4 “‘Ila hiki ndicho ambacho hamtakula kati ya wacheuaji na wenye ukwato uliopasuka: ngamia, kwa sababu ni mcheuaji lakini hana ukwato uliopasuka. Huyo si safi kwenu.+
25 Nanyi mtatofautisha mnyama aliye safi na asiye safi na kutofautisha ndege aliye safi na asiye safi;+ nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa zenye kuchukiza+ kupitia mnyama na ndege na kitu chochote ambacho hutembea juu ya nchi ambacho nimekitenga kwa ajili yenu kwa kuvitangaza kuwa si safi.
14 Nami nikasema: “Ole wangu, Ee Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova! Tazama! Nafsi yangu haijatiwa unajisi;+ Sijala mnyama ambaye tayari amekufa wala mnyama aliyeraruliwa tangu ujana wangu,+ mpaka sasa, na nyama chafu haijaingia kinywani mwangu.”+