-
2 Mambo ya Nyakati 32:15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Na sasa msiache Hezekia awadanganye+ wala kuwashawishi+ ninyi hivyo wala msimwamini, kwa maana hakuna mungu yeyote wa taifa lolote au ufalme aliyeweza kuwakomboa watu wake kutoka mkononi mwangu na kutoka mkononi mwa mababu zangu. Basi, Mungu wenu atawezaje kuwakomboa ninyi kutoka mkononi mwangu!’”+
-
-
Danieli 3:15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Basi sasa ikiwa mko tayari ili mnaposikia sauti ya baragumu, zumari, zeze, kinubi chenye pembe tatu, kinanda, zumari-tete na aina zote za vyombo vya muziki,+ mwanguke chini na kuiabudu sanamu ambayo nimeitengeneza, ni vema. Lakini msipoabudu, mtatupwa wakati huohuo ndani ya tanuru inayowaka moto. Na ni mungu gani huyo anayeweza kuwaokoa ninyi kutoka mikononi mwangu?”+
-