Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Wakorintho 13
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

2 Wakorintho—Yaliyomo

      • Maonyo ya mwisho na himizo (1-14)

        • “Endeleeni kujijaribu kama mko katika imani” (5)

        • Mrekebishwe upya; mfikiri kwa upatano (11)

2 Wakorintho 13:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kinywa cha.”

Marejeo

  • +Kum 19:15; Mt 18:16

2 Wakorintho 13:4

Marejeo

  • +Ro 6:4; 1Pe 3:18
  • +2Ti 2:11, 12
  • +1Ko 6:14

2 Wakorintho 13:5

Marejeo

  • +1Ko 11:28; Gal 6:4

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    3/2024, kur. 12-13

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    1/2023, uku. 10

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    1/2018, uku. 13

    Mnara wa Mlinzi,

    7/15/2014, uku. 11

    3/15/2014, uku. 13

    7/15/2008, uku. 28

    7/15/2005, kur. 21-25

    2/15/2005, uku. 13

    9/15/2002, uku. 18

    4/15/1999, kur. 19-20

    1/15/1998, kur. 14-15

  • Fahirishi ya Machapisho

    w08 7/15 28; w05 2/15 13; w05 7/15 21-25; w02 9/15 18; w99 4/15 19-20; w98 1/15 14-15

2 Wakorintho 13:7

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/15/1990, kur. 21-22

2 Wakorintho 13:8

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    6/1/1997, kur. 8-9

  • Fahirishi ya Machapisho

    w97 6/1 9

2 Wakorintho 13:9

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/1/1990, kur. 29-31

2 Wakorintho 13:10

Marejeo

  • +1Ko 4:21

2 Wakorintho 13:11

Marejeo

  • +2Ko 1:3, 4
  • +Flp 2:2
  • +1Th 5:13; Yak 3:17; 1Pe 3:11; 2Pe 3:14
  • +1Ko 14:33

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    11/2020, kur. 18-23

    Mnara wa Mlinzi,

    9/1/2008, uku. 5

    6/1/1996, uku. 25

    3/1/1991, kur. 21-22

    11/1/1990, kur. 29-31

  • Fahirishi ya Machapisho

    w08 9/1 5; w96 6/1 25

2 Wakorintho 13:14

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Utatu, uku. 23

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

2 Kor. 13:1Kum 19:15; Mt 18:16
2 Kor. 13:4Ro 6:4; 1Pe 3:18
2 Kor. 13:42Ti 2:11, 12
2 Kor. 13:41Ko 6:14
2 Kor. 13:51Ko 11:28; Gal 6:4
2 Kor. 13:101Ko 4:21
2 Kor. 13:112Ko 1:3, 4
2 Kor. 13:11Flp 2:2
2 Kor. 13:111Th 5:13; Yak 3:17; 1Pe 3:11; 2Pe 3:14
2 Kor. 13:111Ko 14:33
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
2 Wakorintho 13:1-14

Barua ya Pili kwa Wakorintho

13 Hii ni mara ya tatu ambayo ninakuja kwenu. “Kila jambo linapaswa kuthibitishwa kwa ushahidi wa* mashahidi wawili au watatu.”+ 2 Ingawa sipo sasa, ni kana kwamba nipo kwa mara ya pili, nami ninatoa onyo mapema kwa wale waliotenda dhambi mwanzoni na kwa wengine wote, kwamba ikiwa nitakuja tena sitawahurumia, 3 kwa kuwa mnatafuta uthibitisho kwamba Kristo, ambaye si dhaifu kuwaelekea ninyi bali ni mwenye nguvu kati yenu, kwa kweli anazungumza kupitia mimi. 4 Ni kweli kwamba aliuawa kwenye mti kwa sababu ya udhaifu, lakini yuko hai kwa sababu ya nguvu za Mungu.+ Ni kweli kwamba sisi pia ni dhaifu pamoja naye, lakini tutaishi pamoja naye+ kwa sababu ya nguvu za Mungu kuwaelekea ninyi.+

5 Endeleeni kujijaribu kama mko katika imani, endeleeni kuthibitisha jinsi ninyi wenyewe mlivyo.+ Au je, hamtambui kwamba Yesu Kristo yumo katika muungano pamoja nanyi? Isipokuwa muwe mmekataliwa. 6 Kwa kweli ninatumaini mtatambua kwamba hatujakataliwa.

7 Basi tunasali kwa Mungu kwamba msifanye kosa, si ili sisi tuonekane kuwa waliokubaliwa, bali mfanye yaliyo mema, hata tukionekana kwamba tumekataliwa. 8 Kwa maana hatuwezi kufanya jambo lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli. 9 Hakika sisi hushangilia kila mara tunapokuwa dhaifu lakini ninyi mna nguvu. Nasi tunasali kwamba mrekebishwe upya. 10 Hiyo ndiyo sababu ninaandika mambo haya nikiwa sipo, ili nitakapokuja, nisiwe mkali katika kutumia mamlaka ambayo Bwana alinipa,+ ili kujenga na si kubomoa.

11 Mwishowe, akina ndugu, endeleeni kushangilia, kurekebishwa upya, kufarijiwa,+ kufikiri kwa upatano,+ kuishi kwa amani;+ na Mungu wa upendo na amani+ atakuwa pamoja nanyi. 12 Salimianeni kwa busu takatifu. 13 Watakatifu wote wanawatumia salamu zao.

14 Fadhili zisizostahiliwa za Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na ushirika katika roho takatifu ziwe pamoja nanyi nyote.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki