31 “Nami nitauweka mpaka wako kutoka Bahari Nyekundu hadi bahari ya Wafilisti na kutoka nyikani hadi kwenye Mto;+ kwa sababu nitawaweka wakaaji wa nchi hiyo mikononi mwenu, na hakika wewe utawafukuzia mbali kutoka mbele yako.+
24 Kila mahali ambapo wayo wa mguu wenu utakanyaga patakuwa penu.+ Mpaka wenu utakuwa kutoka nyikani hadi Lebanoni, kutoka ule Mto, mto Efrati, hadi bahari ya magharibi.+
16 Wasiria walipoona kwamba wameshindwa+ mbele ya Israeli, wakatuma wajumbe na kuwatoa Wasiria waliokuwa katika eneo la ule Mto,+ na Shofaki mkuu wa jeshi la Hadadezeri akiwa mbele yao.