Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo ya Walawi 26:29
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 29 Basi mtalazimika kula nyama ya wana wenu na nyama ya mabinti wenu.+

  • Kumbukumbu la Torati 28:53-57
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 53 Ndipo mtakapolazimika kuwala watoto wenu* wenyewe, nyama ya wana wenu na mabinti wenu+ ambao Yehova Mungu wenu amewapa, kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu.

      54 “Hata mwanamume mpole sana na aliyedekezwa miongoni mwenu hatamhurumia ndugu yake au mke wake mpendwa au wanawe wanaobaki, 55 naye hatawagawia hata kidogo nyama ya wanawe ambayo atakula, kwa sababu hana kitu kingine chochote cha kula kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu katika majiji yenu.+ 56 Na mwanamke mpole sana na aliyedekezwa miongoni mwenu ambaye hata hawezi kuthubutu kukanyaga chini kwa wayo wa mguu wake kwa sababu ya kudekezwa sana+ hatamhurumia mume wake mpendwa wala mwanawe wala binti yake, 57 wala hata kondo la nyuma linalotoka katikati ya miguu yake wala wana anaozaa, kwa sababu atawala kwa siri kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu katika majiji yenu.

  • Yeremia 19:9
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Nami nitawafanya wale nyama ya wana wao na ya mabinti wao, nao watakula kila mmoja nyama ya mwenzake, kwa sababu ya kuzingirwa na kukata tamaa watakapobanwa na maadui wao wanaotaka kuwaua.”’*+

  • Maombolezo 4:10
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 10 Mikono ya wanawake wenye huruma imewachemsha watoto wao wenyewe.+

      Wamekuwa chakula chao cha maombolezo wakati wa kuangamia kwa binti ya watu wangu.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki