-
Marko 7:32-35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
32 Basi wakamletea mtu aliye kiziwi na mwenye tatizo la kuzungumza,+ nao wakamsihi aweke mkono juu yake. 33 Kisha akampeleka faraghani, mbali na umati. Halafu akamtia vidole masikioni, baada ya kutema mate, akamgusa ulimi.+ 34 Yesu akatazama mbinguni, akavuta pumzi kwa nguvu na kumwambia: “Efatha,” yaani, “Funguka.” 35 Ndipo masikio yake yakafunguliwa,+ na tatizo lake la kuzungumza likaisha, naye akaanza kuzungumza vizuri.
-