Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wimbo wa Sulemani 4
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Wimbo wa Sulemani—Yaliyomo

    • MSHULAMI AKIWA YERUSALEMU (3:6–8:4)

        • 4 Mchungaji (1-5)

          • “Wewe ni mrembo, mpenzi wangu” (1)

Wimbo wa Sulemani 4:1

Marejeo

  • +Hes 32:1; Kum 3:12; Wim 6:5-7

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/15/2006, uku. 19

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 11/15 19

Wimbo wa Sulemani 4:4

Marejeo

  • +Wim 1:10
  • +Ne 3:25; Wim 7:4
  • +2Sa 8:7; 2Fa 11:10

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu, uku. 169

Wimbo wa Sulemani 4:5

Marejeo

  • +Wim 7:3

Wimbo wa Sulemani 4:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “siku ianze kupumua.”

Marejeo

  • +Mhu 2:5

Wimbo wa Sulemani 4:7

Marejeo

  • +Wim 4:1

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2015, uku. 30

    11/15/2006, uku. 20

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 11/15 20

Wimbo wa Sulemani 4:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Milima iliyo ng’ambo ya milima ya Lebanoni.”

Marejeo

  • +Kum 3:25
  • +Kum 3:8, 9; Zb 133:3

Wimbo wa Sulemani 4:9

Marejeo

  • +Met 5:18, 19

Wimbo wa Sulemani 4:10

Marejeo

  • +Wim 7:12
  • +Wim 1:2, 4
  • +Est 2:12; Wim 1:12

Wimbo wa Sulemani 4:11

Marejeo

  • +Met 16:24
  • +Wim 5:1

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2015, uku. 30

    11/15/2006, uku. 19

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 11/15 19

Wimbo wa Sulemani 4:12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    1/15/2015, uku. 32

    11/15/2006, uku. 20

    11/1/2000, uku. 11

    11/15/1987, uku. 25

  • Fahirishi ya Machapisho

    w06 11/15 20; w00 11/1 11

Wimbo wa Sulemani 4:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “Ngozi.”

  • *

    Au “bustani.”

Wimbo wa Sulemani 4:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Utete wenye harufu nzuri.

Marejeo

  • +Yoh 12:3
  • +Isa 43:24
  • +Met 7:17
  • +Zb 45:8
  • +Kut 30:23, 24, 34; Eze 27:2, 22

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    2/1/2014, uku. 10

Wimbo wa Sulemani 4:15

Marejeo

  • +Yer 18:14

Wimbo wa Sulemani 4:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Vumeni taratibu.”

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Wim. 4:1Hes 32:1; Kum 3:12; Wim 6:5-7
Wim. 4:4Wim 1:10
Wim. 4:4Ne 3:25; Wim 7:4
Wim. 4:42Sa 8:7; 2Fa 11:10
Wim. 4:5Wim 7:3
Wim. 4:6Mhu 2:5
Wim. 4:7Wim 4:1
Wim. 4:8Kum 3:25
Wim. 4:8Kum 3:8, 9; Zb 133:3
Wim. 4:9Met 5:18, 19
Wim. 4:10Wim 7:12
Wim. 4:10Wim 1:2, 4
Wim. 4:10Est 2:12; Wim 1:12
Wim. 4:11Met 16:24
Wim. 4:11Wim 5:1
Wim. 4:14Yoh 12:3
Wim. 4:14Isa 43:24
Wim. 4:14Met 7:17
Wim. 4:14Zb 45:8
Wim. 4:14Kut 30:23, 24, 34; Eze 27:2, 22
Wim. 4:15Yer 18:14
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Wimbo wa Sulemani 4:1-16

Wimbo wa Sulemani

4 “Tazama! Wewe ni mrembo, mpenzi wangu.

Tazama! Wewe ni mrembo.

Macho yako ni macho ya njiwa nyuma ya shela yako.

Nywele zako ni kama kundi la mbuzi

Washukao chini kwenye milima ya Gileadi.+

 2 Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi

Ambao wametoka kuoshwa,

Wote wamezaa mapacha,

Na hakuna yeyote aliyepoteza watoto wake.

 3 Midomo yako ni kama uzi mwekundu,

Na maneno yako yanapendeza.

Kama kipande cha komamanga

Ndivyo yalivyo mashavu yako nyuma ya shela yako.

 4 Shingo yako+ ni kama mnara wa Daudi,+

Uliojengwa kwa safu za mawe

Na ngao elfu zimetundikwa juu yake,

Ngao zote za mviringo za wanaume mashujaa.+

 5 Matiti yako mawili ni kama paa wawili wachanga,

Mapacha wa paa,+

Wanaolisha kwenye mayungiyungi.”

 6 “Mpaka upepo uanze kuvuma* na vivuli kukimbia,

Nitakwenda zangu kwenye mlima wa manemane

Na kwenye kilima cha ubani.”+

 7 “Wewe ni mrembo kabisa, mpenzi wangu,+

Huna kasoro yoyote.

 8 Njoo, bibi harusi wangu, tuondoke Lebanoni,

Njoo tuondoke Lebanoni.+

Shuka kutoka kilele cha Amana,*

Kutoka kilele cha Seniri, kilele cha Hermoni,+

Kutoka kwenye mapango ya simba, kutoka kwenye milima ya chui.

 9 Umeuteka moyo wangu,+ dada yangu, bibi harusi wangu,

Umeuteka moyo wangu kwa kunitupia jicho mara moja tu,

Kwa kidani kimoja cha mkufu wako.

10 Maonyesho yako ya upendo yanavutia kwelikweli,+ dada yangu, bibi harusi wangu!

Maonyesho yako ya upendo ni bora zaidi kuliko divai,+

Na manukato ya marashi yako yananukia kuliko kiungo chochote!+

11 Midomo yako, bibi harusi wangu, inadondosha asali ya sega.+

Chini ya ulimi wako kuna asali na maziwa,+

Na manukato ya mavazi yako ni kama manukato ya Lebanoni.

12 Dada yangu, bibi harusi wangu, ni kama bustani iliyofungwa,

Bustani iliyofungwa, chemchemi iliyofunikwa kabisa.

13 Machipukizi* yako ni paradiso* ya makomamanga

Yenye matunda bora kabisa, mimea ya hina na ya nardo,

14 Nardo+ na zafarani, kane*+ na mdalasini,+

Iliyo na miti ya kila aina ya ubani, manemane, na udi,+

Pamoja na marashi yote yaliyo bora kabisa.+

15 Wewe ni chemchemi ya bustani, kisima cha maji safi,

Na vijito vinavyotiririka kutoka Lebanoni.+

16 Amka, ewe upepo wa kaskazini;

Ingia, ewe upepo wa kusini.

Pumueni* kwenye bustani yangu.

Manukato yake na yaenee.”

“Mpenzi wangu na aje kwenye bustani yake

Ale matunda yake yaliyo bora kabisa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki