Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/8 kur. 8-9
  • Mwono-Ndani Katika Akili na Ulimwengu wa Mwanabarafu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwono-Ndani Katika Akili na Ulimwengu wa Mwanabarafu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Hali ya Kidini
  • Historia ya Kale ya Binadamu na Biblia
  • Utafutaji kwa Ajili ya Mianzo
  • Vidokezo kuhusu lile fumbo la Mwanabarafu
    Amkeni!—1995
  • Ile Mami Ambayo Ilikuja Kutoka kwa Barafuto
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Dini Ilianzaje?
    Jitihada ya Ainabinadamu ya Kutafuta Mungu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 5/8 kur. 8-9

Mwono-Ndani Katika Akili na Ulimwengu wa Mwanabarafu

ACHENI tufikirie Ötzi tena. Je, alikuwa asiyestaarabika, mpumbavu, na asiye na hisia ya ujipambaji? Je, vyombo vyake, silaha zake, na nguo zake zafunua nini?

Silaha zake zafunua kwamba Ötzi alikuwa na ujuzi bora sana wa kurusha silaha. Mishale miwili iliyokamilika ilikuwa na manyoya yaliyo ya kawaida katika tako layo. Manyoya yaliwekwa gundi kwa mwegamo fulani ili kuufanya mshale uzunguke urushwapo, yakiruhusu kiasi cha kutosha cha usahihi kufikia mlengo wa meta 30. Nguo zake za ngozi (ngozi mbalimbali za wanyama) hutueleza jambo fulani kuhusu mapendezi ya wakati huo. Leo, vazi halihitaji kufunika tu bali pia kuridhisha matakwa hususa ya ujipambaji. Namna gani katika siku ya Ötzi? Likifafanua ugunduzi huo, gazeti Time lasema: “Joho lilikuwa limefumwa kwa ustadi kwa nyuzi za kano ama nyuzi za mmea, katika kile kilichoonekana kuwa usanii wa kimozeiki.” Nguo pamoja na namna ilivyoshonwa ilichangia katika kufanyiza “matokeo yafananayo na usanii wa kimozeiki,” kikasema kitabu Der Mann im Eis (Mwanamume kwenye Barafu). Juu ya vazi refu, Mwanabarafu alivaa “koti lililofumwa kwa nyasi, kwa wazi ili kumlinda kutokana na baridi, ambalo wakati wa pumziko lingeweza kutumiwa kama ‘godoro’ kuutenganisha mwili wake kutoka ardhini.”—Focus.

“Kiwango fulani cha utata ambacho hakikutazamiwa” katika vifaa vyake kilionekana pia, laeleza Time. Kwa kielelezo, lile jambia, lilikuwa kamili likiwa na “ala fulani iliyobuniwa vizuri, iliyotengenezwa kutoka kwa majani yaliyofumwa.” Mwanabarafu, wakati huo, yaonekana aliishi katika muhula fulani ambao kwa kweli ulikuwa “tajiri na wenye utamaduni mwingi,” kama vile Giovanni Maria Pace aufafanuavyo katika kitabu chake Gli italiani dell’Età della pietra (Waitalia wa Muhula wa Jiwe).

Pia ingeweza kutajwa juu ya uyoga uliopatikana karibu na Ötzi. Huenda ulitumika kuwashia moto, lakini yaelekea zaidi, wasema wastadi, Mwanabarafu alikuwa nawo kwa ajili ya mafaa ya kiuavijasumu na kitiba, kama sehemu ya aina ya “huduma ya kwanza” inayobebeka.”

Ladha ya usanifu wa kimapambo, kiasi cha uelewevu, ujuzi wa kitiba, na ujuzi katika nyanja za usonara, kilimo, na usanii—hizi zaonyesha, kinyume na taswira ambayo mara nyingi huwasilishwa, kwamba watu walioishi wakati mmoja na Mwanabarafu walikuwa wenye ujuzi na mahiri katika nyanja nyingi. Mwakiolojia Mwingereza Dakt. Lawrence Barfield ataarifu hivi: “Wachache wetu leo wana stadi zozote ambazo wengi wa watu wangekuwa nazo wakati wa mileani ya nne [K.W.K.].” Kwa kielelezo, ladha zao zilizochujwa zazuka katika mionyesho ya kisanaa na aathari za kimetali na kivigae zilizobukuliwa kutoka makaburini.

Hali ya Kidini

“Kwa kadiri ambavyo wasomi wamevumbua, hakujapata kuwa watu wowote, mahali popote, katika wakati wowote, ambao hawakuwa na hisia fulani za kidini,” yasema The New Encyclopædia Britannica. Ikisema juu ya fungu kubwa ambalo dini ilichangia katika nyakati za kale, Dizionario delle religioni (Kamusi ya Dini Mbalimbali) yasema kwamba “ikilinganishwa na zilizotumiwa katika maisha ya kila siku, kiasi kikubwa kisicholingana cha bidhaa na nguvu kilitumiwa katika miradi ya kidini.”

Mwelekeo wa kidini wa nyakati za Ötzi kwa wazi wadhihirika sana. Katika mahali kwingi, maeneo ya kale ya kuzika yamepatikana yanayodhihirisha unamna na utajiri wa kanuni za ibada za mazishi. Dazani za viumbo vya udongo vimepatikana pia ambavyo vinaonyesha miungu iliyokuwa ya jamii za kale.

Historia ya Kale ya Binadamu na Biblia

Staarabu zilizozuka kutoka kwa utafiti katika nyakati za kale, zilikuwa tata mno. Picha yenyewe si ya mng’ang’ano wa ustaarabu, miongoni mwa matatizo elfu, ili kufanya maendeleo yasiyowazika kuelekea jamii fulani ya watu iliyoumbika kabisa. Kwa kadiri wanahistoria wahusikavyo, jamii za watu zilikuwa na ukubwa mbalimbali lakini zilizoumbika kabisa.

Hili lina umaana kwa yeyote anayejifunza Biblia. Kitabu cha Mwanzo chaonyesha kwamba mapema sana katika historia ya binadamu—na hasa kadiri jamii ya kibinadamu ‘ilipotapakaa kote kwenye uso wa dunia’—ustaarabu tata na ulioumbika kabisa ulitokea, watu walioufanyiza walikuwa na uwezo wa uelewevu na wa kiroho.—Mwanzo 11:8, 9.

Biblia huthibitisha kwamba uwezo wa kiufundi na wa kisanaa ulihodhiwa na jamii ya kibinadamu hata katika nyakati za mapema mno, kama vile uhunzi wa “kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma.” (Mwanzo 4:20-22) Kulingana na rekodi ya Biblia, wanadamu sikuzote wamekuwa na tamaa ya kuabudu kiabudiwa fulani. (Mwanzo 4:3, 4; 5:21-24; 6:8, 9; 8:20; Waebrania 11:27) Ingawa hivyo udini wake ulidhoofika kadiri wakati ulivyopita, mwanadamu abaki “bila ponyo la kidini,” yasema The New Encyclopædia Britannica.

Utafutaji kwa Ajili ya Mianzo

Ingawa utafiti wa waakiolojia hauwezi kujibu maswali yote yaliyotokezwa na uvumbuzi wa Ötzi, hata hivyo umetuwezesha kupata uelewevu fulani wa ulimwengu alimoishi—ulimwengu tata, ulio tofauti sana na ile taswira ya kawaida ya zile ziitwazo eti nyakati za kabla ya historia. Ilikuwa ya kisasa zaidi kuliko wengi waaminivyo.

Kwa kumalizia, mbali na hakika zilizodondolewa kutoka kwa wonekano na mali ya Mwanabarafu, kama vile National Geographic lilitaarifu, “karibu kila kitu kingine kumhusu ni sehemu fumbo, sehemu udadisi.” Kwa sasa, Ötzi alala katika chumba fulani baridi katika Innsbruck, Austria, zaidi ya mamlaka 140 za taaluma mbalimbali zikiwa zingali zang’ang’ana kutatua mafumbo zaidi ya Mwanabarafu aliyekuja kutoka kwenye baridi.

[Picha katika ukurasa wa 8]

Wastadi wa balagha wachunguza mwili wa Mwanabarafu katika Innsbruck

[Hisani]

Foto: Archiv Österreichischer Alpenverein/Innsbruck, S.N.S. Pressebild GmbH

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki