-
Yeremia 44:12-14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Nami nitawachukua watu wa Yuda waliobaki walioazimia kwenda nchini Misri kukaa huko, na wote wataangamia nchini Misri.+ Watauawa kwa upanga na kuangamia kwa njaa kali; kuanzia mdogo zaidi mpaka mkubwa zaidi, watakufa kwa upanga na kwa njaa kali. Nao watakuwa laana, kitu cha kutisha, matusi, na shutuma.+ 13 Nitawaadhibu wale wanaoishi nchini Misri kama nilivyoliadhibu Yerusalemu, kwa upanga, kwa njaa kali, na kwa ugonjwa hatari.+ 14 Na watu wa Yuda waliobaki ambao wameenda kukaa nchini Misri hawataponyoka wala kuokoka na kurudi kwenye nchi ya Yuda. Watatamani kurudi na kukaa huko, lakini hawatarudi, isipokuwa wachache watakaoponyoka.’”
-
-
Yeremia 44:27, 28Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
27 Sasa ninawatazama ili kuwaletea msiba bali si mema;+ watu wote wa Yuda walio nchini Misri wataangamia kwa upanga na kwa njaa kali, mpaka watakapokwisha kabisa.+ 28 Ni wachache tu watakaoponyoka upanga nchini Misri na kurudi katika nchi ya Yuda.+ Kisha watu wote wa Yuda waliobaki ambao walienda kukaa nchini Misri watajua ni neno la nani lililotimia, langu au lao!”’”
-