43 Msifanye nafsi zenu ziwe zenye kuchukiza kutokana na kiumbe chochote kinachozaana kwa wingi ambacho kinajaa, wala msijifanye kuwa wasio safi kutokana nao na kupata kuwa wasio safi kutokana nao.+
25 Nanyi mtatofautisha mnyama aliye safi na asiye safi na kutofautisha ndege aliye safi na asiye safi;+ nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa zenye kuchukiza+ kupitia mnyama na ndege na kitu chochote ambacho hutembea juu ya nchi ambacho nimekitenga kwa ajili yenu kwa kuvitangaza kuwa si safi.
14 Nami nikasema: “Ole wangu, Ee Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova! Tazama! Nafsi yangu haijatiwa unajisi;+ Sijala mnyama ambaye tayari amekufa wala mnyama aliyeraruliwa tangu ujana wangu,+ mpaka sasa, na nyama chafu haijaingia kinywani mwangu.”+