Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo ya Walawi 12
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Mambo ya Walawi—Yaliyomo

      • Kutakaswa kwa mwanamke baada ya kuzaa mtoto (1-8)

Mambo ya Walawi 12:2

Marejeo

  • +Law 15:19

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2012, uku. 17

    5/15/2004, uku. 23

  • Fahirishi ya Machapisho

    w12 1/15 17; w04 5/15 23

Mambo ya Walawi 12:3

Marejeo

  • +Mwa 17:12; 21:4; Lu 1:59; 2:21, 22; Yoh 7:22

Mambo ya Walawi 12:5

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2004, uku. 23

  • Fahirishi ya Machapisho

    w04 5/15 23

Mambo ya Walawi 12:6

Marejeo

  • +Law 1:10

Mambo ya Walawi 12:8

Marejeo

  • +Law 1:14; 5:7; 14:21, 22; Lu 2:24

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    5/15/2004, uku. 23

  • Fahirishi ya Machapisho

    w04 5/15 23

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Law. 12:2Law 15:19
Law. 12:3Mwa 17:12; 21:4; Lu 1:59; 2:21, 22; Yoh 7:22
Law. 12:6Law 1:10
Law. 12:8Law 1:14; 5:7; 14:21, 22; Lu 2:24
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Mambo ya Walawi 12:1-8

Mambo ya Walawi

12 Yehova akaendelea kumwambia Musa: 2 “Waambie Waisraeli, ‘Mwanamke akipata mimba na kuzaa mtoto wa kiume, mwanamke huyo hatakuwa safi kwa siku saba, atakuwa kama anavyokuwa katika siku zake za hedhi.+ 3 Siku ya nane, mtoto huyo atatahiriwa.+ 4 Kisha kwa siku 33 mwanamke huyo ataendelea kujitakasa kwa sababu ya damu aliyopoteza. Asiguse kitu chochote kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu mpaka atakapokamilisha siku zake za kujitakasa.

5 “Akizaa mtoto wa kike, mwanamke huyo hatakuwa safi kwa siku 14, atakuwa kama anavyokuwa katika siku zake za hedhi. Kisha ataendelea kujitakasa kwa siku 66 kwa sababu ya damu aliyopoteza. 6 Siku zake za kujitakasa zitakapokwisha baada ya kuzaa mtoto wa kiume au wa kike, atamletea kuhani mwanakondoo dume wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu ya kuteketezwa+ na hua mchanga au njiwa tetere kwa ajili ya dhabihu ya dhambi kwenye mlango wa hema la mkutano. 7 Kuhani atatoa dhabihu hizo mbele za Yehova ili kufunika dhambi ya mwanamke huyo, kisha atakuwa safi kutokana na damu yake. Hiyo ndiyo sheria kuhusu mwanamke anayezaa mtoto wa kiume au wa kike. 8 Lakini ikiwa hawezi kuleta kondoo, basi anapaswa kuleta njiwa tetere wawili au hua wawili wachanga,+ mmoja kwa ajili ya dhabihu ya kuteketezwa na wa pili kwa ajili ya dhabihu ya dhambi, naye kuhani atamtolea dhabihu hizo ili kufunika dhambi yake, kisha atakuwa safi.’”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki