutia Moyo Wale Wanaovunjika Moyo kwa Sababu ya Ukosefu wa Haki? (rs-SW uku. 108 fu. 6–uku. 109 fu. 2)

Agosti 13 Usomaji wa Biblia: Zaburi 27-34

Wimbo Na. 130

Na. 1: Filipo—Mweneza-Evanjeli Mwenye Bidii (w99-SW 7/15 kur. 24-5)

Na. 2: Zaburi 28:1–29:11

Na. 3: Kuna Kitia-Moyo Gani kwa Wale Wanaokazwa Sana na Matatizo ya Kiuchumi? (rs-SW uku. 109 maf. 3-7)

Na. 4: Kitia-Moyo kwa Wale Wanaovunjwa Moyo na Makosa (rs-SW uku. 109 fu. 8–uku. 110 fu. 3)

Agosti 20 Usomaji wa Biblia: Zaburi 35-39

Wimbo Na. 18

Na. 1: Mkazo Kutoka kwa Wenzako—Je, Waweza Kuwa kwa Faida Yako? (w99-SW 8/1 kur. 22-5)

Na. 2: Zaburi 38:1-22

Na. 3: Mageuzi—Tatanisho la Kisayansi (rs-SW kur. 159-60 fu. 3)

Na. 4: Mageuzi, Mabaki ya Wanyama na Mimea ya Zamani Yanayogunduliwa Katika Miamba, na Kufikiri Kuzuri (rs-SW uku. 160 fu. 4–uku. 163 fu. 6)

Agosti 27 Kujikumbusha kwa Kuandika. Usomaji wa Biblia: Zaburi 40-47

Wimbo Na. 91

Sept. 3 Usomaji wa Biblia: Zaburi 48-55

Wimbo Na. 36

Na. 1: Zuia Hasira Isikukwaze (w99-SW 8/15 kur. 8-9)

Na. 2: Zaburi 49:1-20

Na. 3:  eJinsi ya Kujibu Maneno ya Wanamageuzi (rs-SW uku. 164 fu. 1–uku. 166 fu. 2)

Na. 4: Kwa Nini Watu Wengi Wanakosa Imani? (rs-SW kur. 91-2 fu. 5)

Sept. 10 Usomaji wa Biblia: Zaburi 56-65

Wimbo Na. 44

Na. 1: Je, Ibilisi Hutufanya Tuwe Wagonjwa? (w99-SW 9/1 kur. 4-7)

Na. 2: Zaburi 59:1-17

Na. 3: Mtu Anawezaje Kupata Imani? (rs-SW uku. 93 maf. 1-4)

Na. 4: Imani Katika Tazamio la Mfumo Mpya wa Mambo Inahakikishwa na Matendo (rs-SW uku. 93 fu. 6–uku. 94 fu. 4)

Sept. 17 Usomaji wa Biblia: Zaburi 66-71

Wimbo Na. 210

Na. 1: Chagua “Fungu Jema” (w99-SW 9/1 kur. 30-1)

Na. 2: Zaburi 69:1-19

Na. 3: Manabii wa Uwongo Wanaweza Kutambuliwaje?

(rs-SW kur. 166-8 fu. 2)

Na. 4: Manabii wa Kweli Hawakuelewa Sikuzote Wakati na Jinsi Mambo Yaliyotabiriwa Yangetukia

(rs-SW uku. 168 maf. 3-8)

Sept. 24 Usomaji wa Biblia: Zaburi 72-77

Wimbo Na. 217

Na. 1: Kwa Nini Utimize Ahadi Zako? (w99-SW 9/15 kur. 8-11)

Na. 2: Zaburi 73:1-24

Na. 3: Matamko ya Nabii wa Kweli Yanaendeleza Ibada ya Kweli (rs-SW uku. 169 maf. 1-2)

Na. 4: Manabii wa Kweli Wanatambuliwa kwa Matunda Wanayotokeza (rs-SW uku. 169 fu. 3–uku. 171 fu. 1)

Okt. 1 Usomaji wa Biblia: Zaburi 78-81

Wimbo Na. 88

Na. 1: Pata Hekima na Ukubali Nidhamu (Kutiwa Adabu) (w99-SW 9/15 kur. 12-15)

Na. 2: Zaburi 78:1-22

Na. 3: Jinsi ya Kujibu Wale Wanaotuita Manabii wa Uwongo

(rs-SW uku. 171 maf. 2-4)

Na. 4: Mungu Haamui Kimbele Wakati Ambapo Kila Mtu Atakapokufa (rs-SW uku. 27 fu. 3—uku. 28 fu. 2)

Okt. 8 Usomaji wa Biblia: Zaburi 82-89

Wimbo Na. 221

Na. 1: Timotheo—“Mtoto Halisi Katika Imani”

(w99-SW 9/15 kur. 29-31)

Na. 2: Zaburi 88:1-18

Na. 3: Kila Jambo Linalotukia Si Mapenzi ya Mungu

(rs-SW uku. 28 fu. 3–uku. 29 fu. 7)

Na. 4: Mungu Hajui Kimbele na Haweki Kimbele Kila Jambo

(rs-SW uku. 30 maf. 1-3)

Okt. 15 Usomaji wa Biblia: Zaburi 90-98

Wimbo Na. 134

Na. 1: Tumeimarishwa Kukataa Kutenda Kosa (w99-SW 10/1 kur. 28-31)

Na. 2: Zaburi 90:1-17

Na. 3: Uwezo wa Mungu wa Kujua Kimbele na Kuweka Kimbele Matukio (rs-SW uku. 30 fu. 4—uku. 31 fu. 3)

Na. 4: Kwa Nini Mungu Hakutumia Ujuzi Wake wa Kimbele Kuhusu Adamu (rs-SW uku. 31 fu. 4—uku. 32 fu. 1)

Okt. 22 Usomaji wa Biblia: Zaburi 99-105

Wimbo Na. 89

Na. 1: Kujifunza Njia Ipitayo Zote ya Upendo (w99-SW 10/15 kur. 8-11)

Na. 2: Zaburi 103:1-22

Na. 3: Mungu Hakuamua Kimbele Mambo Ambayo Yangewapata Yakobo, Esau au Yuda (rs-SW uku. 32 fu. 2–uku. 33 fu. 1)

Na. 4: Ni Katika Njia Gani Mambo ya Kutaniko la Kikristo Yaliamuliwa Kimbele? (rs-SW kur. 33 maf. 2-3)

Okt. 29 Usomaji wa Biblia: Zaburi 106-109

Wimbo Na. 214

Na. 1: “Bwana Huwapa Watu Hekima” (w99-SW 11/15 kur. 24-7)

Na. 2: Zaburi 107:1-19

Na. 3: Ni Nini Maoni ya Kimaandiko Kuhusu Unajimu (Elimu ya Nyota)? (rs-SW uku. 34 maf. 1-5)

Na. 4: Ni Nini Sababu Fulani za Akili za Kuamini Kwamba Kuna Mungu? (rs-SW kur. 218-9 fu. 3)

Nov. 5 Usomaji wa Biblia: Zaburi 110-118

Wimbo Na. 14

Na. 1: Apokalipsi—Je, Tuiogope au Tuitumainie?

(w99-SW 12/1 kur. 5-8)

Na. 2: Zaburi 112:1–113:9

Na. 3: Uovu na Kuteseka Havihakikishi Kwamba Hakuna Mungu (rs-SW uku. 219 maf. 4-6)

Na. 4: Mungu Ni Mtu Halisi Anayeweza Kuwa na Hisia

(rs-SW uku. 220 maf. 1-7)

Nov. 12 Usomaji wa Biblia: Zaburi 119

Wimbo Na. 35

Na. 1: Usiache Uwezo Wako Uwe Udhaifu Wako

(w99-SW 12/1 kur. 26-9)

Na. 2: Zaburi 119:1-24

Na. 3: Mungu Hakuwa na Mwanzo (rs-SW uku. 220 fu. 8—uku. 221 fu. 3)

Na. 4: Kutumia Jina la Mungu Ni kwa Lazima ili Kupata Wokovu

(rs-SW uku. 222 maf. 1-4)

Nov. 19 Usomaji wa Biblia: Zaburi 120-137

Wimbo Na. 175

Na. 1: Zaburi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (Sehemu 1) (si-SW kur. 104-5 maf. 23-7)

Na. 2: Zaburi 120:1–122:9

Na. 3: Je, Dini Zote Ni Nzuri? (rs-SW uku. 222 maf. 5-8)

Na. 4: Yesu Ni “Mungu” wa Aina Gani? (rs-SW uku. 222 maf. 9-10)

Nov. 26 Usomaji wa Biblia: Zaburi 138-150

Wimbo Na. 135

Na. 1: Zaburi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (Sehemu 2) (si-SW kur. 105-6 maf. 28-32)

Na. 2: Zaburi 139:1-24

Na. 3:  fJinsi ya Kujibu Vipingamizi Kuhusu Kuamini Kwamba Kuna Mungu (rs-SW uku. 223 fu. 1–uku. 224 fu. 2)

Na. 4: Kwa Nini Wanadamu Hawakuweza Kusimamisha Serikali Yenye Haki (rs-SW kur. 279-80 fu. 6)

Des. 3 Usomaji wa Biblia: Mezali 1-7

Wimbo Na. 132

Na. 1: Mithali—Utangulizi (Sehemu 1) (si-SW kur. 106-7 maf. 1-5)

Na. 2: Mezali 4:1-27

Na. 3: Kwa Nini Jitihada za Wanadamu za Kuleta Kitulizo Haziwezi Kufanikiwa (rs-SW uku. 281 maf. 1-6)

Na. 4: Ufalme wa Mungu Tu Ndio Utatosheleza Mahitaji ya Kweli ya Wanadamu (rs-SW uku. 282 maf. 1-5)

Des. 10 Usomaji wa Biblia: Mezali 8-13

Wimbo Na. 51

Na. 1: Mithali—Utangulizi (Sehemu 2) (si-SW kur. 107-8 maf. 6-11)

Na. 2: Mezali 13:1-25

Na. 3: Unabii wa Biblia Umeonekana Kuwa Wenye Kutegemeka Kabisa (rs-SW uku. 283 maf. 1-4)

Na. 4: Kuponya Kimuujiza Leo Hakufanywi na Roho ya Mungu

(rs-SW kur. 122-3 fu. 3)

Des. 17 Usomaji wa Biblia: Mezali 14-19

Wimbo Na. 111

Na. 1: Mithali—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (Sehemu 1)

(si-SW kur. 109-10 maf. 19-28)

Na. 2: Mezali 16:1-25

Na. 3: Tofauti Kati ya Maponyo Yaliyofanywa na Yesu na Mitume Wake na Yale Yanayofanywa Leo (rs-SW uku. 123 fu. 4–uku. 124 fu. 2)

Na. 4: Jinsi Wakristo wa Kweli Wanavyotambuliwa Leo (rs-SW uku. 124 fu. 3–uku. 125 fu. 1)

Des. 24 Usomaji wa Biblia: Mezali 20-25

Wimbo Na. 9

Na. 1: Mithali—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (Sehemu 2)

(si-SW kur. 110-11 maf. 29-38)

Na. 2: Mezali 20:1-30

Na. 3: Kwa Nini Zawadi za Kuponya Zilitolewa Katika Karne ya Kwanza (rs-SW uku. 125 fu. 2–uku. 126 fu. 2)

Na. 4: Kuna Tumaini Gani la Kuponywa Kwelikweli kwa Wanadamu Wote? (rs-SW uku. 126 maf. 3-5)

Des. 31 Kujikumbusha kwa Kuandika. Usomaji wa Biblia: Mezali 26-31

Wimbo Na. 180

[Maelezo ya Chini]

a Ikiwa wakati unaruhusu, chunguzeni jinsi ya kujibu maneno, vipingamizi, na kadhalika vitakavyopatana vizuri zaidi na mahitaji ya eneo.

b Ikiwa wakati unaruhusu, chunguzeni jinsi ya kujibu maneno, vipingamizi, na kadhalika vitakavyopatana vizuri zaidi na mahitaji ya eneo.

c Ikiwa wakati unaruhusu, chunguzeni jinsi ya kujibu maneno, vipingamizi, na kadhalika vitakavyopatana vizuri zaidi na mahitaji ya eneo.

d Ikiwa wakati unaruhusu, chunguzeni jinsi ya kujibu maneno, vipingamizi, na kadhalika vitakavyopatana vizuri zaidi na mahitaji ya eneo.

e Ikiwa wakati unaruhusu, chunguzeni jinsi ya kujibu maneno, vipingamizi, na kadhalika vitakavyopatana vizuri zaidi na mahitaji ya eneo.

f Ikiwa wakati unaruhusu, chunguzeni jinsi ya kujibu maneno, vipingamizi, na kadhalika vitakavyopatana vizuri zaidi na mahitaji ya eneo.

    Vichapo vya Swahili (Congo) (1996-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili (Congo)
    • Tumia Wengine
    • Préférences
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Kanuni za Matumizi
    • Kanuni za Kutunza Siri
    • Paramètres Kuhusu Kutunza Siri
    • JW.ORG
    • Ingia
    Tumia Wengine