31 “Nami nitauweka mpaka wako kutoka Bahari Nyekundu hadi bahari ya Wafilisti na kutoka nyikani hadi kwenye Mto;+ kwa sababu nitawaweka wakaaji wa nchi hiyo mikononi mwenu, na hakika wewe utawafukuzia mbali kutoka mbele yako.+
24 Kila mahali ambapo wayo wa mguu wenu utakanyaga patakuwa penu.+ Mpaka wenu utakuwa kutoka nyikani hadi Lebanoni, kutoka ule Mto, mto Efrati, hadi bahari ya magharibi.+
21 Naye Sulemani alikuwa mtawala juu ya falme zote kutoka ule Mto+ hadi kwenye nchi ya Wafilisti na hadi kwenye mpaka wa Misri. Walikuwa wakileta zawadi na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.+