Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 13
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Sauli achagua jeshi (1-4)

      • Sauli atenda kwa kimbelembele (5-9)

      • Samweli amkaripia Sauli (10-14)

      • Waisraeli hawakuwa na silaha (15-23)

1 Samweli 13:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Hati ya Kiebrania haionyeshi idadi ya miaka yake.

Marejeo

  • +Mdo 13:21

1 Samweli 13:2

Marejeo

  • +1Sa 18:1; 2Sa 1:4; 21:7
  • +Yos 18:28; 1Sa 10:26

1 Samweli 13:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “tarumbeta.”

Marejeo

  • +Yos 13:2, 3; 1Sa 9:16
  • +Yos 21:8, 17
  • +Amu 3:26, 27; 6:34; 2Sa 2:28

1 Samweli 13:4

Marejeo

  • +Yos 5:9; 1Sa 11:14

1 Samweli 13:5

Marejeo

  • +Kum 20:1
  • +Yos 7:2; 18:11, 12; 1Sa 14:23

1 Samweli 13:6

Marejeo

  • +1Sa 14:11

1 Samweli 13:7

Marejeo

  • +Hes 32:1, 33; Yos 13:24, 25

1 Samweli 13:9

Marejeo

  • +1Sa 15:22, 23

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    1/2017, uku. 17

1 Samweli 13:11

Marejeo

  • +1Sa 13:6, 8
  • +1Sa 13:5

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    8/1/2000, kur. 12-13

  • Fahirishi ya Machapisho

    w00 8/1 12-13

1 Samweli 13:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “sijautuliza uso wa.”

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    8/1/2000, kur. 12-13

  • Fahirishi ya Machapisho

    w00 8/1 12-13

1 Samweli 13:13

Marejeo

  • +1Sa 15:11

1 Samweli 13:14

Marejeo

  • +1Sa 15:28
  • +1Sa 16:1; 2Sa 7:15; Zb 78:70; Mdo 13:22
  • +Mwa 49:10; 2Sa 5:2; 7:8; 1Nya 28:4
  • +Met 11:2

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    9/1/2011, kur. 26-29

    1/1/1989, uku. 23

    “Kila Andiko,” uku. 63

  • Fahirishi ya Machapisho

    w11 9/1 26-29

1 Samweli 13:15

Marejeo

  • +1Sa 13:7; 14:2

1 Samweli 13:16

Marejeo

  • +1Sa 13:3
  • +1Sa 13:2

1 Samweli 13:18

Marejeo

  • +Yos 10:11

1 Samweli 13:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Kipimo cha zamani ambacho ni karibu theluthi mbili za shekeli.

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ibada Safi, uku. 75

    Tafsiri ya Ulimwengu Mpya, uku. 2028

    The Watchtower,

    3/15/2005, uku. 29

  • Fahirishi ya Machapisho

    w05 3/15 29

1 Samweli 13:22

Marejeo

  • +1Sa 17:47, 50

1 Samweli 13:23

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kituo cha ulinzi cha.”

Marejeo

  • +1Sa 13:2; 14:4, 5

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

1 Sam. 13:1Mdo 13:21
1 Sam. 13:21Sa 18:1; 2Sa 1:4; 21:7
1 Sam. 13:2Yos 18:28; 1Sa 10:26
1 Sam. 13:3Yos 13:2, 3; 1Sa 9:16
1 Sam. 13:3Yos 21:8, 17
1 Sam. 13:3Amu 3:26, 27; 6:34; 2Sa 2:28
1 Sam. 13:4Yos 5:9; 1Sa 11:14
1 Sam. 13:5Kum 20:1
1 Sam. 13:5Yos 7:2; 18:11, 12; 1Sa 14:23
1 Sam. 13:61Sa 14:11
1 Sam. 13:7Hes 32:1, 33; Yos 13:24, 25
1 Sam. 13:91Sa 15:22, 23
1 Sam. 13:111Sa 13:6, 8
1 Sam. 13:111Sa 13:5
1 Sam. 13:131Sa 15:11
1 Sam. 13:141Sa 15:28
1 Sam. 13:141Sa 16:1; 2Sa 7:15; Zb 78:70; Mdo 13:22
1 Sam. 13:14Mwa 49:10; 2Sa 5:2; 7:8; 1Nya 28:4
1 Sam. 13:14Met 11:2
1 Sam. 13:151Sa 13:7; 14:2
1 Sam. 13:161Sa 13:3
1 Sam. 13:161Sa 13:2
1 Sam. 13:18Yos 10:11
1 Sam. 13:221Sa 17:47, 50
1 Sam. 13:231Sa 13:2; 14:4, 5
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
1 Samweli 13:1-23

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

13 Sauli alikuwa na umri wa miaka . . .* alipowekwa kuwa mfalme,+ na kwa miaka miwili alitawala Israeli. 2 Sauli alichagua wanaume 3,000 katika Israeli; 2,000 kati yao walikuwa pamoja na Sauli kule Mikmashi na katika eneo lenye milima la Betheli, na 1,000 walikuwa pamoja na Yonathani+ katika jiji la Gibea+ la Benjamini. Aliwaruhusu waliobaki waende zao, kila mmoja kwenye hema lake. 3 Kisha Yonathani akaishambulia kambi ya kijeshi ya Wafilisti+ iliyokuwa Geba,+ na Wafilisti wakasikia habari hizo. Basi Sauli akaagiza pembe* ipigwe+ nchini kote, akisema: “Waebrania na wasikie!” 4 Waisraeli wote wakasikia habari hizi: “Sauli ameishambulia kambi ya kijeshi ya Wafilisti, na sasa Waisraeli wananuka mbele ya Wafilisti.” Basi watu wakakusanywa ili wamfuate Sauli huko Gilgali.+

5 Wafilisti pia wakakusanyika pamoja ili wapigane na Waisraeli, nao walikuwa na magari 30,000 ya vita na wapanda farasi 6,000 na wanajeshi wengi kama chembe za mchanga kwenye ufuo wa bahari;+ nao wakapanda na kupiga kambi kule Mikmashi upande wa mashariki wa Beth-aveni.+ 6 Na wanaume wa Israeli wakaona kwamba walikuwa hatarini, kwa sababu watu walikuwa chini ya mkazo mkali; basi watu wakajificha ndani ya mapango,+ mashimo, miamba, mahandaki, na hifadhi za maji. 7 Hata baadhi ya Waebrania walivuka Yordani na kuingia nchi ya Gadi na Gileadi.+ Lakini Sauli alikuwa bado Gilgali, na watu wote waliomfuata walikuwa wakitetemeka. 8 Aliendelea kungoja kwa siku saba mpaka wakati uliowekwa na Samweli ulipofika, lakini Samweli hakuja Gilgali, na watu walikuwa wakitawanyika kutoka kwake. 9 Mwishowe Sauli akasema: “Nileteeni dhabihu ya kuteketezwa na dhabihu za ushirika.” Basi akaitoa dhabihu ya kuteketezwa.+

10 Lakini mara tu alipomaliza kutoa dhabihu ya kuteketezwa, Samweli akafika. Kwa hiyo Sauli akaenda kumpokea na kumbariki. 11 Kisha Samweli akamuuliza: “Umefanya nini?” Sauli akamjibu: “Niliona kwamba watu wanatawanyika kutoka kwangu,+ nawe hukuja kwa wakati uliowekwa, na Wafilisti walikuwa wakikusanyika huko Mikmashi.+ 12 Kwa hiyo nikajiambia, ‘Sasa Wafilisti watashuka kunishambulia Gilgali, nami sijatafuta kibali cha* Yehova.’ Kwa hiyo nikahisi kwamba nina wajibu wa kutoa dhabihu ya kuteketezwa.”

13 Ndipo Samweli akamwambia Sauli: “Umetenda kipumbavu. Hukutii amri ambayo Yehova Mungu wako alikupa.+ Kama ungetii, Yehova angeimarisha ufalme wako juu ya Waisraeli milele. 14 Lakini sasa ufalme wako hautadumu.+ Yehova atamtafuta mtu anayeupendeza moyo wake,+ na Yehova atamweka kuwa kiongozi juu ya watu wake,+ kwa sababu hukutii mambo uliyoamriwa na Yehova.”+

15 Kisha Samweli akainuka na kupanda kwenda zake kutoka Gilgali mpaka jiji la Gibea la Benjamini, naye Sauli akawahesabu watu; wale waliobaki naye walikuwa wanaume wapatao 600.+ 16 Sauli na Yonathani mwana wake pamoja na watu waliobaki pamoja nao walikuwa wakikaa katika jiji la Geba+ la Benjamini, nao Wafilisti walikuwa wamepiga kambi kule Mikmashi.+ 17 Na makundi ya wavamizi yalikuwa yakitoka katika kambi ya Wafilisti katika vikosi vitatu. Kikosi kimoja kilikuwa kikielekea kwenye barabara inayoenda Ofra, katika nchi ya Shuali; 18 kikosi kingine kilikuwa kikielekea kwenye barabara ya Beth-horoni;+ na kikosi cha tatu kilikuwa kikifuata barabara inayoelekea kwenye mpaka ulio ng’ambo ya bonde la Seboimu, kuelekea nyikani.

19 Basi hakukuwa na fundi yeyote wa chuma katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walikuwa wamesema: “Ili Waebrania wasitengeneze upanga wala mkuki.” 20 Na Waisraeli wote walilazimika kushuka kwenda kwa Wafilisti ili majembe yao ya plau, sururu, mashoka, au miundu yao inolewe. 21 Bei ya kunoa ilikuwa pimu moja* kwa majembe ya plau, kwa sururu, kwa vifaa vyenye meno matatu, kwa mashoka, na pia kwa ajili ya kurekebisha mchokoo wa ng’ombe. 22 Na siku ya vita, hakuna yeyote kati ya watu waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani aliyekuwa na upanga wala mkuki mkononi mwake;+ Sauli na Yonathani mwanawe ndio tu waliokuwa na silaha.

23 Basi kikosi cha wanajeshi* Wafilisti kilikuwa kimeenda kwenye kivuko kilicho kwenye njia inayoenda Mikmashi.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki