Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 5/8 kur. 3-4
  • Majeruhi au Wafia-Iman Kuna Tofauti Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Majeruhi au Wafia-Iman Kuna Tofauti Gani?
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu kwa Nini Makanisa Yalikaa Kimya
    Amkeni!—1995
  • Washika Uaminifu-Maadili Walio Wajasiri Washinda Mnyanyaso wa Nazi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Vita Huua Vijana Wengi
    Amkeni!—1997
  • Wafia-Imani wa Siku Hizi Watoa Ushahidi Nchini Sweden
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 5/8 kur. 3-4

Majeruhi au Wafia-Iman Kuna Tofauti Gani?

KUPITIA historia yote, ukatili wa binadamu kwa wanaume, wanawake, na watoto umesababisha taabu nyingi sana na kutokeza mamilioni ya majeruhi. Hata sababu iwe ni ya kisiasa, kitaifa, ya ubaguzi wa rangi, au ya kidini, damu isiyo na hatia imemwagwa na inaendelea kumwagwa. Chuki hushinda upendo na uelewano. Ushupavu hukandamiza uvumilio. Nayo mauaji yaendelea.

Katika karne zilizopita, vita vilikuwa ni baina ya jeshi na jeshi, na raia walihusika kidogo sana kwa kulinganisha. Katika karne yetu ya 20, kwa kutokezwa kwa mabomu ya kutupwa kutoka angani, makombora na silaha za masafa marefu, vifo vya raia vimepanda juu sana hivi kwamba uchunguzi mmoja ulisema hivi: “Raia ndio wanaouawa kwa kadiri kubwa sana vitani. Katika karne hii, raia wasiokuwa na silaha wameuawa zaidi ya wanajeshi halisi.” Watu wasiokuwa na hatia ambao maisha yao yaonwa kuwa si kitu wameuawa na vita vilivyoanzishwa na viongozi wa kisiasa. Katika karne yetu pekee, idadi ya wanaoathiriwa na vita imeongezeka sana, zaidi ya milioni mia moja wakiwa wamekufa na mamia ya mamilioni wakiumizwa sana moyoni na majeraha na vifo vya wapendwa wao.

Kwa kuongezea majeruhi wa vita vya siku-hizi, kumekuwa pia na wafia-imani.a Kuna tofauti gani kati ya majeruhi wa vita na wafia-imani? Mamilioni—Wayahudi, Waslavi, Wagipsi, wagoni jinsia-moja, na wengine—walikufa wakiwa majeruhi katika Ujerumani wa Nazi kwa sababu tu ya kuwa jinsi walivyokuwa. Hawakuwa na njia nyingine, hawakuwa na la kufanya. Chini ya mfumo huo mwovu, kifo chao hakingeepukika. Kwa upande mwingine, haikuwa lazima wengine wafe. Wangeepuka kifo, lakini, kwa sababu ya kanuni zao, waliamua wasiepuke kifo.

Mfano mmoja unaojulikana sana ulikuwa wa kasisi wa Katoliki Maximilian Kolbe, aliyesaidia wakimbizi Wayahudi wakati wa Vita ya Ulimwengu 2. Katika 1941 “alipelekwa [kwenye kambi ya mateso ya Nazi katika] Auschwitz, ambako alijitolea uhai wake badala ya mfungwa aliyehukumiwa Franciszek Gajowniczek. Kwanza alinyimwa chakula na kisha hatimaye alidungwa shindano ya fenoli [sumu] na mwili wake ukachomwa moto.” (Encyclopœdia Britannica) Akawa mfia-imani mwenye kujidhabihu—jambo lisilo la kawaida katika dini za Kiprotestanti na Kikatoliki.

Wakati wa enzi ya Nazi katika Ujerumani (1933-45), Mashahidi wa Yehova walinyanyaswa kikatili kwa kutokuunga mkono upande wowote na kwa kukataa kutumikia jitihada za vita ya Hitler. Maelfu walipelekwa katika kambi za mateso zenye kuogofya sana, ambako wengi waliuawa na wengine wakafa kwa kutendwa vibaya. Lakini haikuwa lazima wateseke na kufa. Wangeweza kuchagua. Walipewa njia ya kutokea. Ikiwa wangetia sahihi karatasi iliyokana imani yao, wangeachiliwa huru. Wengi sana walikataa kuitia sahihi na hivyo wakawa majeruhi wa ukatili wa Wanazi na vilevile wakawa wafia-imani. Kwa hiyo, ingawa wafia-imani wote ni majeruhi, ni wachache tu wa majeruhi wangeweza kuwa na ambao kweli walichagua kuwa wafia-imani. Walikuwa washindi wajapokabiliwa na kifo.

Ushuhuda usiopendelea upande wowote kutoka kwa wasio Mashahidi wathibitisha jambo hilo. “Pasta Mswisi Bruppacher alionelea katika 1939 kwamba ‘Huku watu wanaojiita Wakristo wakiwa wameshindwa katika majaribu makubwa, mashahidi hao wa Yehova wasiojulikana, wakiwa wafia-imani Wakristo, wanadumisha upinzani mkali dhidi ya kulazimishwa kwa dhamiri na ibada ya kilimwengu . . . Wanateseka na kufa kwa sababu, wakiwa Mashahidi wa Yehova na washiriki wa Ufalme wa Kristo, wanakataa ibada ya Hitler na Swastika.’”

Hata hivyo, si katika Ujerumani pekee ambako Mashahidi wa Yehova wamedumisha ushikamanifu wao wajapokabiliwa na kifo. Wamelazimika kuonyesha ujasiri wao wajapokabiliwa na Ukomunisti, Ufashisti, na aina nyingine ya uonevu wa kisiasa, pamoja na upinzani wa kidini. Hata katika zile nchi zinazoitwa eti za kidemokrasia za Magharibi, Mashahidi wamekabili ujeuri. Makala yetu inayofuata itaelezea kindani visa fulani ambavyo vimehusu Mashahidi waliopata ushindi wajapokabiliwa na kifo.

[Maelezo ya Chini]

a Mjeruhi ni “yule anayeumizwa au kuuawa na mwingine . . . Yule anayeumizwa au kufanywa ateseke kutokana na tendo, hali, kitu au jambo fulani.” Kwa upande mwingine, mfia-imani ni “yule ambaye anachagua kifo badala ya kuacha kanuni za kidini. . . Yule anayejidhabihu sana au kuteseka sana ili kuendeleza itikadi, kusudi, au kanuni fulani.”—The American Heritage Dictionary of the English Language, Toleo la Tatu.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Baada ya vita ya Ulimwengu 2, mahakama za Ujerumani Mashariki zilihukumia kimakosa Mashahidi wa Yehova kuwa wajasusi wa Amerika

[Hisani]

Neue Berliner Illustrierte

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki