Tito
3 Endelea kuwakumbusha wawe katika ujitiisho na wawe watiifu kwa serikali na mamlaka zikiwa watawala, wawe tayari kwa ajili ya kila kazi njema, 2 wasiseme kwa ubaya juu ya yeyote, wasiwe wataka-vita, wawe wenye kukubali sababu, wakionyesha wazi upole wote kuelekea watu wote. 3 Kwa maana hata sisi wakati mmoja tulikuwa wenye kukosa akili, wasiotii, tukiongozwa vibaya, tukiwa watumwa wa tamaa na raha za namna mbalimbali, tukiendelea katika ubaya na husuda, wenye kukirihisha, tukichukiana.
4 Hata hivyo, wakati fadhili na upendo kwa ajili ya binadamu kwa upande wa Mwokozi wetu, Mungu, vilipodhihirishwa, 5 si kwa sababu ya kazi za kuwa katika uadilifu ambazo sisi tulikuwa tumefanya, bali kulingana na rehema yake alituokoa kupitia mwosho uliotuleta kwenye uhai na kupitia kutufanya sisi wapya kwa roho takatifu. 6 Roho hii yeye aliimwaga kwa wingi juu yetu kupitia Yesu Kristo Mwokozi wetu, 7 ili, baada ya kutangazwa kuwa waadilifu kwa msingi wa fadhili isiyostahiliwa ya huyo, sisi tupate kuwa warithi kulingana na tumaini la uhai udumuo milele.
8 Wa uaminifu ni huu usemi, na kuhusu mambo haya natamani wewe usisitize imara daima, ili wale ambao wameamini Mungu wapate kuweka akili zao juu ya kudumisha kazi zilizo bora. Mambo haya ni bora na yenye manufaa kwa watu.
9 Lakini epuka kabisa maswali-maswali ya upumbavu na nasaba na zogo na mapigano juu ya Sheria, kwa maana hayo hayana faida na ni yenye ubatili. 10 Kwa habari ya mtu akuzaye farakano, mkatae baada ya onyo la upole la kwanza na la pili; 11 ukijua kwamba mtu wa namna hiyo amegeuzwa kutoka njiani na anafanya dhambi, yeye akiwa amejihukumia hatia mwenyewe.
12 Wakati nitumapo Artemasi au Tikiko kwako, fanya yote kabisa uwezayo uje kwangu katika Nikopolisi, kwa maana huko ndiko nimeamua kuwa wakati wa majira ya baridi kali. 13 Kwa uangalifu gawa mahitaji kwa Zenasi, aliye na ujuzi mwingi katika Sheria, na Apolo kwa ajili ya safari yao, ili wasikose kitu chochote. 14 Lakini acha watu wetu pia wajifunze kudumisha kazi zilizo bora ili kutimiza mahitaji yao muhimu, ili wasiwe wasiozaa matunda.
15 Wale wote walio pamoja nami wakupelekea wewe salamu zao. Wape salamu zangu wale walio na shauku nasi katika imani.
Fadhili isiyostahiliwa na iwe pamoja na nyinyi watu wote.