-
Mathayo 20:17-19Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
17 Alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu, Yesu akawaita faraghani wale wanafunzi 12 na kuwaambia wakiwa barabarani:+ 18 “Tazama! Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa binadamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi. Nao watamhukumia kifo+ 19 na kumtia mikononi mwa watu wa mataifa ili wamdhihaki, wampige mijeledi, na kumuua kwenye mti;+ na siku ya tatu atafufuliwa.”+
-
-
Marko 10:32-34Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
32 Sasa walikuwa barabarani wakipanda kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa akiwatangulia, nao walikuwa wameshangaa, lakini wale waliofuata wakaanza kuogopa. Akawapeleka kando tena wale 12 na kuanza kuwaambia mambo yaliyokuwa karibu kumpata:+ 33 “Tazama! Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa binadamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi. Nao watamhukumia kifo na kumtia mikononi mwa watu wa mataifa, 34 nao watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua, lakini baada ya siku tatu atafufuka.”+
-