Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/8 kur. 3-4
  • Ubuni wa Sayansi—Kuzuka Kwao Kufikia Umaarufu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ubuni wa Sayansi—Kuzuka Kwao Kufikia Umaarufu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ubuni Wawa Uhalisi
  • Kutazama Ubuni wa Sayansi wa Leo
    Amkeni!—1995
  • Kile Ambacho Wakati Ujao Unacho Hasa
    Amkeni!—1995
  • Waweza Kuitumaini Sayansi Kadiri Gani?
    Amkeni!—1998
  • Kupatanisha Sayansi na Dini
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 12/8 kur. 3-4

Ubuni wa Sayansi—Kuzuka Kwao Kufikia Umaarufu

MWAKA wa 1982 uliona jambo moja lililokuwa la kwanza kwa biashara ya sinema ya Marekani. Wakati wa msimu wa 1982/83, filamu iliyo maarufu zaidi “perfomer” hakuwa mtu halisi kamwe. Kulingana na The Illustrated History of the Cinema, alikuwa ET, mhusika wa kuwaziwa lakini mwenye kupendeza kutoka anga za nje ambaye alinawiri katika ile filamu ET: The Extraterrestrial!

Hali hii ya kipekee ni uthibitisho mmoja tu wa umaarufu usio na kifani ambao ubuni wa sayansi (SF) umefurahia katika miaka ya hivi majuzi. Mbeleni ukionwa kuwa habari ya magazeti ya hali ya chini na kufikiriwa kuwa habari ya kufurahisha wapweke na waota-ndoto, ubuni wa sayansi umekuwa sehemu kuu ya vitumbuizo kwa watu wengi. Lakini ni nini kinachochochea kuzuka kwao kwenye kutazamisha katika umaarufu?

Ili kujibu swali hili, kwanza ni lazima tuchunguze historia ya ubuni wa sayansi. Tangu zamani za kale watu wamesimulia visakale murua ili kutisha, kupendeza, au kutumbuiza tu. Hata hivyo, wakati wa karne ya 17 na 18, Ulaya iliingia muhula wa maendeleo ya kisayansi na mali za kimwili. Wengi walianza kupinga maoni na mamlaka za kidesturi. Katika hali hii wengine walianza kukisia-kisia kuhusu jinsi maendeleo ya kisayansi yangeathiri wanadamu wakati ujao.

Kujua ni nani hasa aliyeanzisha ubuni wa sayansi ni jambo lisilo hakika. Watungaji wa vitabu wa karne ya 17 Francis Godwin na Cyrano de Bergerac waliandika vitabu vya ubuni ambavyo vilihusisha safari za anga. Katika 1818, kitabu cha Mary Shelley, Frankenstein, or The Modern Prometheus kilionyesha mwanasayansi akiwa na uwezo wa kuumba uhai na kilionyesha yale matokeo yenye kuogofya.

Waandikaji wengine walitumia aina hii ya ubuni kutokeza mapungukio ya jamii ya binadamu. Kwa hiyo Jonathan Swift alipoifanyia mzaha jamii ya Waingereza ya karne ya 18, alitoa kinaya chake katika mifululizo ya safari za baharini za kubuni. Tokeo lilikuwa Gulliver’s Travels, istiara yenye kuchambua ambayo imeitwa “uandishi wa kwanza” wa ubuni wa sayansi.

Lakini waandikaji Jules Verne na H. G. Wells kwa kawaida husifiwa kwa kuweka riwaya ya ubuni wa sayansi katika hali yake ya kisasa. Katika 1865, Verne aliandika From the Earth to the Moon—moja ya mfululizo wa riwaya zenye kufanikiwa. Katika 1895, kitabu maarufu cha H. G. Wells The Time Machine kilitokea.

Ubuni Wawa Uhalisi

Kufikia mapema miaka ya 1900, wanasayansi walikuwa wameanza kufanya ndoto hizi kuwa kweli. Kulingana na kitabu Die Großen (Walio Wakubwa), mwanafizikia Mjerumani Hermann Oberth alitumia miaka mingi kujaribu kuifanya ndoto ya Jules Vernes ya kuruka katika anga za nje kukifanywa na wanadamu kuwa uhalisi. Makadirio ya Oberth yalisaidia kuweka msingi wa kisayansi wa kusafiri angani. Hata hivyo, hakuwa mwanasayansi pekee ambaye aliathiriwa na ubuni wa sayansi. Asema mwandikaji maarufu wa ubuni wa sayansi Ray Bradbury: “Wernher von Braun na wenzake katika Ujerumani na kila mtu katika Houston na Cape Kennedy walisoma vitabu vya H. G. Wells na Jules Verne walipokuwa watoto. Waliamua kwamba wakati wangekuwa wakubwa, wangeyafanya yote yatimie.”

Kwa hakika, ubuni wa sayansi umekuwa kikanyagio kuelekea uvumbuzi katika nyanja nyingi. Mtungaji René Oth adai kwamba kumekuwa na ‘mavumbuzi au magunduzi machache mno ambayo ubuni wa sayansi haukutabiri kimbele.’ Nyambizi, roboti, na roketi zenye kubeba binadamu zote hizi zilikuwa bidhaa za ubuni wa sayansi muda mrefu kabla hazijakuwa halisi. Mwandikaji wa ubuni wa kisayansi Frederik Pohl hivyo ashikilia kwamba “kusoma vitabu vya ubuni wa sayansi ni kupanua akili.”

Bila shaka, si ubuni wote wa sayansi ambao kwa kweli huhusu sayansi. Baadhi ya vitabu na filamu maarufu zaidi kuhusu ubuni wa sayansi kwa hakika ni aina za kile wengine huita fantasia ya sayansi. Uhalisi wa kisayansi mara nyingi huwa ndio lengo kuu la ubuni wa sayansi, ilhali masimulizi ya fantasia huwekewa mipaka tu na mawazio ya watungaji wazo. Kiinimacho na ulozi huenda hata zikahusika.

Hata hivyo, maoni ya ubuni wa sayansi ya wakati ujao ni sahihi kadiri gani? Je, ubuni wote wa sayansi wastahili kusomwa au kutazamwa? Makala zifuatazo zitazungumzia maswali haya.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Riwaya ya Jules Verne “From the Earth to the Moon” ilichangia sana kuamsha upendezi wa kusafiri angani

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Rocket Ship: General Research Division/The New York Public Library/Astor, Lenox and Tilden Foundations

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki