-
Mathayo 13:14, 15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
14 Na unabii wa Isaya unatimia kwao unaosema: ‘Kwa kweli mtasikia lakini hamtaelewa, nanyi kwa kweli mtatazama lakini hamtaona.+ 15 Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa migumu, nao wamesikia kwa masikio yao bila kuitikia, nao wamefunga macho yao, ili wasione kamwe kwa macho yao na kusikia kwa masikio yao na kuelewa kwa mioyo yao, kisha wageuke nami niwaponye.’+
-
-
Matendo 28:25-27Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Basi kwa sababu hawakukubaliana miongoni mwao, wakaanza kuondoka, naye Paulo akasema jambo hili moja:
“Kwa kufaa roho takatifu ilisema kupitia Isaya nabii kwa mababu zenu, 26 ikisema, ‘Nenda kwa watu hawa uwaambie: “Kwa kweli mtasikia lakini hamtaelewa kamwe, na kwa kweli mtatazama, lakini hamtaona kamwe.+ 27 Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa migumu, nao wamesikia kwa masikio yao bila kuitikia, nao wamefunga macho yao, ili wasione kamwe kwa macho yao na kusikia kwa masikio yao na kuelewa kwa mioyo yao, nao wageuke nami niwaponye.”’+
-